Mkuu wa Mkoa, jukumu la kuwaondoa Wamachinga ni lako. Usilikwepe

Mkuu achana na polojo hizo, sasa hivi hilo linaenda kutendeka na kubakia historia, kwani imekuwa kero kubwa mno!!yaani waenda kwa miguu sasa hivi wanagongwa na magari kisa sehemu zao zimepangwa vitu!!kwa taarifa yako huu ni mkakati wa nchi nzima sasa!

Hatuwezi kukaa na kuwaogopa watu wakijiamulua kufanya wanavyotaka tu eti kisa utachukiwa, nenda mbagala ukaone wachina wanavyopata kazi kwenye ujenzi wa barabara za mwendokasi, hadi wanatishiwa kupigwa, kisa kuwaambia watoe bidhaa zao ili kazi zifanyike!!!, Kwani ccm mnategemea kura zilizopigwa ili kushinda?mmeanza lini?

Wiki iliyopita kule kwenye stendi ya magufuri kwa nje walikuwa wameanza kujenga mabanda, yote yalivunjwa na mgambo!!
 
Jamaa km umemsikiliza msala na mpira amewapa Wakuu wilaya na Wakurugenzi yeye kajitoa kweny hili sakata ili likibuma lisimkute
Kama huelewi utaratibu kaa kimya!!hayo maeneo yote yako chini ya manispaa, na DC, na DED, ndio wahusika , wenye vyombo vya utekelezaji, na wasimamizi wa BY LAWS!!zamu hii lazima wawekewe utaratibu, mtu anafungua grocery juu ya mtalo, wateja wake wanajisaidia barabarani!!
 
SAHAU huyo bwana kutumbuliwa.

Au nikuulize kwa mtego huu ambao wewe kachero "uchwara" unasema amenaswa unategemea mpaka lini atakua ametumbuliwa?

Maana unaweza ukapita mwaka akatumbuliwa ndo useme kisa wamachinga, Hahahahaha..

umebugi, SUPERBUG.
 
Acha wanga
 
Labda akaroge na akatambike zaidi pale Kwao Kawe Ukwamani nyuma ya Hotel ya Ghorofa ya Victoria alipozaliwa na Kukulia pia, ili Mizimu imuokoe ila hili la Wamachinga ndilo linaenda Kumuondoa kama RC wa Dar es Salaam muda wowote kutoka sasa.
Acha kuwanga
 
Sijui shule gani mlisoma!?

Yani mawazo yako binafsi unayalazimisha...
 
Nafikiri hivi..kama kuna mtu anajitaftia riziki sehemu na habughuzi riziki zako achana naye!
Hizo ni fikira zako lakini ghasia za wamachinga zimepita kipimo, maeneo mengi watembea kwa miguu inawabidi watumie barabara za magari ambazo nazo zimevamiwa na wamachinga. Janga jingine ni nini kinachoendelea nyuma ya vibanda vyao wakati wa usiku, wizi.
 
Chochote kinachofanyika bila utaratibu ni ghasia na fujo
 
Chochote kinachofanyika bila utaratibu ni ghasia na fujo
Utaratibu ni pale unapokuwa haujaruhusiwa, lakini hawa waliruhusiwa na mwendazake kufanya biashara hata kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa na akasema wasibughuziwe.
 
Dar es Salaam inapaswa kuwa safi,sio Kama ilivyo Sasa ipo Kama dampo
 
Labda akaroge na akatambike zaidi pale Kwao Kawe Ukwamani nyuma ya Hotel ya Ghorofa ya Victoria alipozaliwa na Kukulia pia, ili Mizimu imuokoe ila hili la Wamachinga ndilo linaenda Kumuondoa kama RC wa Dar es Salaam muda wowote kutoka sasa.
Lengo la kuwafukuza wamachinga Ni kutengeneza mfumo wa biashara rasmi ili tupate Kodi.Na kwa vile mama Ni muumini wa Tozo,naona Kama Makalla hatafukuzwa
 
Shida machinga wameshindwa kuwa wastaarabu
 
Kwa hiyo watembea kwa miguu sio binadamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…