TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

TANZIA Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wafariki dunia

eneo la nyatwali ni hifadhi ya serengeti na kuanzia geti la maliasili pale lamadi hadi mizani ya tanroad ni speed limit ya 50kph, na kibao kipo na tulishapigwa faini sana, huyu shofeli wa boss angefuata sheria hii dhahama isingetokea, achilia kugonga lori angeweza kugonga Tembo fisi nyani, pale daraja la lubana na hotel ya serengeti stop over huwa kuna nyani wengi, hapo ni corridor ya wanyama kwenda kunywa maji ziwani hasa usiku wa manane utakutana na makundi ya tembo nyati fisi pofu

mie nashauri, TAWA waweke gate pale dabaga magari yalipe na yakaguliwe, wakati wa jiwe na mpina TAWA waliweka ukaguzi wakawa wana kamata vibambala, tuweke ushuru wa elfu 2000 kwa kila gari inayopita hapo, pia TAWA waweke speed detector, kwa anaezidisha speed alipe faini ya elfu 30,
 
Mungu aliye wa haki awape marehemu stahiki zao.Tunakushukuru Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi nao na kufurahia matunda ya kazi na sawa umeamua kuwatwaa.Tunakuomba Mungu wetu S.W uwafariji wanafamilia na marafiki wa marehemu.Amina
 
Hapana jamaa ni Mkurya wa Tarime karibu na kwaGachuma njia ya kwenda Nyamongo. Gissima Nyamo-hanga. Hiyo Nyamo-Hanga ilikosewa na mwalimu wakati wa uhandikishaji wa majina shuleni, badala ya kuandika Nyamhanga yeye akaandikq Nyamo-hanga.

Class mate wangu tokea Sekondari hadi chuo kikuu UDSM. Waliopata bahati ya kutoondolewa kwenye ile mgomo pale UDSM kipindi kile cha Rais Mwinyi. Wengine tulirudia mwaka wakatutangulia kuhitimu.
Kuna mswahili mmoja aliweka hiyo taswira labda kutokana na Jina kukosewa
 
dereva hana makosa, alikuwa anaambiwa na bosi wake kuwa anawahi musoma so achochee moto kadri awezavyo. Na asipotii amri ya mkuu wake anapoteza ajira yake. Wapumzike kwa amani.
Ulikuwepo
 
Inawezekana, kwa umri wake pamoja na nyadhifa na majukumu yake unaweza kuwa sahihii. Pia kumbuka kuna wengine ni wanachama wa ccm ila hawahusiki kwenye mambo ya chama ata kulipia kadi ya mwanachama anashangaa tu analipiwa.
Tumempoteza mtu wise sana na mtu anaeamini katika kusoma vitabu ili kuongeza maarifa.
Pumzika kwa amani Eng. Gissima, homeboy Maswi pole sana kwa kumpoteza rafiki.
Kwa supidii ya dereva wake hukutumia busara kumuona Dereva, aende supidi yenye hadhari
 
Matokeo ya manung'uniko ya watanzania kuhusu gharama kubwa ya umeme wakati mradi mkubwa wa umeme wa JNHEPP umekamilika ambao ungepunguza gharama ya kununua umeme.mfano ilitakiwa umeme wa elftano tupate uniti miamoja kama ilivyo Burundi na Djibouti
Kumbuka maharage allsha sema hata JNHEPP likikamilika 100 ,gharama za umeme zitabaki palepale ili kufidua mkopo kutoka (china)
 
Kupitia hizo picha inaonekana ni collision kwa nyuma..Lori limepaki barabarani pengine bila kuwasha indicators au kuweka alama kuashiria limesimama..utii wa sheria za barabarani kwa watanzania ni mdogo sana..hali ya kutokujali ni ya kiwango cha juu sana!
RIP Dereva na Eng. Gissing.
IMG-20250413-WA0005.jpg
 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme TANZANIA yaani TANESCO , Mhandisi Gissima Nyamuhanga Jana Usiku alipata Ajali ya Gari na kufariki hapo hapo, akiwa anatokea mikoa ya Kanda Ya Ziwa. pia Dereva wake naye amefariki,

Hizi ajali Tanzania zimekuwa zikimaliza watu, kwakweli sijui tufanye kitu Gani, naomba serikali iweke nguvu kutengeneza double road Barabara zote zinazounga mikoa na wilaya kama ilivyo nchini china au ulaya
R.I.P Gissima
Zinatakiwa tafiti zifanyike zije na mapendekezo ya nini kifanyike! Labda vyombo...labda madereva...labda barabara zenyewe... Tuwekeze kwenye tafiti Ili kupata suluhisho!

RIP Gissima Nyamohanga!
 
Mhandisi Nyamohanga Gissima Mkurugenzi wa TANESCO na Dereva wake ambaye jina lake ni Muhajir Mohamed Haule, wamefariki Dunia kwenye Ajali liyyotokea saa nane Usiku wakiwa njiani kuelekea Msoma. Walikuwa wanakaribia Serengeti
View attachment 3302678View attachment 3302679
Picha hapa juu ni Muhajir Mohamed Haule, Dereva wa TANESCO wakati wa Uhai wake

Wapumzike kwa amani

"Tunayaangaza maisha yako"

TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA, SIMU 180

TAARIFA KWA UMMA

TANZIA

Jumapili, 13 Aprili 2025.

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kilichotokea leo tarehe 13 Aprili 2025 kufuatia ajali ya gari iliyotokea katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara.

Bodi ya Wakurugenzi inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wa TANESCO, na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi na shughuli nyingine za maombolezo zitatolewa kadri mipango inavyoendelea kuratibiwa.

Imetolewa Na:

KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA

WATEJA TANESCO MAKAO MAKUU DODOMA

====

MY TAKE

Tanzania tumemkosea nini Mungu? Kwanini tukipata Mchapakazi hadumu kwenye Uongozi anafariki Dunia? Inabidi tuliombee Taifa. Nampongeza Nyamohanga kwa kulitendea haki taifa. Alijuwa mchapakazi na mwenye IQ kubwa pia ameachia Vitu vingi na kafanya vitu vingi TANESCO sio Kama yule Maharage na Kampani yake. Nahisi kuna mkono wa mtu.

Dereva yeye Hana bodi ya kumtangaza?!

Hakuwa mwajiliwa wa tanesco ili na yeye atokelezee kwenye barua?!

Au nguvu kazi iliyopotea ilikuwa ni mkurugenzi tu???
 
Ndio asafiri SAA nane ya usiku? Kuendesha Gari usiku ni hatari sana kwa dereva, abiria, chombo chenyewe na watumiaji wengine wa barabara.
Ndio maana kwenye taasisi zinazoongozwa na watu wenye akili wanakuwa na kitu kinaitwa journey management kabla ya kuanza safari yoyote.

Anaonyesha safari itaanza asubuhi ya SAA ngapi, mtapita njia ipi? Barabara mtakayoitumia ikoje? Mtakula wapi? Mtalala wapi? Etc.

Unapoendesha Gari kukiwa na mwanga wa Asili, dereva huona vizuri na akili inakuwa active.

Kuendesha SAA nane usiku ni hatari sana, boss kalala, dereva anaendesha huku kasinzia
Sahihi sana. Bado sio sahihi kwa mtu mkubwa kama huyu kusafiri usiku wa manane, why? Tena njia ya mbugani? Very sad. Mashirika mengi ya umma yaende yakajifunze kampuni binafsi, hawaruhusu hili jambo hata kidogo. RIP mkurugenzi wa Tanesco
 
Back
Top Bottom