Moses Cheyo:
Jambo la kwanza, kama moja wapo ya wazee tujipongeze wote kwakuwa na kikao hiki.
Katika 4R tulizofundishwa jana R moja inayohitajika katika mswada huu ni reform.
Moja kubwa kabisa tafsiri ya tume. Huko kata anaweza kujiita tume.
Upana wa tafsiri juu ya watenda wa tume wawe wa moja kwa moja siyo kuazima kutoka TAMISEMI.
Mkurugenzi anajifungia akifungua mlamgo anatangaza matokeo yaek.
Tukiongea reconcilation ni reconcilation na voters. Mkurugenzi ameonywa kuwa uchaguzi ukienda vibaya kwako mkeka unakuja.
Tume haionekani chini. Kwenye mswada huu hatuoni tume huko chini. Ninawaambia vijana hakuna sehemu ya kukimbilia ni hapa hapa tutengeneza tume nzuri.
La pili tume wajibu wake, itusaidie kusimamia pesa. Maana uchaguzi wa sasa ni mnada ukiwa na pesa ndio unapata ubunge ukiwa huna fedha hupati.
Jukumu moja wapo kubwa kuratibu pamoja na matumizi ya fedha hayaruhusiwi. Na adhabu kali. Leo watu wanatuibia sehemu nyingi ili kukusanya pesa wawe wabunge. Kama hamsikii shauri yenu.
Je, ni lazima tuendelee na utaratibu huu. Je hatuwezi kwenye na propotional representation. Tunashindana vyama hatushindani kuwa tunapesa kiasi. Hii inasaidia kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa. Itutafutie namna kuchaguaniani.
Yaani unahonga kiberiti au kabodo.
Wewe naona unataka numbers sisi tunataka ideas. Eti wamechangia wangapi