Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 1,211
- 233
Tena usiishie hapo kama nimpiga kura wake next time mpige chini kuanzia utakapokutana na kumpa maswali yako wape na elimu ya urai na haki za msingi wapiga kura wa jimbo lake ili nae wambamize atakapojaribu kusimama tena.......!Nakukubali mkubwa mawazo yako . Tuliyasema haya ila Nimrod nitakutana naye Jimboni kwake nitamuuliza kulikoni katetea tajiri na kumwacha Mlalahoi analala kaburini na yeye akiwa Mbunge wa walala hoi kama anavyo jiita ?
Nakukubali mkubwa mawazo yako . Tuliyasema haya ila Nimrod nitakutana naye Jimboni kwake nitamuuliza kulikoni katetea tajiri na kumwacha Mlalahoi analala kaburini na yeye akiwa Mbunge wa walala hoi kama anavyo jiita ?
Maimamu Dar wamjia juu Rais Kikwete, Mtikila
na Prisca Nsemwa
KAMATI ya Maimamu wa Kiislamu, wamewajia juu Rais Jakaya Kikwete na Mchungaji Christopher Mtikila katika masuala mawili nyeti.
Kubwa lililosababisha maimamu hao kumjia kuu Rais Kikwete ni kushindwa kwa serikali yake kuanzisha Mahakama ya Kadhi kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2005.
Maimamu hao walimlaumu Kikwete na CCM kwa kile walichokieleza kutumia ajenda ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi ili kujihakikishia kura zao kabla ya kuiweka ahadi hiyo kando.
Kwa upande wa Mtikila, maimamu hao, walieleza kushangazwa na uamuzi wa kiongozi huyo wa kisiasa kuivalia njuga kesi inayomkabilia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditoplie Mzuzuri.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Msikiti wa Mtoro jana, Katibu wa Kamati ya Maimamu, Sheikh Khalifa Khamisi, alimtaka Rais Kikwete kuhakikisha anatekeleza haraka, ahadi yake ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi.
Sheikh Khamis alisema kuwa ahadi hiyo iliwavuta Waislamu wengi ambao walimchagua Kikwete kwa matarajio kuwa hamu yao ya kuwa na mahakama yao, itatimia. Hata hivyo, Sheikh Khamis alisema kuwa muda unapita sasa na hakuna dalili kuwa Kikwete ana mpango wa kutekeleza ahadi hiyo hivyo wameona ni vema wamkumbushe.
Alisema kuwa ni vema Kikwete akahakikisha kuwa Mahakama ya Kadhi inaanzishwa kama alivyoahidi la sivyo, watazidai kura zao kwani walizitoa wakiwa na matumaini kuwa zitawasaidia kupata chombo hicho muhimu katika masuala ya dini yao.
Alisema kuwa mahakama hiyo ni jambo la msingi kwa Waislamu na ndiyo maana hawakutilia maanani ahadi zilizotolewa na wagombea wengine wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita.
Tunashangaa sana, tunaona shule zinajengwa na misaada inapelekwa katika mikoa mbalimbali kuwasaidia watu wenye shida, lakini Mahakama ya Kadhi imesahaulika. Sasa ahadi hii isipotimizwa kura zetu tulizompa Kikwete tutazitaka, alisema Sheikh Khamis.
Alisema wakati ahadi nyingine zikitekelezwa moja baada ya nyingine, suala la Mahakama ya Kadhi limesahaulika kabisa. Alisema kuwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi kutawasaidia Waislamu kote nchini, kwa kuwa itashughulikia mambo ya ndoa, mirathi na mambo mengine yatakayowahusu Waislamu.
Sheikh Khamis alipogeukia suala la Mchungaji Mtikila, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic, alimtaka aache mara moja kujihusisha na kesi inayomhusu Ditopile. Sheikh Khamis alisema Waislamu na watu wengine wote wanatambua kuwa tuhuma zinazomkabili Ditopile ni za jinai na inapendeza kuona kuwa suala hilo lililokwishafikishwa katika mahakama ambacho ndicho chombo kinachoshughulikia masuala ya kijinai likiachwa huko huko.
Mtikila hana haja ya kuingilia uwezo wa mahakama kuhusu kesi ya Ditopile, anatakiwa asubiri (uamuzi wa mahakama) ndipo akate rufaa haina haja kwa wanasiasa kujiingiza kwenye kesi hiyo, waiachie mahakama ifanye kazi yake, alisema Khamis.
Kauli hiyo inakuja wakati Mtikila akiwa ameshatangaza azima yake ya kufungua kesi mahakamani kupinga kubadilishwa kwa mashitaka yanayomkabili Ditopile kutoka mauaji na kuwa mauaji ya bila kukusudia.
Katika hoja zake, Mtikila anaeleza kuwa duniani kote, hakuna kosa lijulikanalo kama mauaji bila kukusudia bali linalotambulika ni la mauaji. Jaji anayesikiliza kesi ndiye mwenye uwezo wa kutamka baada ya kusikiliza ushahidi wote kuwa mtuhumiwa hakuua kwa kukusudia tunashangaa, mwendesha mashitaka amepata wapi mamlaka ya kuamua kuwa Ditopile aliua bila kukusudia, alisema Mtikila alipozungumza na gazeti hili juzi.
