Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Nakukubali mkubwa mawazo yako . Tuliyasema haya ila Nimrod nitakutana naye Jimboni kwake nitamuuliza kulikoni katetea tajiri na kumwacha Mlalahoi analala kaburini na yeye akiwa Mbunge wa walala hoi kama anavyo jiita ?
Tena usiishie hapo kama nimpiga kura wake next time mpige chini kuanzia utakapokutana na kumpa maswali yako wape na elimu ya urai na haki za msingi wapiga kura wa jimbo lake ili nae wambamize atakapojaribu kusimama tena.......!
 
Shekhe jino kwa jino na Mchungaji kuhusu Dito

Habari Zinazoshabihiana
• Mufti avunja uongozi BAKWATA 16.02.2007 [Soma]
• Kesi ya Dito sasa yaingia msikitini 21.03.2007 [Soma]
• Shekhe, wafuasi 15 mbaroni kwa kuzuia mazishi 04.01.2007 [Soma]

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Kamati ya Maimamu ya Kuokoa Mali za Waislamu Tanzania Shekhe Khalifa Khamis, amemjia juu Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, akimtaka aache kuingilia masuala ya mahakama katika kesi ya mauaji ya bila kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Ditopile Mzuzuri.

Sheikh Khalifa alitsema hayo jana kutokana na kauli za hivi karibuni za Mchingaji Mtikila ambazo amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akieleza kupinga hatua ya Bw. Ditopile kufunguliwa mashitaka ya kuua bila kukusudia na kutaka afunguliwe ya mauaji ya kukusudia.

"Tunashangazwa sana na kauli hizi za Mtikila, akiwa kiongozi wa kisiasa. Katika Uislamu, sheria inasema mtu yeyote anayetuhumiwa kuua iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya, ni lazima ashitakiwe. Ditopile ameshitakiwa basi tuiachie mahakama.

"Kauli za Mtikila kuwa mashitaka aliyopaswa kufunguliwa Bw. Ditopile ni ya mauaji ya kukusudia hazina msingi, kwa sababu yeye hana nguvu wala dhamana ya kuingilia utaratibu wa mashitaka na mwenendo wa mahakama," alisema.

Akifafanua zaidi suala hilo, Shekhe Khalifa alisema watu wote wanaomfahamu Bw. Ditopile wanaujua unyenyekevu wake na namna alivyokuwa kipenzi cha watu.

"Ditopile si jambazi na wala si mtu katili, wanaomfahamu tangu akiwa mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Lindi, Pwani na Tabora, wanamjua jinsi alivyo mtu mwenye bashasha na mkarimu. Kilichomtokea ni dhahiri halikuwa jambo la kukusudia," alitetea Shekhe Khalifa.

Alimtaka Mtikila aache kuingilia masuala yasiyomhusu na kuhoji uanaharakati wa mwanasiasa huyo katika matukio mengine.

"Hivi karibuni kesi ilitokea Songea. Kuna kijana alikutwa na meno ya tembo akafungwa miaka minane. Padri akakutwa na kosa kama hilo akafungwa dakika 45 tu. Mbona Mtikila hakukata rufaa dhidi ya adhabu ndogo aliyopewa Padri huyo? Tunamwomba aache kuingilia masuala yasiyomhusu," alisisitiza.

Mchungaji Mtikila amekuwa akisisitiza kuwa anakamilisha taratibu na mawakili wake kutaka kufungua kesi ya kikatiba kuomba pamoja na mambo mengine, amri za certiorari na mandamus, ambazo zinaitaka Mahakama Kuu ya Tanzania kuuamuru upande wa upelelezi, ufuate kanuni za kisheria kwa kumfungulia Bw. Ditopile mashitaka ya mauaji, ambayo anaamini ndiyo ambayo yanathibiti kwa mujibu wa ushahidi uliopo

Wanabodi,

Je wanabodi katika hili munasemaje???
 
