Mkuu wa nchi lazima awe mkali na aogopwe. Asipoogopwa kila kitu kitakwenda mrama. Hata hayati Julius Nyerere aliogopwa na alikuwa mkali

Mkuu wa nchi lazima awe mkali na aogopwe. Asipoogopwa kila kitu kitakwenda mrama. Hata hayati Julius Nyerere aliogopwa na alikuwa mkali

Hata Mimi nilishangaa,Rais wetu aliposema hatafokea MTU yeyote.

Toka enzi za utawala wa kifalme na usultan,Mtawala Ni Lazima aogopwe,vinginevyo,Kazi zitafanyika kwa kulipua,na wizi wa Mali ya Uma utakuwa mkubwa Sana.

Ukichukulia pia Rais wetu Ni wa Jinsia ya Kike,Asicheke na wezi wa Mali ya umma.

Ikithibitika umeiba Mali ya Uma,Wezi hao wafilisiwe na kufidia mpaka centi ya mwisho iliyoibiwa,pesa irudishwe kwenye mfuko wa Serikali kuu.

HAKUNA KUCHEKA NA WEZI WA MALI YA UMA,NA WANAOCHEZEA NIDHAMU YA KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMA.
 
Mkuu wa nchi amabae ndio ndio custodian wa mali za taifa la watanzania kudai kuwa hawezi kufokea mtumishi wa umma ni kushangaza umma wa watanzania. Kwamba watumishi wa umma wakiharibu atawabembeleza?

Nimekaa na wazee wengi waliofanya kazi na hayati Julius Nyerere wanasema wazi kuwa Mwalimu alikuwa mkali sana. Ilitokea akikuita kwake Msasani au Ikulu ilikuwa lazima upate wasiwasi na woga mkuu. Wengine aliwaita kuwapongeza lakini hawakuamini walichoitiwa wapo pia aliowafokea hadaharani au hata kifichoni.

Kwamba mkuu wa nchi unafanya kazi kwa kuonea aibu wateule wako? Kwamba utakuwa unawabembeleza?

Mbona hii sio sawa? Mkuu wa kaya lazima uwe mkali ili nidhamu ipatikane kuanzia juu mpaka chini.

Hatusemi ufokee watu kama watoto wako. Bali uwe na maamuzi na maelekezo yenye kuonyesha kuwa kuna kiongozi mwenye mamlaka aisiyetaka mzaha na anataka watu wafanye kazi.

Mfano, tulitegemea umkaripie January Makamba maana mradi wa JNHP unaweweseka kama vile hauna manufaa kwa wanaCcM wenzake.
Huyu Mama bwana anatulostisha sana, akiachana na Kikwete pamoja na wale mawaziri useless waliotemwa na Jiwe angetupeleka mbali sana.
 
Mkuu wa nchi amabae ndio ndio custodian wa mali za taifa la watanzania kudai kuwa hawezi kufokea mtumishi wa umma ni kushangaza umma wa watanzania. Kwamba watumishi wa umma wakiharibu atawabembeleza?

Nimekaa na wazee wengi waliofanya kazi na hayati Julius Nyerere wanasema wazi kuwa Mwalimu alikuwa mkali sana. Ilitokea akikuita kwake Msasani au Ikulu ilikuwa lazima upate wasiwasi na woga mkuu. Wengine aliwaita kuwapongeza lakini hawakuamini walichoitiwa wapo pia aliowafokea hadaharani au hata kifichoni.

Kwamba mkuu wa nchi unafanya kazi kwa kuonea aibu wateule wako? Kwamba utakuwa unawabembeleza?

Mbona hii sio sawa? Mkuu wa kaya lazima uwe mkali ili nidhamu ipatikane kuanzia juu mpaka chini.

Hatusemi ufokee watu kama watoto wako. Bali uwe na maamuzi na maelekezo yenye kuonyesha kuwa kuna kiongozi mwenye mamlaka aisiyetaka mzaha na anataka watu wafanye kazi.

Mfano, tulitegemea umkaripie January Makamba maana mradi wa JNHP unaweweseka kama vile hauna manufaa kwa wanaCcM wenzake.

Kwanini kwenye kila kitu aigwe Nyerere?

Watu milioni 60 tunatawaliwa na kuongozwa kwa fikra za mtu mmoja tuu, kwani sisi North Korea?

Nyerere kweli aliwaloga Watanzania na ndiyo maana tunakwama kwenye mambo mengi sana.
 
Hawatakaa waguse tena. Imeisha hiyo
Achana na hawa watu wamezoea kuchunga ng'ombe, wanafikiri na binadamu anachapwa tu mijeledi kama ngombe,

Ndo maana nyumba nyeupe hawatakaa wapate bahati tena ya kuingia!
 
