BABUU ISAKI RITTE
Senior Member
- Jan 20, 2024
- 198
- 195
Yupo Mkenya mmoja anaitwa Cristopher Kirubi alisoma Kairuki Univercity na kuajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona ndugu zetu wanaajiriwa Nchi zingine?Yupo Mkenya mmoja anaitwa Cristopher Kirubi alisoma Kairuki Univercity na kuajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Hili nilisikia sana maeneo ya kibiti mwaka 2019.Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.
Siku zote walikuwa wapi kwaniTiss waingie kazini sasa washapewa hints..mama kaongea vizuri kweli katoa taadhali 2024,2025 vyombo vya ulinzi na usalama viwe makini kweli na kujiandaa kwa lolote...
Kama kijana kakulia Tanzania kuanzia akiwa mdogo kumuondoa kwenye madara kwasababu ya wazazi kuwa wakimbizi ni ubaguzi na haina manufaa yeyote. Tuwape uraia watu na tuondokane na ubaguzi
Hilo pia linawezekana maana haya ya vyeti unaweza kukuta kama ulizaliwa hospital na jina lako lipo huko Kuna uwezekano mkubwa wa wafanyakazi kuuza jina lako na kumpa mtu cheti chako maana kuna watu wengi wala hawajawahi kuuliza wala kuuliza na hata kujua ina faida ganiCha kufanya tuachane na utaratibu wa vyeti bali Kila kitu kiwe compurized pale mtoto anapozaliwa tu basi taarifa zake ziingizwe chapu kwenye mfumo, na mifumo isomane mtu akisema amezaliwa sehemu flani basi chapu unaingia website Kila kitu unakikuta vyeti vinaoza,vinaliwa na panya,mende,vinasombwa na mafuriko,vinaungua na moto n.k
Sasa utaratibu huo ufuatwe je wanatoa hizo huduma wako clean na kufuata masharti yote bila kupindisha?Mambo ya ugaidi yametoka wapi tena kinachoongelewa ni watu kufuata utaratibu ndo maana ya kuwepo uhamiaji hata marekani watu kibao wanakua deported sababu tu hawajafuata utaratibu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024
CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.
Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.
CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.
Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.
RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”
Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.
Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."
Linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, siyo la CCM, CHADEMA au TLP, watambue nafasi yao na kufanya wajibu wao.Samia ameanza kuliagiza jeshi tena kuhusu hizi chaguzi 2 za 2024/2025!!!....
Kwamba Jeshi liwe tayari kwa lolote Lile!
Hii kwa jeshi sio ombi tena!... Ni amri-tekelezi ....Ni tayari!.
Hii ni taa nyekundu tayari kwa vyama vyote kuelekea 2024/25 vijiandae kisaikolojia!
Hii ina Maana chaguzi za 2024/2025 zitakuwa na backup ya jeshi!
Hizi chaguzi hazitakuwa tofauti na ule uchaguzi wa 2019/2020 wa mwendazake.
Hii nchi Bado tuna safari ndefu sana ya kuwa na demokrasia huru.
Hayo unauliza wewe yeye kashamaliza kaziStatement ina maswali mengi kuliko majibu wanaashiria nini haswa.
Wamejuaje kuna watu wana nafasi serikalini wakiwa wakimbizi? Wakati statement kama hiyo ulitegemea kutolewa na uhamiaji.
Je wakimbizi wakipewa uraia awaruhusiwi kufanya kazi serikalini au kushiriki siasa.
Je kuna mienendo ya watu walikuwa inawafuatulia katika uchunguzi wao wakabaini hawana makaratasi sahihi ya kushika hizo nafasi
Je wanaashiria uhamiaji inatoa uraia kirahisi without due processes.
Je wanaashiria ni rahisi kupata vitambulisho na huko serikalini hawana system nzuri ya ku-very background ya watu.
Ni statement tata sana with ‘fuzzy logic’ conclusion.