Hata hivyo, Sheikh Khamis alisema kuwa Mtikila hana uwezo wa kuilazimisha mahakama kufanya kazi kama anavyotaka yeye, bali mahakama inafuata taratibu za kisheria.
Alisema kuwa si kwamba Waislamu wanamtetea Ditopile, bali katika uongozi wake hakuwahi kupatikana na tuhuma za ujambazi wala ukatili, na kuamini kuwa tukio hilo lilikuwa ni bahati mbaya.
Aidha, alisema hakuna sababu za kuonyesha chuki kwa Ditopile na mahakama inatakiwa ipewe fursa ya kufuata sheria inavyosema kabla ya kufanya maamuzi yanayostahili.
dini nayo imo...
Jembajemba,
Hapo ni harufu mbaya, tafisiri yake inatisha kwa mustakabadhi wa taifa letu kwa siku za soni.
Story gani ya ajabu ambayo unaifikiria ingetokea ?Ulikuwa unamaanisha nini ulipoandika Dereva mbonde akawa kama alivyo?Jembajemba,
hapa inanipa picha mbaya laiti Dito angekuwa kafiri na na dereva Mbode akawa kama alivyo na mambo yangekuwa kama yalivyokwenda nafikiri story ya ajabu saana ingetoka kwa hawa maimamu.
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Licha ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu hivi karibuni, baada ya kusota mahabusu kwa miezi kadhaa kutokana na kesi anayotuhumiwa kuua mtu bila ya kukusudia, imefahamika kuwa mambo bado hayajawa shwari sana kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Kapteni Mstaafu Ditopile Mzuzuri.
Imefahamika kuwa sababu hasa ya mambo ya Dito kutokuwa shwari ni tishio la kufunguliwa kesi mpya tano, zote zenye nia ya kuishawishi mahakama iamini kuwa Dito anastahili kushitakiwa kwa `kuua` na sio `kuua bila ya kukusudia`.
Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu jana, Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye ndiye aliyeshupalia jambo hilo, kwa kile anachosema kuwa ni kupigania haki za wanyonge, amesema hivi sasa yuko kamili kwa ajili ya kesi hizo mpya kwa Dito na wakati wowote kuanzia sasa atazuka kortini na Dito lazima arejee rumande.
Hivi sasa, Dito aliyeachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu, anatuhumiwa kumuua bila ya kukusudia dereva wa daladala Hassan Mbonde. Lakini, Mchungaji Mtikila ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha DP, amesema piga ua, lazima afungue kesi mpya tano ili Dito arudishwe rumande kwa kile anachodai kuwa ni kutendeka kwa haki.
Akasema Mchungaji Mtikila kuwa licha ya kutangaza kusudia lake hilo kwa siku kadhaa sasa, alitulia kwa muda ili kukamilisha mambo fulani muhimu kabla ya kutua rasmi kortini. Nilikuwa nikikusanya maelezo muhimu ya kunisaidia katika kumbana Ditopile na hatimaye kushuhudia haki ikitendeka. kwa kosa hili anapaswa kuwa rumande hivi sasa, akasema Mchungaji Mtikila.
Aidha, Mtikila amesema hivi sasa anakamilisha mambo mengine muhimu na wanasheria wake kabla ya kutua kortini na kutekeleza azma yake hiyo wakati wowote kuanzia sasa. Akazitaja kesi hizo tano mpya kwa Dito kuwa ni pamoja na ile anayodai imeendeshwa kimizengwe ili kumuokoa Dito - ambayo ni ya Kuua kwa kukusudia'.
Nyingine, akasema Mtikila kuwa ni ya madai ya fidia ambayo yenyewe, anadai ameombwa kuifungua na wanafamilia wa marehemu. Kesi ya tatu, Mtikila ameitaja kuwa ni ya Dito kudharau mahakama, tangu kesi ya mtuhumiwa ilipokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na pia katika Korti Kuu ambako alidiriki hata kupitia katika milango ambayo watuhumiwa huwa hawaruhusiwi kuitumia.
Kesi nyingine ameitaja kuwa ni ya Dito na ndugu zake kuwashambulia waandishi wa habari katika siku aliyopewa dhamana na Mahakama Kuu. Kwa mujibu wa Mtikila, kesi ya tano anayokusudia kumfungulia Dito ni ya ndugu zake kuwanyima wananchi haki yao ya kupata habari kwa kuwazuia waandishi kufanya kazi yao katika siku ya kesi yake.
Niko katika mawasiliano na baadhi ya vituo vya luninga ili nipate mikanda nitakayoitumia kama sehemu ya ushahidi, akasema Mtikila. Dito anakabiliwa na kesi ya kumuua dereva Mbonde bila kukusudia mnamo Novemba 4 mwaka jana, kosa analotuhumiwa kulifanya katika eneo la njia panda ya Kawe na Barabara ya Bagamoyo Jjijini Dar es Salaam.