Msameheni tu huyu ndugu zanguni.
Hajui na wala hajawajua WAHUNI wapoje. WAHUNI wameshamteka tayari. Nchi imerudi kwa WAHUNI.
Tukumbuke:-
*Angekuwepo JPM, umeme usingekuwa unakatika katika kama ilivyo sasa.
*Angekuwepo JPM, mbolea na bidhaa zingine zisingekuwa zimepanda bei kwa kiasi hiki cha 120%.
*Angekuwepo JPM, Ajali nyingi zinazotokea zisingekuwepo.
Kilichomsaidia JPM kudhibiti upumbavu huu ni ukali wake.
Maana ilikuwa akiongea tu, hadi sisimizi wanasikia sauti yake.

Nashangaa kuona kiongozi anasema tena hadharani eti hataweza kumkaripia mtu aliyekosea. Tafsiri yake ni kwamba, Dereva ameachia usukani, kwa hiyo kila abiria apambane na hali yake ili kujinusuru.
hayo yoote yalikuwepo wakati wa huyo unayemtaja
 
Macho yenyewe yameshalegea sijui kama yanaona ofisi zote ni hovyoooo tunadaiwa rushwa wazi wazi wala hawajali huduma mbovu mwacheni Magu aitwe Magu alikuwa kiboko na hatutapata tena rais kama Magu mkimtaka mtu wa aina ya Magu nichagueni mimi na ntashika adabu
 
Mkuu wa nchi amabae ndio ndio custodian wa mali za taifa la watanzania kudai kuwa hawezi kufokea mtumishi wa umma ni kushangaza umma wa watanzania.

Kwamba watumishi wa umma wakiharibu atawabembeleza?

Nimekaa na wazee wengi waliofanya kazi na hayati Julius Nyerere wanasema wazi kuwa Mwalimu alikuwa mkali sana.

Ilitokea akikuita kwake Msasani au Ikulu ilikuwa lazima upate wasiwasi na woga mkuu.

Wengine aliwaita kuwapongeza lakini hawakuamini walichoitiwa wapo pia aliowafokea hadaharani au hata kifichoni.

Kwamba mkuu wa nchi unafanya kazi kwa kuonea aibu wateule wako? Kwamba utakuwa unawabembeleza?

Mbona hii sio sawa? Mkuu wa kaya lazima uwe mkali ili nidhamu ipatikane kuanzia juu mpaka chini.

Hatusemi ufokee watu kama watoto wako. Bali uwe na maamuzi na maelekezo yenye kuonyesha kuwa kuna kiongozi mwenye mamlaka aisiyetaka mzaha na anataka watu wafanye kazi.

Mfano, tulitegemea umkaripie January Makamba maana mradi wa JNHP unaweweseka kama vile hauna manufaa kwa wanaCcM wenzake.
Kutokana na yaliyotokea 2019 na 2020 hakuna asiye na guilty conscience. Watu wanaoficha ukweli hawawezi kuwa huru mioyoni mwao na mbele za Mungu. Mengine yote ni matokeo!
 
Mkuu kwenye hii hospital ninayofanyia kazi siku hizi tunaingia ofisi 07:30 then tunakuwa na vikao vya Morning Report mpaka 09:00 hadi 09:30.

Hapo mtaenda kuhudumia wagonjwa hadi kwenye 10:30 halafu watu wanaenda canteen kunywa chai. Chai inanyweka huku stori zinapigwa hata mpaka 12:00 hivi au zaidi.

Mkirudi mnafanya kazi saa moja au moja na nusu mnarudi canteen kupata lunch ndio mpaka saa 15:30 watu wanarudi ku-sign out. Siku imeisha.

Hiyo ndio nidhamu ya moyoni ya hawa Watanzania hapa nilipo. Enzi za Magufuli tulinyooshwa na kazi zilifanyika kwa weledi knowing ukizingua imekula kwako.

RIP Magufuli.
Huu ndio ujinga wetu watanzania, nyinyi ni wauwaji Kama wauwaji wengine tu,Yani unashindwa kuwatibia ndugu zako kisa raisi hakutishii kukufukuza kazi?huu ni ujinga uliopitiliza
 
Kwanini kwenye kila kitu aigwe Nyerere?

Watu milioni 60 tunatawaliwa na kuongozwa kwa fikra za mtu mmoja tuu, kwani sisi North Korea?

Nyerere kweli aliwaloga Watanzania na ndiyo maana tunakwama kwenye mambo mengi sana.
Nimetolea mfano tu, sijasema aigwe. Lakini kwa taifa lolote mkuu wa nchi lazima awe mkali na kuogopwa ili asimamie taifa lake vizuri
 
Marekani na Ulaya, ambapo tunawaiga kwa demokrasia, hawabembelezani.

Trump alikuwa anafukuza watu karibu kila siku.

Hakuna kitu kinachoitwa nidhamu ya moyoni!
Yaani unadiriki kutoa mfano wa Trump...pua,puaa,puaaaaaa
 
kwani sasa hivi hamuwi kwenye matatizo? siku yakikukuta utashukiwa individually.

Hata kipindi cha Magu walikuwepo nunda kama wewe, ndio maana leo tunawaona Makonda na Sabaya wakitiwa akili.

