Mkuu wa Mkoa, jukumu la kuwaondoa Wamachinga ni lako. Usilikwepe

Najiuliza Hilo swali zile grocery za barabarani huwa wanajisaidia wap
 
Hivi wewe Genta unajua kuwa alikuwa Mweka hazina wa CCM huyo kijana makala?
 
Wataendelea kuwapo, haya yote tunayoyasikia ni kutuonesha tu kuwa na wao wapo kazini.
 

Nakubaliana na ww hakuna Dc mwenye uwezo na ujasiri kwa hili la wamachinga Rc Makalla alibebe mwenyewe
 
Nakwambia watakinukisha mbaya
 
Kwaiyo mnataka wamachinga wapange bidhaa zao Hadi kwenye njia za waenda kwa miguu??! Kwani wao nani hadi ifikie waogopwe kuondolewa
 
Hoja yako dhaifu sana, kwa hiyo nchi hii tumekuwa tunachaguliwa kiongozi na wamachinga? saficha mji wote na 2025 chama kinashinda upige kura usipige ila kusema huu upuuzi basi kesho watakuja vibaka na kusema mkitukamata hatupigi kura itabidi uwaachie tu kesho tu malaya sijui atakuja nani tena. mkuu wa mkoa safisha ni bora utengeliwe kwa kufanya jambo sawa kuliko kuendekeza huu upuuzi.
 
Issue ni wamachinga wanaopanga bidhaa barabarani, Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam ni vema ikaandaa maeneo rafiki ya kufanyia biashara kwa wamachinga watakao ondolewa barabarani au njia za waenda kwa miguu.
Elimu itolewe kabla ya kutekelezazoezi hilo, na kazi iendelee.
 
Serikali nzima ipo nyuma ya hili. Anayetaka kuota ndoto za mchana, aendelee. Machinga wataondolewa, hakuna wa kutumbuliwa wala kutumbua.
 
Hicho alichosema ni nukuu tu toka kwa mwendazake, yeye alisema hawa ni wapigakura wake wasibugudhiwe na ruksa kufanya biashara hata mlangoni kwa mkuu wa mkoa na barabara zimejengwa kwa ajili yao wafanyie biashara, sasa sijiui unamkatalia nini, kauli ile ndiyo inayowafanya viongozi wote kuwaogopa wamachinga na kila aliyewagusa aliondoka yeye.
 
Hajasema nukuu usipotoshe na hata kama JPM ameshafariki hii ni serikali mpya na sera mpya ni kama chanjo alizikataa na sasa zinakubaliwa hakuna haja ya kumuingiza Marehemu katika hili. Tuongelee ya sasa kama wamachinga walikuwa wapiga kura wake basi Mama wapiga kura wake watembea kwa miguu na wafanya biashara. Hakuna kuwa kiburi machinga wala nini kwanza hao hata hawapigi kura wako busy na biashara tu. Safisha mji mkuu wa mkoa.
 
Chochote kinachofanyika bila utaratibu ni ghasia na fujo
Ghasia ni ile unayofanya bila ruhusa, ukiruhusiwa kufanya biashara katikati ya barabara, hiyo si ghasia ndiyo sababu hawaguswi na mtu yoyote.
 
Nafikiri hivi..kama kuna mtu anajitaftia riziki sehemu na habughuzi riziki zako achana naye!
Kutafuta riziki ni sawa, ila kuna watu ambao halimashauri za wilaya zimechukua hela chungu nzima kama kodi, na ada za leseni ila kwa usumbufu wa hawa wajasiriamali wamefunga njia zote za kufikia haya maduka!! Wewe binafsi unaona hii ni sawa!?
 
Mkuu pamoja na ushauri wako mzuri lakini nadhani tukijua majukumu ya viongozi wetu wa juu ya uendeshwaji wa shughuli za Serikali, hakuna tatizo lolote katika kulishughulikia suala hili, vinginevyo ni baadhi ya viongozi wa juu kutaka kujimwambafai, ni hili ndilo tatizo kubwa kwa Viongozi wengi. Suala hili kuwa chini ya Mkuu wa Mkoa ndio mahala pake; yeye na wakuu wa wilaya ndio wanapanga namna na mbinu na mikakati ya jinsi ya kulitatua.
Watendaji Kata na Mitaa/Vijiji ndio watekelezaji katika maeneo yao, ni suala la kuwezeswa na kupatiwa nyenzo za kazi.

Serikali ndio yenye Dola, hivyo ni matumaini yangu kwa % 100 inauwezo wa kutatua tatizo hili bila ya madhara yeyote na kila mmoja wetu akarizika kabisa na utekelezaji wake, la msingi ni kila Kiongozi atimize wajibu wake. Suala hili si la vyama ni suala la Kiserikali Kwa manufaa ya Wananchi wote
 
Hili jambo sio lake wala la mtu mmoja...

Hili jambo ni letu Sote....

 
Kinachotakiwa sasa ni kusahau yaliyopita na kuanza kuweka miji yetu katika ustaarabu!! Zamani hawa mama lishe walikuwa angalau wanaogopa uwepo wa sheria walikuwa wanapikia maeneo yasiyokuwa na usumbufu na kuleta chakula kilichopikwa!! Sasa wanapikia popote!! Hii ni aibu sana
 
Kwanza wamachinga awampendi mama yetu kutwa kumsema vibaya Bora wafurushwe warudi maporini kwao,au Chato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…