Sahihi kabisa. Lakini kabla ya hayo mazungumzo lazima dhamira ya dhati ya kuweka uwanja sawa wa kuendesha siasa ionekane. Kama utakua na kumbukumbu ya mkutano wa ndani wa NCCR Mageuzi uliozuiwa na Polisi Msimbazi Centre hivi karibuni, pale ndipo utaona hiyo dhamira bado iko mbali sana. Elimu ya siasa ya vyama vingi ifikishwe kwa jeshi la Polisi kwanza ndipo vikao vya aina hiyo vitaeleweka. Tatizo kubwa kwa Tanzania ni elimu ya siasa iko chini sana kwa wananchi, ndiyo maana watu wanaona chama cha siasa cha upinzani hakitakiwi kuwepo, na CCM wanatumia ignorance ya watu kuonesha kama vyama vingine vyote havifai, isipokua CCM pekee na kwa sababu POLISI wetu ndo hao wa division 5, basi hali ndiyo inafika tulipo.