T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Usikaze kichwa. Point sio jina, alikozaliwa, alikosomea, alikofanya kazi au nini. Point ni kuwa na taarifa za mtumishi nyeti wa serikali na ikiulizwa kama hivi usibeze.Umetoa mfano mzuri wa huyo muisrael ambaye alijipachika jina linalofanana na jamii ya Syria na alifanya hivyo ili asitambulike kwahiyo hata hapa kwetu nina imani adui yeyote hawezi kujiweka katika hali ya kutiliwa shaka ndio maana watu wanambeza mleta uzi kwa sababu huyo angekuwa jasusi hawezi tena kutumia jina la kwao kiasi cha kumtilia shaka.
Mfano Marekani wana 5 levels of security clearance. Level ya chini anaweza kuwa fundi kurekebisha bomba la ofisini ameitwa, level ya staff kama mpishi ni nyingine, level ya mfanyakazi mwenye access ya taarifa za kuagizwa ni nyingine, level ya juu kabisa ya mwenye maamuzi ni Confidential clearance. Hata kama mtu kazaliwa nje anapitia security clearance kufanya kazi fulani akifaulu ndio anapata hata baba yake awe nje kama Obama.
Albert Einstein usalama walimkataa hawakumpa security clearance kwa kuwa ni Mjerumani na katoka uko ukubwani, hawakutaka ahusike na Manhattan project kutengeneza nuclear weapons wakati at the time alikuwa top scientist.
Ukienda nchi nyingine kama UK ukauliza historia ya wazazi au uraia wa viongozi utaambiwa Rish Sunak Waziri Mkuu ambavyo mama yake alizaliwa Tanzania na baba akazaliwa Kenya. Taarifa unapewa kwa uwazi kabisa, bongo ukiuliza background ya kiongozi unafichwafichwa as if haikuhusu. Kama mnataka private life si mfanye biashara au kilimo, huwezi taka kuongoza watu kisha maisha yako wasiyajue