TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

Hivi kazi ya yale ma Airbag huwa nini hasa kwenye ma V8? Sababu ukiangalia wapoonyesha crash testing kuyatangaza unajua hata ukiwa spidi 200 ukagonga treni lazima utoke salama
Hayo machuma waliyogonga si yanayatoboa tu hata kabla collision haijaisha
 
Atasema steshen zote za redio na television nchini zina majina mengi ya vipindi kwa lugha hiyo
🤣🤣🤣🤣
Sawa mkuu, lakini hizo steshen za Radio ni kwa ajili ya watu wote yaani Watanzania na wageni
 
Siku hiizi magari mengi ya serikali yanabandikwa namba binafsi fake, jirani yangu anaishi Kibaha gari yake ilionekana inadaiwa faini kwa makosa yaliyofanywa Mwanza kama sikosei Arusha wakati haijawahi kwenda huko, jamaa akaomba jina la dereva aliyekuwa na hilo gari, akapewa akaenda fb akalitafuta akafanya urafiki na huyo jamaa baada ya kumdodosa akamblock
Hii ni hatari
 
Hakuna tulipomkosea Mungu mpaka siku serikali itapo amaua kushughulikia made madereva wake wanaoendesha hovyo bila tahadhari.
Funga speed control, gari ikipaishwa ijizime. Track mwendo, adhibu dereva akikimbiza. Nadhani teknolojia hizo zote zipo.
 
daa we jamaa
kauli za kiswahili kabisa izi
yani huna habari wewe ndo mwenye jukumu la kwanza kulinda uhai wako😳
 
Ila kuwa na kadi lazima. Hulambi hicho cheo kama siyo kijani
Si kweli...

Unafanya "generalization"...

Kuna wasio na kadi na wasio wanaCCM...bali nijuacho tu ni kuwa hawajihusishi na SIASA na kubwa "hawapingi maamuzi ya CCM"....

Kwa hiyo kutoipinga CCM ndiyo umekuwa mwanachama kindakindaki ?!!
 
Mhandisi Nyamohanga Gissima Mkurugenzi wa TANESCO na Dereva wake ambaye jina lake ni Muhajir Mohamed Haule, wamefariki Dunia kwenye Ajali liyyotokea saa nane Usiku wakiwa njiani kuelekea Msoma. Walikuwa wanakaribia Serengeti
View attachment 3302678View attachment 3302679
Picha hapa juu ni Muhajir Mohamed Haule, Dereva wa TANESCO wakati wa Uhai wake

Wapumzike kwa amani

"Tunayaangaza maisha yako"

TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA, SIMU 180

TAARIFA KWA UMMA

TANZIA

Jumapili, 13 Aprili 2025.

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo tarehe 13 Aprili 2025 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.

Bodi ya Wakurugenzi inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wa TANESCO, na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi na shughuli nyingine za maombolezo zitatolewa kadri mipango inavyoendelea kuratibiwa.

Imetolewa Na:

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA

WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA

====

MY TAKE

Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.

Huu mzinga sio poa aisew dereva alikuwa 240km/h nini
 
Ngoja niwape siri;

1. Magari ya serikali na taasisi zake yanapaswa kusafiri mwisho saa 12 jioni, ila mabosi walio wengi wanaforce, mabosi kibao wanatingwa na adhoc zisizoisha such that kwenye safari hajui anaondoka saa ngapi, most of them wanalazimika kusafiri usiku. Wakisema waondoke na Air Tanzania ndo hao abiria mnajikuta ratiba ya safari inabadilishwa kuwasubiri.

2. Huyo dereva angepona angekiona cha mtema kuni, maana wadogo ndiyo huadhibiwa zaidi, wakubwa hukingiana kifua. Hapo dereva hana say bosi akisema twende mnaenda! Anytime, anywhere

3. Magari ya serikali na taasisi zake yanakimbia mnoooooo! Sijui mnanielewa? Kwa speed wanayopendaga kwenda anything minor kikitokea can lead to a catastrophic disaster, ndo maana wanakufa sana. Ukiachana na kufa wanapata sana ajali, probably kuliko category nyingine yeyote ya vehicles za barabarani.

