Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yupo Mkenya mmoja anaitwa Cristopher Kirubi alisoma Kairuki Univercity na kuajiriwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Mbona ndugu zetu wanaajiriwa Nchi zingine?

Sioni tatizo hapo ikiwa vilifuatwa vigezo.
 
Nishapanda gari na mtu anazungumza kiswahili cha kongo lakini niliona wakati akitoa waleti ana kitambulisho cha NIDA.
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.
Hili nilisikia sana maeneo ya kibiti mwaka 2019.
 
Tiss waingie kazini sasa washapewa hints..mama kaongea vizuri kweli katoa taadhali 2024,2025 vyombo vya ulinzi na usalama viwe makini kweli na kujiandaa kwa lolote...
Siku zote walikuwa wapi kwani

Ova
 
Kama kijana kakulia Tanzania kuanzia akiwa mdogo kumuondoa kwenye madara kwasababu ya wazazi kuwa wakimbizi ni ubaguzi na haina manufaa yeyote. Tuwape uraia watu na tuondokane na ubaguzi

Cha kufanya tuachane na utaratibu wa vyeti bali Kila kitu kiwe compurized pale mtoto anapozaliwa tu basi taarifa zake ziingizwe chapu kwenye mfumo, na mifumo isomane mtu akisema amezaliwa sehemu flani basi chapu unaingia website Kila kitu unakikuta vyeti vinaoza,vinaliwa na panya,mende,vinasombwa na mafuriko,vinaungua na moto n.k
Hilo pia linawezekana maana haya ya vyeti unaweza kukuta kama ulizaliwa hospital na jina lako lipo huko Kuna uwezekano mkubwa wa wafanyakazi kuuza jina lako na kumpa mtu cheti chako maana kuna watu wengi wala hawajawahi kuuliza wala kuuliza na hata kujua ina faida gani

Hivi unafikiri kwanini watu huwa wanaambiwa wewe sio mtz au hujazaliwa hapa
Utakuta jina anafanyia kazi mtu mwingine kabisa

Yaani usalama huu wanaokazana watu kuusema hawajui kuna watu wana jina la babu yangu 😄 🤣
 
Mambo ya ugaidi yametoka wapi tena kinachoongelewa ni watu kufuata utaratibu ndo maana ya kuwepo uhamiaji hata marekani watu kibao wanakua deported sababu tu hawajafuata utaratibu
Sasa utaratibu huo ufuatwe je wanatoa hizo huduma wako clean na kufuata masharti yote bila kupindisha?
Home office ya UK kuna wafanyakazi kibao wqnaijeria ila wazawa au walikuja wadogo lakini wanafuata sheria walizopewa na sio vingine
Ukiomba passport huonani na binadamu bali kila kitu online mpaka picha unaituma mara moja tu
Kama nao hawataomba chochote tusingefika huku
Mkuu wa Majeshi anajua analenga wapi mumuelewe
 
Tabia ya Serikali kusema wengine sio raia na kuhoji asili zao pale wanapokuwa na maoni tofauti ndio inafanya iwe rahisi hata wasio raia wa TZ kuingia kwasababu tu wanapo support chama na Serikali.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024


CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."


Well done CDF, namna hiyo, sasa angalau tunaanza kuona JWTZ tunaIolitaka, jamani muongee sasa na mufike mbali "MUKEMEE" viongozi, wengi wao hawawaogopi, hawawa heshimu ndomana wanaipeleka nchi kama wanavyotaka, juzi katoka mmoja katoa amri mukazibue vyoo tar. 24 hii ni dharau kubwa sana kwa JWTZ.
 
Samia ameanza kuliagiza jeshi tena kuhusu hizi chaguzi 2 za 2024/2025!!!....

Kwamba Jeshi liwe tayari kwa lolote Lile!

Hii kwa jeshi sio ombi tena!... Ni amri-tekelezi ....Ni tayari!.

Hii ni taa nyekundu tayari kwa vyama vyote kuelekea 2024/25 vijiandae kisaikolojia!

Hii ina Maana chaguzi za 2024/2025 zitakuwa na backup ya jeshi!

Hizi chaguzi hazitakuwa tofauti na ule uchaguzi wa 2019/2020 wa mwendazake.

Hii nchi Bado tuna safari ndefu sana ya kuwa na demokrasia huru.
Linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, siyo la CCM, CHADEMA au TLP, watambue nafasi yao na kufanya wajibu wao.
 
