Mkuu wa nchi ambae ndio ndio custodian wa mali za taifa la watanzania kudai kuwa hawezi kufokea mtumishi wa umma ni kushangaza umma wa watanzania.
Kwamba watumishi wa umma wakiharibu atawabembeleza?
Nimekaa na wazee wengi waliofanya kazi na hayati Julius Nyerere wanasema wazi kuwa Mwalimu alikuwa mkali sana.
Ilitokea akikuita kwake Msasani au Ikulu ilikuwa lazima upate wasiwasi na woga mkuu.
Wengine aliwaita kuwapongeza lakini hawakuamini walichoitiwa wapo pia aliowafokea hadaharani au hata kifichoni.
Kwamba mkuu wa nchi unafanya kazi kwa kuonea aibu wateule wako? Kwamba utakuwa unawabembeleza?
Mbona hii sio sawa? Mkuu wa kaya lazima uwe mkali ili nidhamu ipatikane kuanzia juu mpaka chini.
Hatusemi ufokee watu kama watoto wako. Bali uwe na maamuzi na maelekezo yenye kuonyesha kuwa kuna kiongozi mwenye mamlaka aisiyetaka mzaha na anataka watu wafanye kazi.
Mfano, tulitegemea umkaripie January Makamba maana mradi wa JNHP unaweweseka kama vile hauna manufaa kwa wanaCcM wenzake.
Kiongozi Ukiwa mwadilifu,mpen da haki,muwazi, unauependa matokeo mazuri.na makubwa, ...honest,Integrity,principled(Kingereza kwa msisitizo) ...watu watakuogopa by Default...!
JPM hakuwa na hayo ,kama alikuwa nayo kidogo sana ....yeye aliogopwa Kwa kuwa alikuwa mkali ,anatisha,haaminiki,hatabiriki,roho Mbaya,fyatu.....Ili uelewe ZAIDI ilikuwa mi sawa na Mtu Mwenye Sura Mbaya ambaye watoto hutishiwa wasifanye Kitu Fulani!
Nyerere alikuwa anaogopwa kutokana na uadilifu wake,matendo yake mazuri Kwa umma yalimfanya atishe....tena waliokuwa wanamwogopa ZAIDI,ni wazembe,wasio waadilifu ...wasiojiamini...vilaza!
Unafikiri Mtei,Sokoine au Kambona Walikuwa wanamwogopa...Tafuta picha za Nyerere na Sokoime uone body language ya Mwalimu AKIWA na Sokoine 😁
Bahati Mbaya hivi vitu havilazimishwi vinakuja tu na Karama kutoka Kwa Mungu!
Ukilazimisha itafikia kuanzaa kutesa,kukandamiza watu ,pengine hata kuua!
Kwa Chief Hangaya...wote mnamjua ...no comment?🤭🤭😁😁
Mwisho,hata sisi wananchi tupo tulio na Karama hizo...basi tu hatujapewa jukwaa ,Ndio maana Tunadai Katiba Mpya Ili I- Gorvene ' Uendeshaji wa Nchi ..kuwathibiti Makarmastili kama Nyerere na wale wanaotaka kuwa Makarasmatiki kimichongo!
Na wasio eleweka pia !
Mungu Ibariki TANZANIA!