Sidhani kama ni hivyo.Samia ameanza kuliagiza jeshi tena kuhusu hizi chaguzi 2 za 2024/2025!!!....
Kwamba Jeshi liwe tayari kwa lolote Lile!
Hii kwa jeshi sio ombi tena!... Ni amri-tekelezi ....Ni tayari!.
Hii ni taa nyekundu tayari kwa vyama vyote kuelekea 2024/25 vijiandae kisaikolojia!
Hii ina Maana chaguzi za 2024/2025 zitakuwa na backup ya jeshi!
Hizi chaguzi hazitakuwa tofauti na ule uchaguzi wa 2019/2020 wa mwendazake.
Hii nchi Bado tuna safari ndefu sana ya kuwa na demokrasia huru.
Inamaana adui ameingia chumbani tena kitandani? Maana hii itasababisha public panic...Mnataarifiwa watanzania. Ni taarifa ambayo CDF ameamua kuichomoa toka kwenye hadhi ya SIRI na kuileta kwa jamii. Mchango wako juu ya hili ni muhimu kwake.
Samia ameongea kwa tafsida...nyepesi sana kueleweka hata na Std VII... Waliopewa hayo maagizo chini ya bosi wao CDF... Wanaelewa Samia amemaanisha nini!.... 2024 sio mbali... Will see!!!Sidhani kama ni hivyo.
Vipi kuhusu wakurya na wajaluo wanajiita watanzania kumbe ni wakenya ?Zis is serias!
Wanyarwanda na warundi bado wamo jeshini na usalama?
Nchi hii hatuko serious na usalama wa nchi!
Alikua mnyarwandaKuna mwaka siukumbuki CFD waliwahi kutangaza kuwa kamanda wao wa jeshi upande wa tehama alitoweka kusiko julikana, ikasemekana kuwa yawezekana alikuwa siyo m tz karudi kwao sjui nchi gani. Hadi leo labda jeshi tu ndo wanajua ukweli wake.
mhutu hana tatizo bali mtusi ndio mwenye tatizo na watusi wapo wengi kwenye sector nyeti na hao ndio wabaya kuliko yeyote na ndio maana kagame anatamba kwa sababu hiyoCDF yupo sahihi, kazi ya Jeshi ni kulinda mipaka ya nchi na katika hilo wameona tatizo.
Kazi ya kutathmini ilipaswa kuwa ya Uhamiaji na TISS, kwa bahati mbaya wapo 'busy' na mambo yasiwahusu.
Kwa mfano Uhamiaji imetumika kuadhibu watu kisiasa, TISS wapo mguu sawa na Wapinzani
Afadhali CDF amesema maana wahusika hawana habari na hili ni jambo la hatari.
Lakini pia vetting katika ajiri na Teuzi ni tatizo ambalo TISS walipaswa kuliona
Pili, Tanzania ina Wakimbizi katika Vijiji bila kuwatawanya. Ipo siku Watakuwa M23 n.k. kwasababu wana maeneo.
DRC wanalipa gharama ya uzembe, '' Raia '' waliokuwa wakimbizi kutoka Rwanda sasa wanashirikiana na Rwanda
Wakimbizi walipaswa kutawanywa ili wachanganyike na Raia wengine si kuwapa ' nchi' ndani ya Nchi
Tatu, kikao hiki kimefanywa kwa 'mkakati' wakati CDM wakiandaa maandamano na fagio la RC kudoda.
RC alilitumbukiza Jeshi katika uzoaji taka, sasa Rais analiingiza Jeshi katika siasa kwa njia ya usalama wa uchaguzi.
Hapa anawaamuru kwamba wakipata maagizo waingilie kati. Ipo siku utasikia '' tumebaini' viashiaria vya hali XX
Bado tatizo la kuliingiza Jeshi katika siasa lipo pale pale ingawa leo limefanywa 'kiufundi' .
Hatari ni kwamba Jeshini kuna Watu wenye itikadi tofauti za kila eneo iwe siasa au dini.
JokaKuu Tindo Pascal Mayalla