Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Zile trillions za ma Profesa Mruma na Ossoro zimefia wapi?

Tundu Lissu alisema ule ulikuwa upuuzi mkubwa akaitwa majina yote.. Sasa kiko wapi?
Tujifunze kusikiliza upande wa pili.. Tanzania ni moja..
Tumeufyata mikia ndani huku "Mabeberu"" wakicheka kuelekea bank

..ukisikiliza hotuba ya Prof.Kabudi ni kwamba makubaliano haya yametokana na "hisani" na "huruma" ya mabeberu wa barrick.

..Prof.Kabudi anakiri kuwa alishindwa. Kuna wanasheria walikuwa wameweka msimamo.

..sasa hiyo maana yake ni kwamba serikali ilikuwa haina hoja zenye uzito wa kisheria dhidi ya accacia na barrick.

..CCM ndiyo waliotuingiza ktk hasara na fedheha hii. Wao ndiyo waliopitisha sheria mbaya za madini na nishati. Ni serikali za CCM ndizo zilizosaini mikataba mibovu ya kinyonyaji.

..Kwa miaka kadhaa CCM na mawakala wao walikuwa wakitetea mikataba mibovu ya madini.Walipaswa kuamka mapema na siyo miaka 20 baadae.
 
Mkuu barrick walikua wanasafirisha dhahab iliyochenjuliwa tayar wakiichanganya na makinikia ili kukimbia kodi,ndomana ishu ilibumburuka,ila kwa maana ya makinikia kama makinikia,ni ngum sana kukuta kiasi king hvyo cha dhahab

Ulikua ni mchezo mchafu walicheza barrick
Nadhani ni Accasia na sio Barrick waliokua wakicheza mchezo huo.
 
Mnalazimisha wapinzani waonekane si chochote ilhali tuliokuwepo miaka hiyo watu wakinyang'anywa maeneo yao ya uchimbaji madini,waliopinga mfumo huo waliitwa majina na kuonekana wanakwamisha maendeleo.

Mlipogundua ukweli mkakurupuka na kuzuia makinikia,mkasema tutalipwa US $ 190mil,wapinzani waliwaonya kuwa hatulipwi na tunaweza kushtakiwa mkwaita tena kuwa ni wasaliti,leo mnakuja tena na maneno mengi kuwa wapinzani wameumbuka.Mnaenda na mdundo wa ngoma ya manju wenu.

CCM/Watawala wetu wanatuhadaa,mikataba yenye maslahi ya kitaifa mnafanya SIRI,yakiwashinda mnalia na wapinzani.@Titicomb,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnalazimisha wapinzani waonekane si chochote ilhali tuliokuwepo miaka hiyo watu wakinyang'anywa maeneo yao ya uchimbaji madini,waliopinga mfumo huo waliitwa majina na kuonekana wanakwamisha maendeleo.Mlipogundua ukweli mkakurupuka na kuzuia makinikia,mkasema tutalipwa US $ 190mil,wapinzani waliwaonya kuwa hatulipwi na tunaweza kushtakiwa mkwaita tena kuwa ni wasaliti,leo mnakuja tena na maneno mengi kuwa wapinzani wameumbuka.Mnaenda na mdundo wa ngoma ya manju wenu.
CCM/Watawala wetu wanatuhadaa,mikataba yenye maslahi ya kitaifa mnafanya SIRI,yakiwashinda mnalia na wapinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijui kama unajibu kulingana na hoja au unajibu kulingana na hisia?
Hatutaweza kufanya mjadala na wewe, tufanye hivi wewe upo sahihi mimi na tunaosifia jitihada za serikali kwenye sakata la madini hatupo sahihi.
Mwisho wa mjadala.
 
Kwa ushauri wako tufanye nini kama CCM ni tatizo hapa Tanzania?
1. Tuchague viongozi wa Chama kingine chenye Sera na viongozi tofauti.
2. Tuandike Katiba ya Wananchi ili mikakati na vipaumbele vya maendeleo viwekwe sawa.
3. Tutafute haki,maridhiano na kuepuka visasi kama Taifa.
4. Tujenge nchi bila ubaguzi wa dini,kikabila,kikanda,kivyama na aina nyingine za ubaguzi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu;
Soma vizuri na uelewe maoni yangu!

Ni wapi nimesema huo ni mchanga kama mchanga wa kawaida?