Nakukubali mkubwa mawazo yako . Tuliyasema haya ila Nimrod nitakutana naye Jimboni kwake nitamuuliza kulikoni katetea tajiri na kumwacha Mlalahoi analala kaburini na yeye akiwa Mbunge wa walala hoi kama anavyo jiita ?

Mzee ni Nimrodi ni mtu wa kufuatilia pale pesa ilipo tu; huu ubunge ni mahala pa kupumzikia tu. Kuna wakati alisema kuwa serikali haisomi mikataba sawasawa ndiyo maana wanaingizwa mkenge lakini, yeye ndiye aliyekuwa "PRIVATIZATION LEGAL ADVISOR & CONSULTANT wa serikali hiyo hiyo ambayo iliingizwa mkenge na mashirika kama SAA kwenye swala la ATC. Hebu angalia kweye Excel file iliyoko hapa. Itabidi usearch "Mkono" kwa vile waliopata ulaji huo ni wengi kidogo; pesa yenyewe iko katika US$.
 
Maimamu Dar wamjia juu Rais Kikwete, Mtikila
na Prisca Nsemwa

KAMATI ya Maimamu wa Kiislamu, wamewajia juu Rais Jakaya Kikwete na Mchungaji Christopher Mtikila katika masuala mawili nyeti.

Kubwa lililosababisha maimamu hao kumjia kuu Rais Kikwete ni kushindwa kwa serikali yake kuanzisha Mahakama ya Kadhi kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2005.

Maimamu hao walimlaumu Kikwete na CCM kwa kile walichokieleza kutumia ajenda ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi ili kujihakikishia kura zao kabla ya kuiweka ahadi hiyo kando.

Kwa upande wa Mtikila, maimamu hao, walieleza kushangazwa na uamuzi wa kiongozi huyo wa kisiasa kuivalia njuga kesi inayomkabilia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditoplie Mzuzuri.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Msikiti wa Mtoro jana, Katibu wa Kamati ya Maimamu, Sheikh Khalifa Khamisi, alimtaka Rais Kikwete kuhakikisha anatekeleza haraka, ahadi yake ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

Sheikh Khamis alisema kuwa ahadi hiyo iliwavuta Waislamu wengi ambao walimchagua Kikwete kwa matarajio kuwa hamu yao ya kuwa na mahakama yao, itatimia. Hata hivyo, Sheikh Khamis alisema kuwa muda unapita sasa na hakuna dalili kuwa Kikwete ana mpango wa kutekeleza ahadi hiyo hivyo wameona ni vema wamkumbushe.

Alisema kuwa ni vema Kikwete akahakikisha kuwa Mahakama ya Kadhi inaanzishwa kama alivyoahidi la sivyo, watazidai kura zao kwani walizitoa wakiwa na matumaini kuwa zitawasaidia kupata chombo hicho muhimu katika masuala ya dini yao.

Alisema kuwa mahakama hiyo ni jambo la msingi kwa Waislamu na ndiyo maana hawakutilia maanani ahadi zilizotolewa na wagombea wengine wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita.

“Tunashangaa sana, tunaona shule zinajengwa na misaada inapelekwa katika mikoa mbalimbali kuwasaidia watu wenye shida, lakini Mahakama ya Kadhi imesahaulika. Sasa ahadi hii isipotimizwa kura zetu tulizompa Kikwete tutazitaka,” alisema Sheikh Khamis.

Alisema wakati ahadi nyingine zikitekelezwa moja baada ya nyingine, suala la Mahakama ya Kadhi limesahaulika kabisa. Alisema kuwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi kutawasaidia Waislamu kote nchini, kwa kuwa itashughulikia mambo ya ndoa, mirathi na mambo mengine yatakayowahusu Waislamu.

