Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024


CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Kuna ka mchomali humu jf kalivuka mipaka na kusema eti hii ardhi yao😂😂😂 haya sasa bishana na wakulungwa .... na msako wa nyumba kwa nyumba uanzwe kutoa hivyo vipaka pori vinavyo chochea ugaidi maana wanakuaga na siri zao hao mixer long term plans , udhibiti ufanyike kwa hawa watu wa itikadi kali maana tutakao umia ni sisi raia wazawa na wazelendo wa nchi yetu. Tunapenda kula kwa kutabasamu na utulivu sio kukimbia kimbia kama walivyozoea wao!!!
 
Na hao JW wenyewe wamelala tu


View attachment 2879502
Wakati huo Vyombo vya habari vilikuwa vinaweza kupaza sauti na kuiokoa Tz.

Kwa sasa wacha tuendelee hivi hivi.
 
Raia kutoka Zanzibari kwa sasa pia wamejazana mnoooooo kwenye taasisi za serikali zisizo za Muunganiko usio na Muunganiko, hadi watu tunashindwa kuhema

Ukiwagusa wanakwambia kwao Tanga, lakini story na mazungumzo yao yote ni kuhusu Zanzibar;

Jamaa hawajui hata ng'ombe sasa kweli kuna Mtanganyika asiyejua ng'ombe???
Ficha ujinga wako.
 
Wahamiaji haramu hujipenyeza kwanza kwenye vyombo vya usalama, vyama tawala na ukaribu/urafiki na familia za viongozi.
Changamoto kubwa huwa ipo hapo (siyo kwa Tanzania tu).
Hata hivyo, viongozi waovu huwapenda na huwatumia kuwadhibiti wazawa.
Jambo la muhimu ni raia kujitambua na kuwatambua wageni pia kuwatendea haki katika hadhi yao ya ugeni au ukimbizi.
Raia wa kawaida hana cha kufanya kwenye hili.

Ndugu mtoa comment nikupe changamoto kwenye hoja yako.

Najua kila raia ana haki ya kuchagua mrengo wake wa siasa au ufuasi. Je umeshaona Watanzania wasio asili ya Tanzania wanajiunga na chama nje ya ccm?

Na bahati nzuri wote ni matajiri tu.


Mchana mwema. Tuendelee kutafakari hoja ya CDF
Niliandika sehemu wanapolenga au kupitia;
1. Vyombo vya usalama
2. Vyama tawala
3.Ukaribu na viongozi au familia zao

Matokeo yake = teuzi na baadaye kutawala nchi.
 
Statement ina maswali mengi kuliko majibu wanaashiria nini haswa.

Wamejuaje kuna watu wana nafasi serikalini wakiwa wakimbizi? Wakati statement kama hiyo ulitegemea kutolewa na uhamiaji.

Je wakimbizi wakipewa uraia awaruhusiwi kufanya kazi serikalini au kushiriki siasa.

Je kuna mienendo ya watu walikuwa inawafuatulia katika uchunguzi wao wakabaini hawana makaratasi sahihi ya kushika hizo nafasi

Je wanaashiria uhamiaji inatoa uraia kirahisi without due processes.

Je wanaashiria ni rahisi kupata vitambulisho na huko serikalini hawana system nzuri ya ku-very background ya watu.

Ni statement tata sana with ‘fuzzy logic’ conclusion.
 
Hii ni hatari Sana sana, analengwa Nani hapa? Hussein au Nani?
Analengwa Mr Slim na mapandikizi
Wasomali ni wapambanaji tu kaangalie Nairobi walivyoishika kwa Uchumi
Watoto wa Baba hao hata US na kwingine wanakubalika kwa uaminifu

Screenshot_20240103_195532_Instagram~2.png
 
Daah Jeshi nao wanalia kuwa Wakimbizi wapo kwenye maamuzi nilitegemea kwa Mamlaka yao wafanye kazi na Uhamiaji tu ila pia ni ngumu kuwatoa wana Siasa waliochimba mizizi mikubwa..
 
Kuna mwaka siukumbuki CFD waliwahi kutangaza kuwa kamanda wao wa jeshi upande wa tehama alitoweka kusiko julikana, ikasemekana kuwa yawezekana alikuwa siyo m tz karudi kwao sjui nchi gani. Hadi leo labda jeshi tu ndo wanajua ukweli wake.
 
Back
Top Bottom