Ngoja niwape siri;
1. Magari ya serikali na taasisi zake yanapaswa kusafiri mwisho saa 12 jioni, ila mabosi walio wengi wanaforce, mabosi kibao wanatingwa na adhoc zisizoisha such that kwenye safari hajui anaondoka saa ngapi, most of them wanalazimika kusafiri usiku. Wakisema waondoke na Air Tanzania ndo hao abiria mnajikuta ratiba ya safari inabadilishwa kuwasubiri.
2. Huyo dereva angepona angekiona cha mtema kuni, maana wadogo ndiyo huadhibiwa zaidi, wakubwa hukingiana kifua. Hapo dereva hana say bosi akisema twende mnaenda! Anytime, anywhere
3. Magari ya serikali na taasisi zake yanakimbia mnoooooo! Sijui mnanielewa? Kwa speed wanayopendaga kwenda anything minor kikitokea can lead to a catastrophic disaster, ndo maana wanakufa sana. Ukiachana na kufa wanapata sana ajali, probably kuliko category nyingine yeyote ya vehicles za barabarani.
Umewahi kusikia magari ya NGO yanapata ajali, say AMREF, FAO, sijuo UN, mbona yapo mengi sana na wanasafiri sana long distances?, ni yana nidhamu, maana ofisi zao zinacontrol speed na location za magari! Dereva anaweza kupoteza kazi, so afisa huna say, dereva akisema gari inapark, inapark!!!
4. Mabosi kufasiri kwa ndege would lead to gharama kubwa sana za kuendesha ofisi za serikali. Fungu za hizi idara ni ngumu sana kusema waweke na gharama za usafiri wa anga na vile hapa tz ni very expensive, these people wanasafiri sana pia, probably several time a month. Kwa gari tu hapo usishangae yeye na dereva na mafuta ofisi ikalipa hata 5m kwa safari ya siku 5. Akifika kule atahitaji gari, wanaoendaga kwa ndege magari yanawafuata chini. After all ndege ya nini kama ofisi ina gari na dereva anayelipwa kila mwezi kwa kazi hiyo, hamuoni kama ni kuongeza gharama zinazoepukika?
Ushauri: Nyie mlio juu ya hawa mabosi acheni kuwapa pressure zisizo na maana. Kama ana safari mwache ajiandae na aendelee na safari yake salama. Hizo calls za ghafla mara waziri anataka hiki, mara Katibu Mkuu anataka hiki, mara fulani kaagiza hili ni kukosa mipango mizuri ya kazi, why can't you coordinate schedules zenu ili kuheshimu ratiba ya kila mmoja wenu?. Stop the nonsense ad-hoc issues.
Halafu, wewe kama ni bosi, kuna shida gani ukichelewa event kama aliye juu yako alikuchelewesha? Wait for a proper time, control speed ya dereva na make sure analala vya kutosha! Madereva wengi macho mekundu almost meusi indicating hawalani hawa watu, na you trust this person na maisha yako? Pathetic.
Usingizi ni takwa na asili la binadamu yeyote, akilimbikiza mwili utamlazimisha tu alale au asifunction vizuri, so maamuzi ya ovyo yasikushangaze. Na usiku ni wa kulala siyo kusafiri, unless dereva alilala 8 hours mchana.
Kuamini kuna uchawi hapa ni kudisplay tu imani zako za kishirikina.
Anyway, RIP. Gone too soon.