Sheikh Khamis alipogeukia suala la Mchungaji Mtikila, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic, alimtaka aache mara moja kujihusisha na kesi inayomhusu Ditopile. Sheikh Khamis alisema Waislamu na watu wengine wote wanatambua kuwa tuhuma zinazomkabili Ditopile ni za jinai na inapendeza kuona kuwa suala hilo lililokwishafikishwa katika mahakama ambacho ndicho chombo kinachoshughulikia masuala ya kijinai likiachwa huko huko.

“Mtikila hana haja ya kuingilia uwezo wa mahakama kuhusu kesi ya Ditopile, anatakiwa asubiri (uamuzi wa mahakama) ndipo akate rufaa… haina haja kwa wanasiasa kujiingiza kwenye kesi hiyo, waiachie mahakama ifanye kazi yake,” alisema Khamis.

Kauli hiyo inakuja wakati Mtikila akiwa ameshatangaza azima yake ya kufungua kesi mahakamani kupinga kubadilishwa kwa mashitaka yanayomkabili Ditopile kutoka mauaji na kuwa mauaji ya bila kukusudia.

Katika hoja zake, Mtikila anaeleza kuwa duniani kote, hakuna kosa lijulikanalo kama mauaji bila kukusudia bali linalotambulika ni la mauaji. “Jaji anayesikiliza kesi ndiye mwenye uwezo wa kutamka baada ya kusikiliza ushahidi wote kuwa mtuhumiwa hakuua kwa kukusudia… tunashangaa, mwendesha mashitaka amepata wapi mamlaka ya kuamua kuwa Ditopile aliua bila kukusudia,” alisema Mtikila alipozungumza na gazeti hili juzi.

Hata hivyo, Sheikh Khamis alisema kuwa Mtikila hana uwezo wa kuilazimisha mahakama kufanya kazi kama anavyotaka yeye, bali mahakama inafuata taratibu za kisheria.

Alisema kuwa si kwamba Waislamu wanamtetea Ditopile, bali katika uongozi wake hakuwahi kupatikana na tuhuma za ujambazi wala ukatili, na kuamini kuwa tukio hilo lilikuwa ni bahati mbaya.

Aidha, alisema hakuna sababu za kuonyesha chuki kwa Ditopile na mahakama inatakiwa ipewe fursa ya kufuata sheria inavyosema kabla ya kufanya maamuzi yanayostahili.

dini nayo imo...
 
Hili swala huwa siliewi maana yake. Kuna tofuti gani kati ya mahakama ya Kadhi na mahakama ya kawaida? Je Mahakama ya kadhi inasikiliza kesi zinazohusu sheria za dini tu au inasikiliza kesi zinazohuss sheria za nchi kama zilivyotungwa na bunge? Je ni kwa nini mahakama ya Kadhi inadaiwa sana na waislamu?

Jembajemba,
Hapo ni harufu mbaya, tafisiri yake inatisha kwa mustakabadhi wa taifa letu kwa siku za soni, maana busara haikutumika kwa viongozi wa dini kuanza jkujiiingiza namna hii, hapa inanipa picha mbaya laiti Dito angekuwa kafiri na na dereva Mbode akawa kama alivyo na mambo yangekuwa kama yalivyokwenda nafikiri story ya ajabu saana ingetoka kwa hawa maimamu. Kuhusu wakili Nimrod, wote wanamjua kuwa Nimrod si advocate mzuri yeye kesi zake zote huwanunua mahakimu au Jaji, down to earth corrupt.
 
Jembajemba,
hapa inanipa picha mbaya laiti Dito angekuwa kafiri na na dereva Mbode akawa kama alivyo na mambo yangekuwa kama yalivyokwenda nafikiri story ya ajabu saana ingetoka kwa hawa maimamu.
Story gani ya ajabu ambayo unaifikiria ingetokea ?Ulikuwa unamaanisha nini ulipoandika Dereva mbonde akawa kama alivyo?
 
2007-04-12 16:02:39
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Licha ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu hivi karibuni, baada ya kusota mahabusu kwa miezi kadhaa kutokana na kesi anayotuhumiwa kuua mtu bila ya kukusudia, imefahamika kuwa mambo bado hayajawa shwari sana kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Kapteni Mstaafu Ditopile Mzuzuri.

