Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Mkuu 'Stuxnet' umejibu kwa staha, kwa hilo nitaheshimu, lakini umekosea kuniweka kwenye hilo kundi la DIKTETA.

Kuhusu hiyo unayoiita "dira ya mama", hilo tunaweza kulijadili kwa kina. Binafsi sikubaliani na utegemezi wa kuja kuendelezwa na mtu mwingine. Tutajiendeleza kwa juhudi zetu. Hii haina maana kwamba hatutashirikiana na wengine kutoka nje kwa heshima na maslahi yetu yakiwa ndio kipaumbele.
Usitake kupotosha kwa kudai kwamba ninaposisitizia juhudi zetu kujiendeleza ndio iwe maana ya kwamba sitaki ushirikiano na wengine.
 
Sasa dar ukipanda miti kwenye eneo la 20*20 utapata hata sehemu ya kupaki baiskeli?
 
kinachoniuma zaidi ni kuomba misaada ya kutunza mzingira halafu huku yetu tunayaharibu maksudi
 
Unaishi Karagwe nini!
 
Hata ukiwa na juhudi zako nzuri na raslimali zote kama utakuwa huna multitateral na bilateral cooperation na nchi zingine huwezi kupiga hatua.

Hamna mtu anabeza juhudi binafsi za nchi na wananchi wake
 
Neno hilo
 
Hotuba safi kabisa imetolewa na yule mama wa Barbados. Huyo mama nimeona ni kiongozi anayejitambua na siyo wa kwetu ambaye ameonekana kuhangaikia kujulikana. Ni kama amekwenda kujitangaza ili ajulikane. Ni makosa yake na makosa ya kutafuta wasaidizi wabovu.
Hii ndo hotuba
 
Kinachojadiliwa ni hotuba yake Glasgow. Una maana yeye kila anakokwenda anatafuta pesa ya msaada? Suala la mazingira siyo jambo la kurukia tu na kuandikiwa hotuba. Alistahili awe na watu welevu wanaojua dynamics za mikutano ile. Sisi kama TZ tuna alama kubwa sana ya climate change; Kilimanjaro na Z'bar kama sehemu ya visiwa vinavyozama. Huo ungekuwa mtaji mkubwa sana wa kuwafanya viongozi wengine wasikilize. Kwa nini yeye ameishia kuzungumzia theories za climate change kwa watu wanaojua kuliko yeye?

Mkutano kama ule unaanza kueleza madhara ya climate change? Unamueleza nani asiyejua?
 
Kweli kabisa
 
[ ] Nina amini kwamba madhumuni ya mkutano unaoendelea nchini Scotland ni kuweza kujadili changamoto mbali mbali zinazohusu mabadiliko ya tabia nchi. Ni jambo kubwa kuweza kuwa kusanya viongozi wote walio hudhuria na kwasababu hiyo vipaumbele lazima vilihusu kupata solutions kutatua tatizo hili. Umeelezea kuhusu ulazima wa nchi zilizo endelea kusaidia kifedha nchi zinazo endelea lakini sidhani kama mkutano huo ulikuwa muafaka kuwa kumbusha kuhusu "Jukumu" hilo. Instead huo ulikuwa muda wa kujenga hoja nzito, kuwa na taarifa mbali mbali kuhusu tatizo hili na kuwa na mchango ambao unatekelezeka na kudumu katika mawazo ya viongozi wengine.
 
Mipango bila pesa ni ubatili mtupu.
 
Una kubali kwamba fedha hizo zinapatikana bila kuonyesha mikakati inayo tekelezeka na kubaini uzito wa tatizo hilo nchini?
 
Tafadhali fuatilia hapa umsikilize Waziri Mkuu wa Barbados....ameupiga mwingi sana! 👇👇


Kwa taarifa tu ni kuwa mkutano wa UNFCCC COP unatanguliwa na matoleo ya ripoti za kisayansi juu ya mabadiliko ya tabianchi. Fuatilia zaidi hapa:👇👇 https://www.ipcc.ch/

KWa asilimia kubwa hizo reports ndo zinakuwa kiini cha majadiliano na makubaliano mengi kwenye mkutano wa UNFCCC COP.
Mijadala itaendelea na nyakati wakati wanafikia muafaka. Sema kuna wakati mambo yanavurugika bila makubaliano yoyote ya maana!
Tufiatilie COP26 kule Glasgow tujue yatakayojiri!
 
Hotuba zote ni hotuba... Kila mtu na kipaji chake!
Muhimu ujumbe ufike! #SSH hawezi kuwa huyo PM wa Barbados; Bi Mia Mottley! Ni binadamu wawili tofauti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…