Dito awaokoa mahabusu
2007-07-31
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Kwa maneno mafupi unaweza kusema kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, imefungua ukurasa mpya wa neema kwa mahabusu walio katika magereza mbalimbali nchini.
Kutokana na changamoto zilizoambatana na kesi hiyo, sasa kilio cha muda mrefu na machungu ya mahabusu hao, Serikali imekisikia na imetangaza mikakati kabambe ya kumaliza kero hizo.
Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi katika wizara yake jana, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Mary Nagu alitangaza hatua kadhaa ambazo Serikali itachukua ili kuboresha mchakato wa kupatikana kwa haki nchini.
Kwa mujibu wa Dk. Nagu, Serikali itajenga mahakama nyingine nyingi zaidi ili hatimaye kupunguza mlundikano wa kesi kama ilivyo sasa na hatimaye haki kupatikana kwa haraka.
Akasema Dk. Nagu katika hotuba yake hiyo alisema kuwa Serikali ina mpango wa kuajiri mahakimu wengi zaidi na hivyo kupunguza mlundikano wa kesi zinazoshughulikiwa na mahakimu wa sasa.
Aidha, Waziri alisema kesi zitashughulikiwa kwa haraka zaidi na wakati mapambano dhidi ya rushwa katika vyombo vya kutetea haki yataongezwa mara dufu.
Pia tutawasisitiza wanasheria kuzingatia maadili ya kazi zao, alisema Dk. Nagu.
Hatua hizo zimekuja huku ikiwa ni miezi michache tangu mahabusu walipogoma wakilalamikia kile walichodai kuwa kesi zao zinachelewa.
Ditopile anakabiliwa kesi ya kumuua bila kukusudia dereva wa daladala Hassan Mbonde, mnamo Novemba 4 mwaka jana.
Alipofikishwa mahakamani, kesi yake ilikwenda fasta fasta katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na suala lake likafikishwa Mahakama Kuu ambako baadaye aliweza kuachiwa kwa dhamana.
Baada ya hapo, mahabusu wa magereza kadhaa nchini wakafanya mgomo, wakipinga kesi zao kucheleweshwa kila mara kwa maelezo kuwa upelelezi haujakamilika.
Wakataka na wao kesi zao ziende haraka kama ilivyokuwa ya Dito.
Serikali ilijibu malalamiko ya mahabusu hao kwa kuahidi kushughulikia tatizo moja baada ya jingine ambapo sasa, mambo yameanza kuwa swafi kutokana na hatua kadhaa zilizotangazwa na Waziri Nagu jana.
- SOURCE: Alasiri
Lucas Raphael, Tabora
HabariLeo; Thursday,August 09, 2007 @00:02
MAMIA ya watu akiwamo aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile –Mzuzuri walijitokeza jana kumzika aliyekuwa Waziri wa Kwanza wa Sheria nchini, Chifu Abdallah Fundikira (86).
Chifu Fundikira (86) ambaye alikuwa Waziri katika Serikali ya Tanganyika kuanzia mwaka 1959 hadi 1964, alifariki dunia wiki hii nyumbani kwake mjini hapa kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.
Ditopile- Mzuzuri ambaye alijiuzulu ukuu wa mkoa baada ya kukabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia mwaka jana, alikuwa miongoni mwa mamia walioshiriki mazishi ya mwanasiasa huyo ambayo yaliongozwa na Rais Jakaya Kikwete.
Mkuu huyo wa mkoa wa zamani alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliotambulishwa kwenye msiba huo. Alitambulishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Moshi Shang'a akimuita mheshimiwa.
Lakini Ditopile Mzuzuri alisema kuwa: "Kibinadamu unaweza ukawa mheshimiwa lakini ikafikia wakati ukaitwa mzee. Hivi sasa mimi naitwa Mzee wa Wanyamwezi."
Katika mazishi hayo yaliyoongozwa na Sheikh Mohamed Mbega wanasiasa wengine wakongwe waliohudhuria ni Sir George Kahama na Mzee Rashidi Kawawa.
Rais Kikwete ndiye aliongoza waombolezaji hao kuweka mchanga katika kaburi na akafuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Malecela.
Akizungumza kwa niaba ya familia, Naibu Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliwashukuru watu wote walioshiriki katika maziko hayo yaliyofanyika katika eneo la Utemi wa utawala wake linalojulikana kama Itetemya.
Chifu Fundikira alizaliwa Februari 2, 1921 akiwa ni mtoto wa kwanza wa familia ya Mzee Said Fundikira. Alisoma Shule ya Msingi Bagamoyo kati ya mwaka 1933 na 1935.
Na alionekana kwenye picha za TVT siku hiyo.Dito aibuka maziko ya Chifu Fundikira
Muuaji huyu amekwenda kuibukia Tabora. Hivi naye anathamini maisha kweli baada ya kuua kwa makusudi vile?