Imefahamika kuwa sababu hasa ya mambo ya Dito kutokuwa shwari ni tishio la kufunguliwa kesi mpya tano, zote zenye nia ya kuishawishi mahakama iamini kuwa Dito anastahili kushitakiwa kwa `kuua` na sio `kuua bila ya kukusudia`.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu jana, Mchungaji Christopher Mtikila, ambaye ndiye aliyeshupalia jambo hilo, kwa kile anachosema kuwa ni kupigania haki za wanyonge, amesema hivi sasa yuko kamili kwa ajili ya kesi hizo mpya kwa Dito na wakati wowote kuanzia sasa atazuka kortini na Dito lazima arejee rumande.

Hivi sasa, Dito aliyeachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu, anatuhumiwa kumuua bila ya kukusudia dereva wa daladala Hassan Mbonde. Lakini, Mchungaji Mtikila ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha DP, amesema piga ua, lazima afungue kesi mpya tano ili Dito arudishwe rumande kwa kile anachodai kuwa ni kutendeka kwa haki.

Akasema Mchungaji Mtikila kuwa licha ya kutangaza kusudia lake hilo kwa siku kadhaa sasa, alitulia kwa muda ili kukamilisha mambo fulani muhimu kabla ya kutua rasmi kortini. Nilikuwa nikikusanya maelezo muhimu ya kunisaidia katika kumbana Ditopile na hatimaye kushuhudia haki ikitendeka. kwa kosa hili anapaswa kuwa rumande hivi sasa, akasema Mchungaji Mtikila.

Aidha, Mtikila amesema hivi sasa anakamilisha mambo mengine muhimu na wanasheria wake kabla ya kutua kortini na kutekeleza azma yake hiyo wakati wowote kuanzia sasa. Akazitaja kesi hizo tano mpya kwa Dito kuwa ni pamoja na ile anayodai imeendeshwa kimizengwe ili kumuokoa Dito - ambayo ni ya Kuua kwa kukusudia'.

Nyingine, akasema Mtikila kuwa ni ya madai ya fidia ambayo yenyewe, anadai ameombwa kuifungua na wanafamilia wa marehemu. Kesi ya tatu, Mtikila ameitaja kuwa ni ya Dito kudharau mahakama, tangu kesi ya mtuhumiwa ilipokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na pia katika Korti Kuu ambako alidiriki hata kupitia katika milango ambayo watuhumiwa huwa hawaruhusiwi kuitumia.

Kesi nyingine ameitaja kuwa ni ya Dito na ndugu zake kuwashambulia waandishi wa habari katika siku aliyopewa dhamana na Mahakama Kuu. Kwa mujibu wa Mtikila, kesi ya tano anayokusudia kumfungulia Dito ni ya ndugu zake kuwanyima wananchi haki yao ya kupata habari kwa kuwazuia waandishi kufanya kazi yao katika siku ya kesi yake.

Niko katika mawasiliano na baadhi ya vituo vya luninga ili nipate mikanda nitakayoitumia kama sehemu ya ushahidi, akasema Mtikila. Dito anakabiliwa na kesi ya kumuua dereva Mbonde bila kukusudia mnamo Novemba 4 mwaka jana, kosa analotuhumiwa kulifanya katika eneo la njia panda ya Kawe na Barabara ya Bagamoyo Jjijini Dar es Salaam.

Tunasubiri kwa hamu.

SOURCE: Alasiri
 
Mtikila anyumbulisha kesi ya Ditopile
*Afungua nyingine kutaka arejeshewe kesi ya mauaji
*Adai ushahidi unaonyesha aliua kwa makusudi

MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amefungua kesi ya katiba katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba mahakama hiyo ifungue upya kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ili iwe ya kuua kwa kukusudia.

