Mkuu wa Wilaya Arusha na mbwembwe za misafara

Anapoenda kukagua miradi wakuu wa idara wanaenda na nini kama sio usafiri wa magari, acheni majungu.
 
Queen Sendinga RC wa Iringa nae jana nimeona 'convoy' yake ikiongozwa na FOTON ya Polisi na pia GX nyingine sijui ya nani. Kwa hiyo 'convoy' yake ni gari 3, ya kwanza PT yenye king'ora na mataa, inafuata yake RC na ya tatu GX yenye namba STL. Hapo trafiki anasimamisha magari yampishe RC anaenda home kwake.

Nchi hii ina matukio sana
 

Tulio pata bahati ya kuona awamu ya kwanza huu ujinga haukuwepo kabisa.
 
Nimemwandikia mam warak kwenye mkeka wake niwemo, hususan anipangie Kaskazini

Nikifika TUTAELEWANA tu.
Ila anipe na mtu anayejua hata kusoma maana mi darasa la Saba B
 
Juzi wakati nipo Samunge gari iliyokuwa inaongoza msafara wake kidogo inigonge yaani
 
Juzi wakati nipo Samunge gari iliyokuwa inaongoza msafara wake kidogo inigonge yaani

Anaongozwa na ulimbukeni wa madaraka.Barabara zenyewe za Arusha zimeshavamiwa na machinga halafu anatokea mshamba anakimbiza magari bila sababu za msingi ukiuliza anachokimbilia nini hana majibu.
 
Naam, wewe utakua ni mkazi wa Arusha. Huyu kijana amesaidia wananchi wengi Sana,, bila kujali itikadi zao. Binafsi niliwahi kufika Mara kadhaa ofisini kwake, akifika anawasalimia wananchi kwa nidham huezi amini ni Mkuu wa wilaya. Kuna wanasheria zaidi ya kumi pale ofisini kwake wa kujitolea kwa ajili ya kuwasaidia wananchi yeye ndo naskia anawafadhili. Amekua anafanya semina za ujasiriamali kuwafundisha Wanawake na vijana ujasiriamali.
Nachokiona mh. Mbunge hataki Wala hapendi kuona yule KIJANA anakubalika na kufanya KAZI. Majuzi bila aibu Eti akaitisha kikao Cha bajaji akapanga watu wakumchafua huyu DC. Gambo usipojirekebisha na kufanya hizi siasa zako chafu hatutakuchagua Tena hakika nakuambia.
 
Hii ni KAZI ya Gambo, sio MTU mwingine
 
Wakati mwingine uwe unauliza sisi wa zamani tunajua ni kamati ya ulinzi na usalama yenye DC ,ocd dso mkuu wa kikosi jwtz uhamiaji magereza takukuru fire na das wanakagua miradi itakayozinduliwa na mwenge wa uhuru.muache kuandika mambo msiyoyajua.
Halafu wanatuona sisi wananchi ni hamnazo. Huyu DC wengi wanaomba abaki, isipokua Gambo. Sasa sijui atafanya KAZI na nani
 
Gambo alikua mwonevu, na sasa hapendi viongozi wenzake. Amejisahau kwamba yeye saivi sio mkuu wa mkoa Bali ni mbunge. KILA Rc, DC Ras na Def yeye hua lazma awakatae. Majungu anavyofanywa saizi ni sababu huyo DC anapita hiki KWENYE kata kutatua kero za wananchi. Sasa Gambo yeye hataki, anataka yeye ndo aonekane KILA kitu anafanya.
Sasa Gambo huyu Rc wa sasa ni mpya kwanini umeanza figisu za chini chini, Rc huyu amekufanyaje,, KUMBUKA huyu alikuja Arusha KABLA yako
 
Duuu mwogope Mungu. Wananchi yupo na tunaona. Halafu mama hafanyi KAZI kupitia mitandao ama kwa kuskiza cheap gossips. Uraisi ni TAASIS, taarifa za jinsi huyo DC anafanyaje majukumu yake zipo kwa usahihi
 
Sabaya alipokuwa anakuja kufanya fujo hapo yeye alikuwa wapi?
 
Tatizo sio Ma DC vijana kiongozi,, tatizo ni Ma DC wanaotokea UVCCM.
Nimetazama hii video kidogo tu nikashindwa kuendelea...jamani tuelezane ukweli, hii tabia ya kishenzi ya kuwadhalilisha wananchi imetoka wapi?

Najua hawa vijana wanaoteuliwa wanatokea huko huko UVCCM, je ni huko ndiko wanalelewa na kuwa kama wanyama wa porini kwa jinsi walivyokosa malezi bora, duh!

Halafu kwa ujeuri hajali anachukuliwa kwenye video! Ni kama vile anajua hiyo video itamuongezea CV akaweza kupanda zaidi labda na kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa!

Your browser is not able to display this video.


Asante Mungu kwa kutuepusha japo kwa muda na hili wimbi la ukatili na mateso lililotuandama kwa miaka mitano!

Unamkuta polisi na nyota zake eti anatii maagizo ya vijana wakora kama hawa na kuwaumiza wananchi hadi ndugu zake wa kuzaliwa!

Unamkuta hakimu kwa maagizo kutoka juu na bila kujali miiko yake ya kazi anatoa hukumu kwa kesi si za hovyo tu bali na za kubambikiza!

Na hivyo hivyo katika taasisi zote za serikali ambako ungetegemea kupata ulinzi, haki na usalama kama mwananchi...hakika tulifikia pabaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…