Umewahi kusikia magari ya NGO yanapata ajali, say AMREF, FAO, sijuo UN, mbona yapo mengi sana na wanasafiri sana long distances?, ni yana nidhamu, maana ofisi zao zinacontrol speed na location za magari! Dereva anaweza kupoteza kazi, so afisa huna say, dereva akisema gari inapark, inapark!!!

4. Mabosi kufasiri kwa ndege would lead to gharama kubwa sana za kuendesha ofisi za serikali. Fungu za hizi idara ni ngumu sana kusema waweke na gharama za usafiri wa anga na vile hapa tz ni very expensive, these people wanasafiri sana pia, probably several time a month. Kwa gari tu hapo usishangae yeye na dereva na mafuta ofisi ikalipa hata 5m kwa safari ya siku 5. Akifika kule atahitaji gari, wanaoendaga kwa ndege magari yanawafuata chini. After all ndege ya nini kama ofisi ina gari na dereva anayelipwa kila mwezi kwa kazi hiyo, hamuoni kama ni kuongeza gharama zinazoepukika?

Ushauri: Nyie mlio juu ya hawa mabosi acheni kuwapa pressure zisizo na maana. Kama ana safari mwache ajiandae na aendelee na safari yake salama. Hizo calls za ghafla mara waziri anataka hiki, mara Katibu Mkuu anataka hiki, mara fulani kaagiza hili ni kukosa mipango mizuri ya kazi, why can't you coordinate schedules zenu ili kuheshimu ratiba ya kila mmoja wenu?. Stop the nonsense ad-hoc issues.

Halafu, wewe kama ni bosi, kuna shida gani ukichelewa event kama aliye juu yako alikuchelewesha? Wait for a proper time, control speed ya dereva na make sure analala vya kutosha! Madereva wengi macho mekundu almost meusi indicating hawalani hawa watu, na you trust this person na maisha yako? Pathetic.

Usingizi ni takwa na asili la binadamu yeyote, akilimbikiza mwili utamlazimisha tu alale au asifunction vizuri, so maamuzi ya ovyo yasikushangaze. Na usiku ni wa kulala siyo kusafiri, unless dereva alilala 8 hours mchana.

Kuamini kuna uchawi hapa ni kudisplay tu imani zako za kishirikina.

Anyway, RIP. Gone too soon.
Exquisite comment!

Kudos !!
 
Tatizo kubwa pia ni barabara. Lanes zinapozidi kuwa zaidi ya nne zina punguza sana ajali.za kijinga.

Hili la kuovertake unakutana na gari inakuja unapoenda ni la kizamani sana na hatarishi. Pesa zijenge barabara za kueleweka
 
Useless explanation! Kama umewahi kusoma kitabu cha Kusadikika cha Shaaban Robert basi utakuwa ulikutakana na watu wanaoitwa wasadikika ambao waliishi miaka mingi iliyopita, na walikuwa na mawazo kama yako. Kama hujui siku ya kufa ndiyo usichukuwe tahadhari na kufuata kanuni za maisha salama? Mbona ukiugua unakimbilia hospital?
Ha ha ha ha
 
Hapana jamaa ni Mkurya wa Tarime karibu na kwaGachuma njia ya kwenda Nyamongo. Gissima Nyamo-hanga. Hiyo Nyamo-Hanga ilikosewa na mwalimu wakati wa uhandikishaji wa majina shuleni, badala ya kuandika Nyamhanga yeye akaandikq Nyamo-hanga.

Class mate wangu tokea Sekondari hadi chuo kikuu UDSM. Waliopata bahati ya kutoondolewa kwenye ile mgomo pale UDSM kipindi kile cha Rais Mwinyi. Wengine tulirudia mwaka wakatutangulia kuhitimu.
Kumbe jamaa ni mrundi
 
Back
Top Bottom