Kesi hiyo namba 41 ilifunguliwa jana katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam majira ya saa 6.30 mchana na Mtikila mwenyewe.

Kesi hiyo imewasilishwa mahakamani hapo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika kesi hiyo, Mtikila ameomba mahakama imruhusu kumshtaki binafsi Ditopile badala ya DPP na aliwasilisha hoja 17 akitaka kesi hiyo ifunguliwe upya, na maafisa wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama Kuu wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuzuia haki isitendeke.

Pia, ameiomba Mahakama Kuu iwachukulie hatua za kisheria waliokuwa walinzi na wasindikizaji wa Ditopile ambao walishiriki kudharau Mahakama ya Kisutu na Mahakama Kuu kwa kitendo cha kuwazuia na kuwapiga waandishi wa habari na kuwasababishia maumivu.

Mtikila pia anaiomba mahakama hiyo iendeshe kesi hiyo mpya aliyofungua kupitia wakili wa kujitegemea.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari1.asp
 
ninamsapoti mzee tikila kupigania haki bila kujali cheo na fedha za mtu
 
Hivi huyu muuaji yuko wapi au wamekwisha tuzuga?
 
Dito awaokoa mahabusu

2007-07-31
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Kwa maneno mafupi unaweza kusema kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, imefungua ukurasa mpya wa neema kwa mahabusu walio katika magereza mbalimbali nchini.

Kutokana na changamoto zilizoambatana na kesi hiyo, sasa kilio cha muda mrefu na machungu ya mahabusu hao, Serikali imekisikia na imetangaza mikakati kabambe ya kumaliza kero hizo.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi katika wizara yake jana, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Mary Nagu alitangaza hatua kadhaa ambazo Serikali itachukua ili kuboresha mchakato wa kupatikana kwa haki nchini.

Kwa mujibu wa Dk. Nagu, Serikali itajenga mahakama nyingine nyingi zaidi ili hatimaye kupunguza mlundikano wa kesi kama ilivyo sasa na hatimaye haki kupatikana kwa haraka.

Akasema Dk. Nagu katika hotuba yake hiyo alisema kuwa Serikali ina mpango wa kuajiri mahakimu wengi zaidi na hivyo kupunguza mlundikano wa kesi zinazoshughulikiwa na mahakimu wa sasa.

Aidha, Waziri alisema kesi zitashughulikiwa kwa haraka zaidi na wakati mapambano dhidi ya rushwa katika vyombo vya kutetea haki yataongezwa mara dufu.

“Pia tutawasisitiza wanasheria kuzingatia maadili ya kazi zao,” alisema Dk. Nagu.

Hatua hizo zimekuja huku ikiwa ni miezi michache tangu mahabusu walipogoma wakilalamikia kile walichodai kuwa kesi zao zinachelewa.

Ditopile anakabiliwa kesi ya kumuua bila kukusudia dereva wa daladala Hassan Mbonde, mnamo Novemba 4 mwaka jana.

Alipofikishwa mahakamani, kesi yake ilikwenda fasta fasta katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na suala lake likafikishwa Mahakama Kuu ambako baadaye aliweza kuachiwa kwa dhamana.

Baada ya hapo, mahabusu wa magereza kadhaa nchini wakafanya mgomo, wakipinga kesi zao kucheleweshwa kila mara kwa maelezo kuwa upelelezi haujakamilika.

Wakataka na wao kesi zao ziende haraka kama ilivyokuwa ya Dito.

Serikali ilijibu malalamiko ya mahabusu hao kwa kuahidi kushughulikia tatizo moja baada ya jingine ambapo sasa, mambo yameanza kuwa ‘swafi’ kutokana na hatua kadhaa zilizotangazwa na Waziri Nagu jana.
  • SOURCE: Alasiri
  • Hapa ndipo tumeisahau hii, lakini bado iko kwenye pipe mzee Dua! Tunatakiwa kuikomalia mpaka kieleweke. They can't fool us to that extent! Dito si ajabu ukasikia ni mkuu wa wilaya flani soon!
 
