Habari wakuu,
Ninekuja mtembelea jamaa yangu hapa nimemkuta anafuatilia mkutano wa CCM na zoezi la upigaji kura liko linafanyika huko. Kilichonichekesha katika zoezi hili ni:
1. Hakuna usiri
2. Wajumbe wanapigiana kura (nimeona mmoja anapiga kwa niaba ya mwenzake)
3. Maandalizi hayakuwa vizuri (kuna uchache wa peni ) naona wana azimana tu, hawajui hata walienda fanya nini.
4. Naona watu wanatumia kujitangaza, baada ya kupiga kura wanajionesha ili teuzi zipite kwao.
5. Ukusanyaji wa kura ni vichekesho
kifupi, sijaona cha maana katika hili zoezi; liko kiswahili swahili sana.