Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na kaiongelea mbele ya mkuu wa nchi
 
100%
 
Twende sawa Ndugu Mwandishi hiyo ni positive au Negative?
 
Wahamiaji haramu hujipenyeza kwanza kwenye vyombo via usalama, vyama tawala na ukaribu/urafiki na familia za viongozi.
Changamoto kubwa huwa ipo hapo (siyo kwa Tanzania tu).
Hata hivyo, viongozi waovu huwapenda na huwatumia kuwadhibiti wazawa.
Jambo la muhimu ni raia kujitambua na kuwatambua wageni pia kuwatendea haki katika hadhi yao ya ugeni au ukimbizi.
 
Wahamiaji haramu hujipenyeza kwanza kwenye vyombo vya usalama, vyama tawala na ukaribu/urafiki na familia za viongozi.
Changamoto kubwa huwa ipo hapo (siyo kwa Tanzania tu).
Hata hivyo, viongozi waovu huwapenda na huwatumia kuwadhibiti wazawa.
Jambo la muhimu ni raia kujitambua na kuwatambua wageni pia kuwatendea haki katika hadhi yao ya ugeni au ukimbizi.
 
Sasa CDF analalamika au anapongeza wakimbizi kupenya serikalini?

Au anaripoti, anakemea au ni nini shida?
Wanaongeaga kinidhamu hao na kizalendo ila wakilianzisha kuwasaka na kukomesha hao vinyemelezi vya ugaidi na imani utatokomezwa mara moja...Mungu ibariki Tanzania maana Ugaidi na vikundi vya kihalifu sikia tu kwa jirani...tuna amini vyombo vyetu litakwisha hili!!!!
 
Raia wa kawaida hana cha kufanya kwenye hili.

Ndugu mtoa comment nikupe changamoto kwenye hoja yako.

Najua kila raia ana haki ya kuchagua mrengo wake wa siasa au ufuasi. Je umeshaona Watanzania wasio asili ya Tanzania wanajiunga na chama nje ya ccm?

Na bahati nzuri wote ni matajiri tu.


Mchana mwema. Tuendelee kutafakari hoja ya CDF
 
Na hao JW wenyewe wamelala tu


 
Hii nchi bhana! Sasa mpaka hao wakimbizi wanajipenyeza katika nafasi nyeti za kimaamuzi; vyombo husika vya kudhibiti huo udhaifu vinakuwa vimelala usingizi, au ndiyo yale matatizo ya kuteuana kwa kujuana!!
 
Wawataje Ili wanyofolewe maana Tiss wanazingua sana.
 
Naibu waziri mkuu ni mkimbizi.....
 
Duh. Ujumbe mzito wa siri. Huu ni mtonyo mkubwa kwa serikali. Naona JW wamewaambia TISS tunawamulika kwa kuwa ninyi ni wazembe, mmelega lega.
 
Kusema kila mtu wa mwenye asili ya nje asikae nchini haiwezekani. Ila nafasi nyeti wapewe wale ambao kweli wako nchini na nchi itakuwa salama. Kuna majasusi wengi wanaoingia kwa mambo haya ya ukimbizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…