Statement ina maswali mengi kuliko majibu wanaashiria nini haswa.

Wamejuaje kuna watu wana nafasi serikalini wakiwa wakimbizi? Wakati statement kama hiyo ulitegemea kutolewa na uhamiaji.

Je wakimbizi wakipewa uraia awaruhusiwi kufanya kazi serikalini au kushiriki siasa.

Je kuna mienendo ya watu walikuwa inawafuatulia katika uchunguzi wao wakabaini hawana makaratasi sahihi ya kushika hizo nafasi

Je wanaashiria uhamiaji inatoa uraia kirahisi without due processes.

Je wanaashiria ni rahisi kupata vitambulisho na huko serikalini hawana system nzuri ya ku-very background ya watu.

Ni statement tata sana with ‘fuzzy logic’ conclusion.
Hayo unauliza wewe yeye kashamaliza kazi
 
Samia ameanza kuliagiza jeshi tena kuhusu hizi chaguzi 2 za 2024/2025!!!....

Kwamba Jeshi liwe tayari kwa lolote Lile!

Hii kwa jeshi sio ombi tena!... Ni amri-tekelezi ....Ni tayari!.

Hii ni taa nyekundu tayari kwa vyama vyote kuelekea 2024/25 vijiandae kisaikolojia!

Hii ina Maana chaguzi za 2024/2025 zitakuwa na backup ya jeshi!

Hizi chaguzi hazitakuwa tofauti na ule uchaguzi wa 2019/2020 wa mwendazake.

Hii nchi Bado tuna safari ndefu sana ya kuwa na demokrasia huru.
Sidhani kama ni hivyo.
 
Katika nafasi zenye maamuzi!! Hii ni hatari sana!! Jeshi likisema hivyo ni ujumbe mzito kwa watala!! Kama majina wanayo wawape TISS wafanyie kazi haraka sana!!
 
CDF yupo sahihi, kazi ya Jeshi ni kulinda mipaka ya nchi na katika hilo wameona tatizo.

Kazi ya kutathmini ilipaswa kuwa ya Uhamiaji na TISS, kwa bahati mbaya wapo 'busy' na mambo yasiwahusu.
Kwa mfano Uhamiaji imetumika kuadhibu watu kisiasa, TISS wapo mguu sawa na Wapinzani

Afadhali CDF amesema maana wahusika hawana habari na hili ni jambo la hatari.
Lakini pia vetting katika ajiri na Teuzi ni tatizo ambalo TISS walipaswa kuliona

Pili, Tanzania ina Wakimbizi katika Vijiji bila kuwatawanya. Ipo siku Watakuwa M23 n.k. kwasababu wana maeneo.
DRC wanalipa gharama ya uzembe, '' Raia '' waliokuwa wakimbizi kutoka Rwanda sasa wanashirikiana na Rwanda

Wakimbizi walipaswa kutawanywa ili wachanganyike na Raia wengine si kuwapa ' nchi' ndani ya Nchi

Tatu, kikao hiki kimefanywa kwa 'mkakati' wakati CDM wakiandaa maandamano na fagio la RC kudoda.

RC alilitumbukiza Jeshi katika uzoaji taka, sasa Rais analiingiza Jeshi katika siasa kwa njia ya usalama wa uchaguzi.
Hapa anawaamuru kwamba wakipata maagizo waingilie kati. Ipo siku utasikia '' tumebaini' viashiaria vya hali XX

Bado tatizo la kuliingiza Jeshi katika siasa lipo pale pale ingawa leo limefanywa 'kiufundi' .
Hatari ni kwamba Jeshini kuna Watu wenye itikadi tofauti za kila eneo iwe siasa au dini.

JokaKuu Tindo Pascal Mayalla
mhutu hana tatizo bali mtusi ndio mwenye tatizo na watusi wapo wengi kwenye sector nyeti na hao ndio wabaya kuliko yeyote na ndio maana kagame anatamba kwa sababu hiyo
 
CDF ameongea mambo mazito mno kuhusu wakimbizi na walowezi wengine kujipenyeza serikalini kwenye nafasi nyeti, ni maajabu amiri jeshi mkuu kwenye hotuba yake ameonesha kuwa yeye anawaza uchaguzi tu na namna ya kulitumia jeshi kuvuka.

Inawezekana wamemwambia sana huko sirini lakini hana muda na hilo, wameamua kuweka mambo hadharani wananchi tujue, wakijua labda SSH atapata msukumo wa kulivali njuga.
 
Back
Top Bottom