Ok, nitakuelewesha...
Nimesema maandiko yako mengi kuhusu uamuzi wa CHADEMA, NCCR na ACT Wazalendo kukataa kushiriki mkutano huu wenye ajenda tatatishi ya "kujadili maudhui ya utekelezaji wa sheria inayoviongoza vyama vya siasa kufanya shughuli zao" ukiongozwa na;
1. Msajili wa vyama vya siasa [msimamizi wa sheria inayolea na kuongoza shughuli za vyama siasa na;
2. Polisi [ambao kwa maagizo ya wanasiasa wa upande wa pili walioko madarakani, huivunja sheria hii waziwazi mchana kweupe]
Kwa maoni yako unadhani kuwa, hivi vyama i.e CHADEMA, ACT Wazalendo & NCCR vinafanya makosa kutoshiriki kikao hki kwa sababu umesema "wanakosa fursa ya ku - air out" grievances zao...
Mimi ndo nakuambia sasa, kuwa huoni uovu uliojificha nyuma ya mipango ya CCM kwa kikao hicho...
Na isitoshe mvunja sheria [msajili wa vyama vya siasa na polisi] wanapata wapi morality ya kuitisha kikao cha mapatano na usuluhishi wakati wao wenyewe ndiyo watuhumiwa wa kuvunja sheria...?
Kwa kifupi sana ndg
Babati ni kuwa, huwezi kupata matokeo mazuri kwa kutumia njia haramu zisizo sahihi....!
Kama serikali inataka political reconciliation kati ya Makundi mbalinbali vikiwemo vyama vya siasa, basi njia sahihi na nzuri itumike kuleta taifa pamoja ....