Nimesem, ''Tuliambiwa na baadhi ya ‘’wataalam wa madini’’ nchini kuwa ule ni mchanga hauna thamani kama ambavyo serikali kupitia Rais Magufuli wanadai!
Ile taarifa ya Yule mkurugenzi wa TPA ilikuwa over exaggerated, kuwa kuna dhahabu nyingi,

Baadaye ikafutiwa na ripoti feki ya akina Mruma na Ossoro kuwa makinikia yana dhahabu nyingi,

Kwa takwimu hizi kama dhahabu na madini mengi yaliyomo kwenye makinikia ni Tshs.bill. 687 bado ni hela ndogo sana

Lissu alisema migodi inatoa 70% na makinikia yanatoa 30% kwa hiyo dhahabu nyingi inaondokea migodini siyo kupitia makinikia

Akasema sisi tunaibiwa na kunyonywa kwenye mikataba wala siyo kwenye makinikia tu.

Naona MATAGA mmeanza kushangilia bila kufanya tafakuli kama kawaida yenu

Niwaulize Maswali

je unadhani Yale makinikia yalikuwa ni container ngapi? Au ni batch ya muda gani
Isijekuwa ilikuwa batch ya mwaka mzima?

je estimate za TMA zilikuwa sahihi kulinganisha na za barick au kuna tofauti?

Je tofauti ya data za TMA, Ossoro, Mruma na bariki ni IPI?
 
Zile trillions za ma Profesa Mruma na Ossoro zimefia wapi?

Tundu Lissu alisema ule ulikuwa upuuzi mkubwa akaitwa majina yote.. Sasa kiko wapi?
Tujifunze kusikiliza upande wa pili.. Tanzania ni moja..
Tumeufyata mikia ndani huku "Mabeberu"" wakicheka kuelekea bank
Nani amesema Tanzania sio moja? Hii statement inaonyesha inferiority complex! Wewe jenga tu hoja zako kama zina nguvu za hoja basi zitasimama!

Hizo trillions za ma Profesa Mruma na Ossoro zimefia kwenye majadiliano ambayo yamefikia mwafaka kwa kutiliana saini za makubaliano.

Msingi wa majadiliano yoyote ya maana unajengwa katika msingi wa mutual concessions and compromises.

Kama serikali ingetaka kuzipata hizo pesa basi ingeenda mahakamani ambako msingi wake ni take or lose.

Utauliza kwa nini serikali haikwenda mahakamani? Serikali haikwenda mahakamani kwa sababu ya hekima ya kisiasa. Ninaposema hekima za kisiasa nina maana kuwa, kesi kama hizi ambazo ni transnational litigation zinachukua muda mrefu sana kumalizika na kuna uwezekano mpaka muda wa awamu ya tano ungeisha bila hukumu ya kesi hiyo kutolewa.

Kilichofanyika ni concessions and compromises kwa pande zote.
 
Lissu aliwaambia zile ripoti za mruma na ossoro zilikuwa ni proffessorial rubbish naona sasa mmemuelewa lissu,
Ni hizo ripoti ndizo zimekuwa msingi wa majadiliano na kufikia muafaka!

Unaweza kuziita kwa jina lolote upendavyo lakini ukweli wake ni kuwa Mkurugenzi wa Barrick Gold amesema thamani ya makontena yaliyoko bandarini Dar yana thamani ya dola milioni 280.

Unajua wamesafirisha makontena mangapi kabla ya haya kuzuiwa pale bandarini? Ukiyajua ndio utafahamu kama ripoti ya Prof Mruma na Ossoro ni proffessorial rubbish.
 
Nadhani ni Accasia na sio Barrick waliokua wakicheza mchezo huo.

..Barrick ndiyo muanzilishi wa kampuni ya Accacia.

..Na wakati mambo hayo yakiendelea Barrick alikuwa akimiliki hisa nyingi zaidi ktk Accacia.

..Hivi leo hii Twiga Mining Corp wakifanya madudu, Barrick anaweza kudai hahusiki na kukwepa lawama?
 
Kwa kukazia zaidi naomba tufahamu hili.

Thamani ya dili la mauziano ya Barrick kwenda Randgold ni $18.3 billion. Maana yake mzigo uliobakia chini ya ardhi ya migodi iliyokuwa ya Barrick ambayo itakuwa chini ya Twiga mineral (Randgold 84% + Serikali 16%) ni zaidi ya $18.3 billion.
Mgao tutakaopata sijajua utakuwa kiasi gani? au mzungu katuingiza chaka?
Link ya wikipedia

 

Attachments

  • IMG_20200128_191143.jpg
    IMG_20200128_191143.jpg
    29.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom