Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkandara
Kumbe nawe unaweza kuchekesha.

Kama imefikia mpaka kiwango cha Mkandara kutengenza mchezo wa kuigiza basi kweli hali ya Tanzania ni mbaya kupindukia.
 
Aljazeera,

- Wananchi Tumechoka, Viongozi Hawajitambui

Ukiwa na wacheza sinema inakulazimu nawe uwe na usanii fulani laa sivyo CV yako mbovu. Hata hivyo Mzee MNKJJ kasema sikuwa mbali sana, unajua tena sinema za Kihindi!
 
Waandishi Wetu
HabariLeo; Saturday,March 10, 2007 @00:07

MAHAKAMA Kuu imeagiza Jeshi la Polisi kuchukua hatua haraka dhidi ya waliohusika kumpitisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile-Mzuzuri katika mlango wa kuingilia majaji wa mahakama hiyo. Imesema iwapo polisi watazembea kuwachuliwa hatua, yenyewe itachukua hatua za kisheria dhidi yao.

Msajili wa Mahakama Kuu, Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Prophir Lyimo aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa bado mahakama inalitathimini suala hilo la mlango huo kutumiwa na mshitakiwa, kitendo ambacho hakijawahi kufanyika nchini na ni kinyume cha taratibu na sheria za mahakama.

Alisisitiza kuwa polisi walifanya makosa kumpitisha mlangoni hapo Ditopile-Mzuzuri anayekabiliwa na kesi ya kuumua bila kukusudia, dereva wa daladala, Hassan Mbonde.

“Hakuna mshitakiwa yeyote aliyewahi kupitishwa katika mlango huo ambao hutumiwa na majaji pekee. Polisi walifanya makosa makubwa kumpitisha mshitakiwa hapo na waliingilia na kuvuruga utaratibu wa Mahakama,” alisema Lyimo.

Alisema pia kuwa Mahakama wiki ijayo itatoa tamko juu ya vurugu zinazodaiwa kusababishwa na ndugu wa Ditopile-Mzuzuri dhidi ya waandishi wa habari na wapiga picha. Polisi waliokuwa katika sare na raia wanaodaiwa kuwa ndugu zake Ditopile - Mzuzuri walimpitisha katika mlango wa majaji kwa nguvu baada ya kudaiwa kumpiga kikumbo mlinzi wa Mahakama Kuu.

Mlinzi huyo naye alisikika akieleza kuwa anahofia kupoteza kazi baada ya kuamriwa kuandika barua ya kujieleza alikuwa wapi wakati lango hilo likitumika kwa watu wasio majaji.

Jumatano ya wiki hii, Ditopile- Mzuzuri alipelekwa mahakamani hapo akiwa amechelewa na kurudishwa tena rumande Keko na ilielezwa kuwa gari aina ya Baloon iliyompeleka hapo iliegesha upande huo wa majaji hadi ilipoondoka. Naye Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, ameiomba radhi Mahakama Kuu na waandishi wa habari kutokana na vitendo vya vurugu na uvunjaji wa sheria vilivyotokea wakati wa kesi ya Ditopile-
Mzuzuri juzi.

Tibaigana alisema amekwisha kuliagiza jeshi lake kufungua jalada kwa ajili ya uchunguzi utakaoliwezesha kuchukua hatua za nidhamu dhidi ya wote waliohusika, ikibainika walitenda makosa.

Kamanda huyo pia aliwaonya ndugu wa mtuhumiwa Ditopile Mzuzuri kwa kitendo chao cha kufanya vurugu katika eneo la Mahakama na kuwatahadharisha kuwa kitendo hicho kikitokea tena asilaumiwe yeye binafsi kwa hatua atakazochukua dhidi yao.

“Nawapa pole wote mliopatwa na adha hii lakini pia napenda kuwaonya ndugu wa mtuhumiwa kwa vitendo vyao vya ubabe waliovionyesha. “Watambue kuwa kesi ni kesi, sasa hivi Ditopile-Mzuzuri atakuwa anakuja mahakamani mwenyewe bila usimamizi wa polisi kwa sababu ya dhamana. Wakifanya tena vurugu, wasimlaumu Tibaigana kwa hatua atakayowachukuliwa,” alisema.

Alisema kujaa mahakamani hapo na kusababisha vurugu hizo inaonyesha dhahiri ndugu hao wa Ditopile- Mzuzuri walijua ndugu yao angetolewa kwa dhamana, jambo ambalo lilimshangaza Tibaigana.

Alisema kwa mujibu wa taarifa alizopewa na askari hao, uamuzi wa kumpitisha Ditopile-Mzuzuri katika mlango huo wa nyuma wa jengo la Mahakama Kuu, ulitokana na taarifa walizopata askari hao walipokuwa gerezani kuwa mahakamani hapo kumejaa watu.

“Kesi hii tangu mwanzo imekuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi hali ambayo tangu mwanzo imekuwa ikiwapa shida askari kudhibiti hali ya usalama wakiwamo ndugu zake mtuhumiwa,” alisema Tibaigana.

Aliwataka wajirudi akisema si vema polisi kuonyeshana ubabe na familia hiyo na pia hadhani kama ni sawa jeshi hilo kutumia askari wengi kushughulikia ulinzi wa mtu mmoja. Ditopile-Mzuzuri anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia dereva wa daladala Hassan Mbonde, Novemba 4, mwaka jana .

Naye Ikunda Erick anaripoti kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Christopher Mtikila amesema vurugu na kuwapiga waandishi zilizofanywa juzi eneo la Mahakama Kuu zilifanywa na polisi waliovaa kiraia.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mtikila alisema polisi waliovaa sare na wengine waliovaa kiraia ndiyo walihusika kufanya vurugu kwa kile kilichoelezwa ni kuwapa hofu wananchi wasihoji masuala ya kesi hiyo.
 
Let me guess!

Mwanakijiji:- Mheshimiwa ndugu Tibaigana, ilikuwaje hasa hadi kufikia mshitakiwa kupitishwa mlango wa jaji jambo ambalo ni kinyume cha taratibu na sheria za mahakama?

Tibaigana:- Aiseee Unajua tulipofika pale kortini kusema kweli umati ulikuwa mkubwa sana. hatukutegemea kabisa kwa hiyo, ili kumlinda mshtakiwa tuliona haja kubwa ya kufanya hivyo. Uamuzi wa haraka sana Ulitakiwa!

Mwanakijiji:- Je, katika kufanya hivyo mlifanya mawasiliano na ofisi ya mahakama kupata ruksa ya kutumia mlango huo?

Tibaigana:- Kijana ebu kwanza ondoa hilo swali, maana sasa wewe unataka kujaribu watu akili hapa. Nimesema ilikuwa ni uamuzi wa haraka, Unazijua wewe taratibu za mahakama? waulize hao waandishi wa habari kwa nini walivamia gari la mshtakiwa wakati akiletwa mahakamani?

Mwanakijiji:- Samahani mzee wangu lakini pamoja na hivyo kwani hii ilikuwa mara ya kwanza mshitakiwa kupelekwa mahakani?

Tibaigana:- Kijana itabidi tuanze upya haya mahojiano. Futa yote yalitotangulia na tafadhali sana kijana usije kuropoka ovyo. Hili ni swala zito sana kuliko umri wako. Unasikia?

Mwanakijiji:- ndio mzee nimekusikia na nimekwisha futa tuanze upya maswali.

Tibaigana:- Heee! heee! kijana ebu nipe kwanza hayo maswali kabla hujaanza kurekodi!

Too much relating,
Tbaigun amerithi ubabe wa bosi wake wa zamani ambaye sasahivi ni memba wa bodi flani ya APANAT(reverse).
 
Mkandara!
Nimesoma leo ameomba msamaha kwa jamaa wa Mahakama ,waandishi na kutoa onyo kwa Ndugu wa Ditto,sasa tusubiri tuone hizo hatua ambazo amesema atazichukua meanwhile tusubiri vile vile mahojiano ya MKJJ.
 
Mie Nawahurumia wale walokuwa mstari wa mbele ktk kutaka haki itendeke, i can't imagine what would be next.
 
Ni MJUMBE wa bodi ya Tanapa lakini atakacha siku za karibuni coz si mwajiriwa wa sirikali tena, Ukiwa mjumbe wa ile bodi lazima uwe mwajiriwa sirikalini sasa yeye alisha uacha uIGP.
 
2007-03-08T19_15_14-08_00.jpg



A killer is hiding his face.
(Picha na Mroki Mroki)​
 
kama uliotea mzee haki haijatendeka kabisa naisistoshe ndugu wa mshitakiwa wamewapiga waandishi wa habari tena ndani ya mahakama kuuuu ya tanzania hiviiii hiii ni nchi au kwa kweli tuna takiwa kuamka dito alistaili kunyongwa kama ni hiv waachiwe na wengine kama wa kina babu seya
 
Hivi huyu tido ni nani kama ni hicho cheo cheo ni dhamana na wala si kama sereksli ilivyofanya jamanii hivi kuna serikali kweli au ni serekali ya kulindana viongozi kwa viongozi kwa hiyo inamaana sheria tumetungiwa sisi tusio na hela wala vyeo serikalini? Sheria ni za wanyonge sio" Kosa alilofanya dito anastahili hukumu inayotambulika kisheria.
Haya sheria imepindwa katolewa ha chakuwapiga waandi nacho si chakukusudia? halafu ilikuionyesha serikali kwamba wao ni wababe ndani ya mnahakama imbayo inaitwa ni nitukufu hapa kweli mahakama ina utukufu wowote?
 
Hatimaye Mahakama ya hakimu mkuu mkazi Kisutu
imemwachia huru aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe.
Ukiwaona Ramadhani Ditopile wa Mzuzuri aliyekuwa
akikabiliwa na kesi ya mauaji bila kukusudia. Hukumu
hiyo iliyosomwa mbele ya umati mkubwa wa watu
waliofurika mahakamani hapo Leo Mchana, ilisomwa na
hakimu Omary Kipyakinyemi na ilisomeka kama ifuatavyo:
-
SHAURI LA MAUAJI NA. 1132/2006
JAMHURI DHIDI YA DITOPILE RAMADHAN MWINYISHEHE
MZUZURI
TAREHE 08 MACHI, 2007
Mahakama kwa kuzingatia sheria za Jamhuri ya
muungano wa Tanzania na ushahidi uliotolewa mbele ya
mahakama, imeonelea kuwa, ili iwe fundisho kwa
Madereva wote wa daladala na makonda wao ni vema
wakajifunza kutokana na mauaji haya na kwamba si vyema
wakawa wabishi na wepesi kuendesha magari yao hovyo
bila kuzingatia sheria za barabarani vitu ambavyo
hupelekea kuwaudhi na kuwakasirisha watumiaji wengine
wa barabara na kuhatarisha maisha yao. Hivyo basi ni
vyema wakafahamu kuwa baadhi ya watumia barabara
humiliki silaha za moto ambazo huwatia nguvu na viburi
kuzitumia na hatimaye kuwasababisha makonda na
madereva kuwa hatarini kupoteza maisha yao kama
ilivyotokea katika kesi hii ya Ditopile.
Kwa maelezo haya, namwachia huru Ditopile kwa kuua
bila kukusudia na kuwa aliudhiwa na tabia chafu
zilizojengeka za marehemu dereva aliyetangulia mbele
ya haki na mungu amrehemu.
Jalada limefungwa na kama kuna malalamiko ama
rufaa kwa kesi hii, upande wa mashitaka unapewa siku
30 kukata rufaa mahakama kuu.
IMETOLEWA KWA AMRI YANGU
OMAR KIPYAKINYEMI
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.
Kooortiiiiiii!!!!!!
 
jamani mie naona hakuna cha muhimu kuongelea hii issue maana huyu ni free man at last, kwanza tunaambiwa alikuwa analala jela lakini je mna uhakika alikuwa analala jela ? kama kweli, angekuwa anachukuliwa na usafiri bomba kama ule kwenda na kurudi mahakamani, after all nani aliyeshuhudia dito akitokea jela asubuhi kwenda mahakamani ? huyu mzee HAKUWA jela sasa kwa taarifa yenu kama mlikuwa hamjui. ila alikuwa kidogo mbali na familia yake katika kipindi hiki cha kesi yake ! all in all, hes free, ndio maana mwanakijiji kashasema kabisa kama ni hivyo basi bora ditto aachiwe ni kweli, lakini sasa tayari keshaachiwa na hakuna kitakachofuata zaidi ya "policies" zao ili waonekane kama kweli yupo jela lakini ni changa la macho ! inasemekana ataonana na JK sasa sijui ni kama ikulu, kwa ditto au wapi lakini wataonana !!
 
Uendeshaji mzima wa kesi ya brother Ditto ni clear reflection of cruel governance which the tz government is embracing!!

Definitily, difference doesn't prevail between our law enforcing agencies and a 'dictatorial regime! WHY ON EARTH DOEN'T THE PRESIDENT INTERVENE??

Wanahabari wanapigwa mahakamani and no arrest have been made so far!!

Niaminivyo mimi, mahakama ina hadhi na heshima ya aina yake, naweza kuifananisha na kanisani au msikitini. Sehemu wapitapo mapadri au mashehe hapiti mtu asiyekuwa na hadhi hiyo. Iweje askari wampitishe muuaji through the door specially used by judges?
 
ditto KAZOEA MILANGO YA NYUMAAAAA!!


JUZI PALE SAMORA ST ILIKUWA KIMBEMBE PALE KAKA DITTO ALIPOSHUKA KWENYE GARI LISILOJULIKANA NA KUINGIA KWENYE DUKA LA SIMU SHIVA -ZE FONO...ili angalau ajinunulie simu ,si mnajua kwa madai yake siku ya tukio alisema aliibiwa simu.,wallet ,na tumilioni tumoja tuwili...sasa baada ya kuingia dukani watoto wakiuni wakiwemo mateja ,waosha magari ,mashanta ets ambao pale ni jobless corner yao wakaaza kupiga makelele na kulizonga duka kwa masaa kama mawili wakiimba ditooo! ditooo! ....masikini hawakujua kuwa commando DITTO alishatokomea kupitia MLANGO WA NYUMA[UWANI] wa duka na KUTOKOMEA....

next time aliingilia MBELE mkamsubiri NYUMA!!!!!!!!!!!!!
 
PM!
Pamoja na kuwa nje kwa dhamana Lakini Nafikiri atakuwa na wakati mgumu sana katika maisha yake na wanajamii waliomzunguka kila pembe ya mji.
 
Ndugu KNKCU ni kweli kwamba huyu Bwana atakuwa na wakati mgumu si na wanaomzunguka tu,bali hata Mkewe!,kwani kuna habari kuwa yule Mwanamke aliyekuwa na Dito siku ya Tukio si ndugu yake bali alikuwa ni kimada.Habari zisizothibitishwa zinasema Mke wa Dito anataka kumjua M'ke huyo!.Kumetumiwa kila njia M'ke huyo hajaitwa kama Shahidi huko Mahakamani kwa sababu kungezua hadithi nyingine!,sasa bado ni kitendawili "alikuwa nani huyo?"Usije kushangaa kuwa alikuwa mke wa Kigogo mwenzie.Kwani Dar kipindi hicho ilikuwa kimya waungwana wote walikuwa Dodoma (Bungeni).Mwenye kujua siri hii ni Bwana dereva wa Dito pekee.Naomba msinivamie naandika nilichokisikia.Naomba kutoa Hoja!
 
kweli kabisa ,ditto anaweza kuwekwa huru na mamlaka ,lakini siku zote wanajamii watamuona muuwaji.....na anavyopenda UMENDE NA KUNYEMELEA vichochoroni ,siku si nyimgi mtasikia ameingia kwenye anga za watu na wakamfanyiza...labda muungwana amshauri atulie ndani kwa usalama wake....anaweza kuwanunua ndugu za mbonde ...lakini hawezi kuwanunua MATEJA WAPIGADEBE,na wengine waliochukizwa ,so kwa usalama wake ashauriwe abakie ndani la sivyo usishangae watu wakampiga mawe kama kibaka uswahilini.....
anayo bahati pia kwa sababu kuna watu wameua BILA KUKUSUDIA KIUKWELI na wana miaka kumi hawajasikilizwa......
ingepasa wale ndugu zake ditto waliodharau mahakama wote wafunguliwe mashtaka pamoja na wale polisi na maofisa usalama kama kweli tunataka kurudisha heshima ya mahakama....
 
Wenye kuishi karibu na Ditopile tufahamisheni maisha yalivyo hapo kwake baada ya kuachiwa kwa dhamana.Amepewa ulinzi au laah?Anaishi hapo kwake aua amehama na hajulikani alipo?
 
Leo majira ya saa tano asubuhi, wafungwa waliokuwa wameletwa kuendelea na kesi zao kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam walikataa katakata kushuka kwenye karandinga.

Karandinga zilikuwa mbili zikiwa na mahabusu wa Keko, Ukonga na Segerea, walipofikishwa mahakamani pale wakaamriwa kama kawaida washuke kwenye karandika ili waswekwe kwenye sero ya pale! Walikataa kwa kupiga kelele na kuimba kwamba hawashuki kwa sababu mahakama za Tanzania haziwatendei haki mahabusu na wafungwa. Aidha wamelalamika kesi zao kuchukua muda mrefu wakiwa wanaachwa rumamnde bila kupata dhamana.

Maaskari baada ya kuona jambo hilo limeanza kuleta mvuto wa ajabu kwa raia ambao walikuwa pale mahakamani kwa kuwasupport ilibidi defender isafishe njia na makarandinga hayo yakatokomea kurudi Keko, Ukonga na Segerea. Waliondoka wanimba wimbo wa "Parapanda ....... !

Kazi kweli kweli, nguvu ya mnyonge labda itaweza kuwaamsha walio katika usingizi wa fofofo!!

Binafsi naona wamefanya kitendo ambacho ni positive, na hata kama haki haitapatikana mapema ila ujumbe wao umefika.

Wasiwasi wangu ni je, wakija tena mahakamani hakimu anaweza kuwahukumu kwa kutoiheshimu mahakama? Ngoja tuone....
 
Back
Top Bottom