Wangekuwa wameisha watu wa hovyo basi jiwe asingekuwa anafukuza/simamisha watu kila leo.

Concern ya Rais ni smart sana,tusimamie taratibu kama wasomi na sio nguruwe mpaka aswagwe.

Tujenge taasisi imara za kusimamiana,rais atapita lakini taasisi smart zitabaki. Mf mzuri Hayati amesepa halafu mnabaki na nini?hayati angekuwa smart angeimarisha taasisi na sio kukaza kichwa tu kama vile utakuwepo milele
Tatizo unadandia mada ambazo huna hata uwezo wa kuzielewa.

Ni kama familia ambayo baba hana sauti na watoto hawamuogopi . Unategemea nini? Kwa nini usikae kimya ili tusikuome mpumbavu.
 
Nadhani mama amesahau kwamba wabongo ni watu wanaotaka kulazimishwa kufanya kazi.

Enzi zile bwana Lyatonga ilibidi awe anatoa viti vilivyokutwa wazi maofisini, wenyenavyo wako kitaa tu kula bata wakati wa kazi.

Wakati wa Kikwete nidhamu ya kazi ilishuka kupita kiasi kwa sababu rais hakuwa serious with anything, zaidi ya kuchekeana na kukwaa pipa kwenda kula bata majuu.

Wakati wa JPM nidhamu ya kazi ilirudi, japo ilikuwa ya woga, lakini watu walianza kufanya kazi na ufanisi wa utendaji ukaongezeka, na sisi makapuku tukawa tunahudumiwa humo maofisini.

Sasa Samia anahubiri nidhmu ya moyoni, mi naona tunarudi kwenye enzi za awamu ya 4!
Na this time itakuwa worse kuliko hata awamu ya nne.
 
Mkuu wa nchi ambae ndio ndio custodian wa mali za taifa la watanzania kudai kuwa hawezi kufokea mtumishi wa umma ni kushangaza umma wa watanzania.

Kwamba watumishi wa umma wakiharibu atawabembeleza?

Nimekaa na wazee wengi waliofanya kazi na hayati Julius Nyerere wanasema wazi kuwa Mwalimu alikuwa mkali sana.

Ilitokea akikuita kwake Msasani au Ikulu ilikuwa lazima upate wasiwasi na woga mkuu.

Wengine aliwaita kuwapongeza lakini hawakuamini walichoitiwa wapo pia aliowafokea hadaharani au hata kifichoni.

Kwamba mkuu wa nchi unafanya kazi kwa kuonea aibu wateule wako? Kwamba utakuwa unawabembeleza?

Mbona hii sio sawa? Mkuu wa kaya lazima uwe mkali ili nidhamu ipatikane kuanzia juu mpaka chini.

Hatusemi ufokee watu kama watoto wako. Bali uwe na maamuzi na maelekezo yenye kuonyesha kuwa kuna kiongozi mwenye mamlaka aisiyetaka mzaha na anataka watu wafanye kazi.

Mfano, tulitegemea umkaripie January Makamba maana mradi wa JNHP unaweweseka kama vile hauna manufaa kwa wanaCcM wenzake.
Kiongozi Ukiwa mwadilifu,mpen da haki,muwazi, unauependa matokeo mazuri.na makubwa, ...honest,Integrity,principled(Kingereza kwa msisitizo) ...watu watakuogopa by Default...!
JPM hakuwa na hayo ,kama alikuwa nayo kidogo sana ....yeye aliogopwa Kwa kuwa alikuwa mkali ,anatisha,haaminiki,hatabiriki,roho Mbaya,fyatu.....Ili uelewe ZAIDI ilikuwa mi sawa na Mtu Mwenye Sura Mbaya ambaye watoto hutishiwa wasifanye Kitu Fulani!
Nyerere alikuwa anaogopwa kutokana na uadilifu wake,matendo yake mazuri Kwa umma yalimfanya atishe....tena waliokuwa wanamwogopa ZAIDI,ni wazembe,wasio waadilifu ...wasiojiamini...vilaza!
Unafikiri Mtei,Sokoine au Kambona Walikuwa wanamwogopa...Tafuta picha za Nyerere na Sokoime uone body language ya Mwalimu AKIWA na Sokoine 😁
Bahati Mbaya hivi vitu havilazimishwi vinakuja tu na Karama kutoka Kwa Mungu!
Ukilazimisha itafikia kuanzaa kutesa,kukandamiza watu ,pengine hata kuua!
Kwa Chief Hangaya...wote mnamjua ...no comment?🤭🤭😁😁
Mwisho,hata sisi wananchi tupo tulio na Karama hizo...basi tu hatujapewa jukwaa ,Ndio maana Tunadai Katiba Mpya Ili I- Gorvene ' Uendeshaji wa Nchi ..kuwathibiti Makarmastili kama Nyerere na wale wanaotaka kuwa Makarasmatiki kimichongo!
Na wasio eleweka pia !
Mungu Ibariki TANZANIA!
 
Back
Top Bottom