Kuna kipindi hapo siku za nyuma alikuwa anatafutiwa kibali cha kusafiri nje ya Nchi kwa ajili ya matibabu.Hakuna habari za Uhakika kama aliondoka au bado anafanyiwa matibabu ndani ya Nchi,lakini wale waliokuwa wanamuhudumia hapo MMC wanasema haendi hapo tena!na hawana Taarifa yoyote kuhusu mgonjwa wao huyo!,Labda anafanyiwa Matibabu Lugalo au Agakhan.
 
mambo kimya kimya..ditto ndio yuko huru tena...hakuna tena kesi hapo...ile kasi ya kusikiliza kesi kabla hajapata dhamana..imekwisha baada ya dhamana ..na tangu ameachiwa kesi haijatajwa tena...duh kali hii!!!!!

alafu naona siku hizi ditto staili mahakamani imekuwa fasheni..nimeona tvt majambazi wanafikishwa mahakamani wameiga uvaaji wa pama kama ditto ili kujificha na wapiga picha!!!!
 
Wa-Tanzania mambo mengine inabidi tunyamaze tu yaishe, maana ubavu wa kuikaba koo serikali yetu hatuna,

Mtikila alipojaribu kuikaba koo serikali, alitumiwa ujumbe na Wa-Isilamu kuwa aache mara moja, na yeye akakubali yakaisha,

Tatizo sio serikali, bali ni sisi wananchi wenyewe!
 
Dito aibuka maziko ya Chifu Fundikira

Lucas Raphael, Tabora

HabariLeo; Thursday,August 09, 2007 @00:02
MAMIA ya watu akiwamo aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile –Mzuzuri walijitokeza jana kumzika aliyekuwa Waziri wa Kwanza wa Sheria nchini, Chifu Abdallah Fundikira (86).

Chifu Fundikira (86) ambaye alikuwa Waziri katika Serikali ya Tanganyika kuanzia mwaka 1959 hadi 1964, alifariki dunia wiki hii nyumbani kwake mjini hapa kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.

Ditopile- Mzuzuri ambaye alijiuzulu ukuu wa mkoa baada ya kukabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia mwaka jana, alikuwa miongoni mwa mamia walioshiriki mazishi ya mwanasiasa huyo ambayo yaliongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mkuu huyo wa mkoa wa zamani alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliotambulishwa kwenye msiba huo. Alitambulishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Moshi Shang'a akimuita mheshimiwa.

Lakini Ditopile Mzuzuri alisema kuwa: "Kibinadamu unaweza ukawa mheshimiwa lakini ikafikia wakati ukaitwa mzee. Hivi sasa mimi naitwa Mzee wa Wanyamwezi."

Katika mazishi hayo yaliyoongozwa na Sheikh Mohamed Mbega wanasiasa wengine wakongwe waliohudhuria ni Sir George Kahama na Mzee Rashidi Kawawa.

Rais Kikwete ndiye aliongoza waombolezaji hao kuweka mchanga katika kaburi na akafuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Malecela.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Naibu Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliwashukuru watu wote walioshiriki katika maziko hayo yaliyofanyika katika eneo la Utemi wa utawala wake linalojulikana kama Itetemya.

Chifu Fundikira alizaliwa Februari 2, 1921 akiwa ni mtoto wa kwanza wa familia ya Mzee Said Fundikira. Alisoma Shule ya Msingi Bagamoyo kati ya mwaka 1933 na 1935.

Muuaji huyu amekwenda kuibukia Tabora. Hivi naye anathamini maisha kweli baada ya kuua kwa makusudi vile?
 
Dito aibuka maziko ya Chifu Fundikira

Muuaji huyu amekwenda kuibukia Tabora. Hivi naye anathamini maisha kweli baada ya kuua kwa makusudi vile?
Na alionekana kwenye picha za TVT siku hiyo.
 
Back
Top Bottom