Mkuu wa Mkoa Songwe ni Mtanzania? Jina kama Mkongo au Mrundi?

Usikaze kichwa. Point sio jina, alikozaliwa, alikosomea, alikofanya kazi au nini. Point ni kuwa na taarifa za mtumishi nyeti wa serikali na ikiulizwa kama hivi usibeze.

Mfano Marekani wana 5 levels of security clearance. Level ya chini anaweza kuwa fundi kurekebisha bomba la ofisini ameitwa, level ya staff kama mpishi ni nyingine, level ya mfanyakazi mwenye access ya taarifa za kuagizwa ni nyingine, level ya juu kabisa ya mwenye maamuzi ni Confidential clearance. Hata kama mtu kazaliwa nje anapitia security clearance kufanya kazi fulani akifaulu ndio anapata hata baba yake awe nje kama Obama.

Albert Einstein usalama walimkataa hawakumpa security clearance kwa kuwa ni Mjerumani na katoka uko ukubwani, hawakutaka ahusike na Manhattan project kutengeneza nuclear weapons wakati at the time alikuwa top scientist.
Ukienda nchi nyingine kama UK ukauliza historia ya wazazi au uraia wa viongozi utaambiwa Rish Sunak Waziri Mkuu ambavyo mama yake alizaliwa Tanzania na baba akazaliwa Kenya. Taarifa unapewa kwa uwazi kabisa, bongo ukiuliza background ya kiongozi unafichwafichwa as if haikuhusu. Kama mnataka private life si mfanye biashara au kilimo, huwezi taka kuongoza watu kisha maisha yako wasiyajue
 
Nilianza naye kule...aibu tupu
 
Mleta uzi ameuliza jina na ndicho kinachompa shaka hadi kuuliza asili ya huyo mtu na ndicho watu wanamjibu,acha kujitia ujuwaji kwa kutoa maelezo marefu ambayo mleta uzi sio hitaji lake.
 
Mleta uzi ameuliza jina na ndicho kinachompa shaka hadi kuuliza asili ya huyo mtu na ndicho watu wanamjibu,acha kujitia ujuwaji kwa kutoa maelezo marefu ambayo mleta uzi sio hitaji lake.
Jamaa kajibu mantiki ya kuulizwa kwa asili ya jina lake. Ujuaji ndio nini sasa!?
 
Eti outsiders. Hawa huwa hawasahau asili zao.

Kwa mfano akitoka Rwanda akaja Tz ni full chinja chinja
 
Mkuu wa mkoa mpya wa Songwe
Francis Kasavubu Michael...ni Mtanzania??niliposikia jina hili wakati yupo katibu wizara ya sayansi. Nilijiuliza hili swali..ni Mtanzania? Mbona jina kama Mcongo au mrundi?...

Kuna anaemjua vizuri hapa JF?

Mtu hadi anateuliwa bado unakuwa na shaka ya uraia wake??
 
Mkuu mpaka hapo basi, huyu ni fwasi ya bukavu au kwa Slimboy, Tanzania hatuna akina Kasavubu piga ua huyu atakuwa mkimbizi kama akina Shusho.
 
Huwa nawashangaa sana watanzania kwa kuwa na vitabia vya kibaguzi, hasa wakiwa na wadhifa fulani Serikalini...
Hawataki kabisa kusikia majina asilia ya Kigoma, Rukwa, na Kagera hasa pale yanapofanana na majina ya nchi jirani za DRC, Rwanda na Burundi.
Kuna wapemba, waarabu, Wahindi, waoman wacomoro na wahindi kibao wamejazana nchi hii na baadhi wako kwenye nyadhifa Serikalini kwa majina ya kiarabu, kihindi na kiajemi ....
huwezi kusikia ngozi nyeusi akihoji!... Sana sana atasilimu na kujiita Abdallah na maisha yataendelea akijisikia kuwa mtanzania halisi,tena mwenye uhalali tosha wa kuhoji watu wa makabila mengine halali ya JMT......Kasumba mbaya sana hii. 😳
 
Surnames za mipakani hasa Kigoma na hata Kagera zinaingiliana na nchi jirani.

Akina Bizimungu,Kwizera,Havyarimana utawakuta Manyovu wakiwa na ID za NIDA.
 
Mleta uzi ameuliza jina na ndicho kinachompa shaka hadi kuuliza asili ya huyo mtu na ndicho watu wanamjibu,acha kujitia ujuwaji kwa kutoa maelezo marefu ambayo mleta uzi sio hitaji lake.
Nimechagua kuwa mjuaji na wewe umechagua kuwa kilaza, hapo hakuna tatizo baki na ukilaza wako kama unakufaa.
Turudi kwenye mada, kuna tatizo gani Mtanzania akiuliza taarifa za wazi za kiongozi wa serikali?
Kuna maficho gani yanafanyika kutaja jina la kiongozi na asili yake. Mwaka 1961 tulimpata Kambarage na jina lake tunajua linatoka wapi likimaanisha nini, mwaka 2023 inakuwa ugomvi kuulizwa kwa jina la kiongozi.
 
Tatizo swali limekuja baada badala lingekuwa limekuja kabla, sasa kama kweli mrundi au mkongo itabadili nini hapa? Ndio maana kuna watu wanasema huu ni unoko kama unoko mwingine
 
Haya maelezo umeandika yanapatikana kwa urahisi tu,swali limeuliza unajua kuwa anaitwa Kasavubu? Na mtoa mada anaulizia asili ya hili jina Kasavubu.
 
Majina ya koo mtu hajipi au kupewa na mzazi, huyakuta tu. Hata kama utaitwa George Washington Mwainyekule, hiyo Mwainyekule bado itatambulisha asili yenu.

Kwani Kasabubu ni la Ukoo? Ni AKA kama za unavyoona Dr Joseph Kasheku Msukuma au Livingstone Lusinde Kibajaji au Kama Said Sued Scud.

Hao watu wana majina ya official na la kitaa ndiyo maana unaweza ukakuta huko kwao wanamuita "Franswa" au "Misheli".
 
Ni aka i ayotumika kwenye official documents!? Aisee! Hii ni kali!
 
Mkuu wa mkoa mpya wa Songwe
Francis Kasavubu Michael...ni Mtanzania??niliposikia jina hili wakati yupo katibu wizara ya sayansi. Nilijiuliza hili swali..ni Mtanzania? Mbona jina kama Mcongo au mrundi?...

Kuna anaemjua vizuri hapa JF?
Record yake ya kuzaliwa, shule, vyuo nk inasemaje
 
Mkuu wa mkoa mpya wa Songwe
Francis Kasavubu Michael...ni Mtanzania??niliposikia jina hili wakati yupo katibu wizara ya sayansi. Nilijiuliza hili swali..ni Mtanzania? Mbona jina kama Mcongo au mrundi?...

Kuna anaemjua vizuri hapa JF?
Anaweza kuwa mkongo au mrundi au UK ila kama alizaliwa Tz ni Mtanzania hivyo huna haja yakuwa na shaka naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…