Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Queen Sendinga RC wa Iringa nae jana nimeona 'convoy' yake ikiongozwa na FOTON ya Polisi na pia GX nyingine sijui ya nani. Kwa hiyo 'convoy' yake ni gari 3, ya kwanza PT yenye king'ora na mataa, inafuata yake RC na ya tatu GX yenye namba STL. Hapo trafiki anasimamisha magari yampishe RC anaenda home kwake.
Nchi hii ina matukio sana
😂😂😂😂 Jamaa ni rapper mkali sana asee!.Nasikia ni rapa
Juzi wakati nipo Samunge gari iliyokuwa inaongoza msafara wake kidogo inigonge yaaniHeshima sana wanajamvi,
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini ni kijana mdogo lakini mwenye mbwembwe nyingi na vituko vya ujana uliopitiliza.Katika siku za karibu amekuwa na tabia ya kusindikizwa na gari la polisi ikiambatana na ving'ora vingi pengine ungefikiri kuna mgonjwa wa Covid 19 anakimbizwa Hospital kuwahi huduma za kitabibu.
Mwezi uliopita kama kumbukumbu zangu zipo sana alizindua mradi mdogo {mradi uchwara} wa kufyatua matofali wa halmashauri ya Jiji la Arusha.Huo msafari ungefikiri anakwenda kuzindia kinu cha Nyuklia gari zilikuwa zinakimbizwa,ving'ora na taa za magari yote zikiwashwa full light.Tutakae tukubali Vijana wakipewa madaraka kidogo wanaharibu sana,wanaumiza wananchi sana,wanatumia madaraka vibaya sana bahati mbaya Mkuu wa Wilaya ya Arusha yumo katika kundi hilo.
Mwaka jana alishiriki zoezi la kuwachapa viboko wafanyabiashara kwa madai ya kununua thamani za shule.DC kawa mpelelezi,akajivika ujaji na mwisho wa siku akamalizia kudhalilisha wananchi pasipo uchunguzi wa haki.
Na huyo sio mwingine ni gamble, sijui ataelewana na kiongozi yupi hapo chugakuna kajiharufu ka wivu hivi hapa.
Juzi wakati nipo Samunge gari iliyokuwa inaongoza msafara wake kidogo inigonge yaani
Naam, wewe utakua ni mkazi wa Arusha. Huyu kijana amesaidia wananchi wengi Sana,, bila kujali itikadi zao. Binafsi niliwahi kufika Mara kadhaa ofisini kwake, akifika anawasalimia wananchi kwa nidham huezi amini ni Mkuu wa wilaya. Kuna wanasheria zaidi ya kumi pale ofisini kwake wa kujitolea kwa ajili ya kuwasaidia wananchi yeye ndo naskia anawafadhili. Amekua anafanya semina za ujasiriamali kuwafundisha Wanawake na vijana ujasiriamali.Kwakweli huyu mkuu wa wilaya ya Arusha simjui vizuri ila ni mtu poa sana.
Nakumbuka mwishoni mwa mwaka jana alitusaidia kupata mafao yetu NSSF baada ya kusumbuliwa karibia mwaka mzima.
Nnachokumbuka tulimfata siku moja tuna akatuambia turudi baada ya siku 3, na tulivyorudi aliondoka na sisi hadi kwenye ofisi za nssf pale Arusha na akaingia na sisi hadi ndani, akakagua computer za pale kwa sababu tulimweleza namna tunavyopigwa danadana muda mrefu bila majibu ya kueleweka....
Meneja alijitahidi kujitetea kwa uongo mwingi lakini kupitia mkuu huyu wa wilaya tulipata mafao yetu bila kuchelewa.
Kumbuka tulikua wengi hivyo alitusaidia sana
Namkubali sana maana amesaidia watu wengi kuanzia waliodhulumiwa maeneo yao, migogoro ya kifamilia na mengine mengi... Kwakweli nilimkubali hadi nikawa nahudhuria kwenye ziara zake za kusikiliza kero za wananchi.
Yule aliyekuwepo kabla yake tulimfata akatufukuza na maneno mbovumbovu bahati nzuri hakumaliza mwezi akaondolewa ndio akaletwa aliyepo sasa.
Hii ni KAZI ya Gambo, sio MTU mwingineMajungu si MTAJI useme utafanikiwa.......
Baadhi ya watu wa ARUSHA NA KILIMANJARO hawawapendi MADC NA MARC wenye misimamo dhidi ya "MADILI YAO"...
Yaani kusikia tu mh.Rais anaandaa "MKEKA WA MADC" basi watu wanajiandaa kuwachafua WENGINE(TARNISHING OF IMAGE)....
#KaziIendelee
Kama walivyomwonea wivu sabaya?kuna kajiharufu ka wivu hivi hapa.
Halafu wanatuona sisi wananchi ni hamnazo. Huyu DC wengi wanaomba abaki, isipokua Gambo. Sasa sijui atafanya KAZI na naniWakati mwingine uwe unauliza sisi wa zamani tunajua ni kamati ya ulinzi na usalama yenye DC ,ocd dso mkuu wa kikosi jwtz uhamiaji magereza takukuru fire na das wanakagua miradi itakayozinduliwa na mwenge wa uhuru.muache kuandika mambo msiyoyajua.
Gambo alikua mwonevu, na sasa hapendi viongozi wenzake. Amejisahau kwamba yeye saivi sio mkuu wa mkoa Bali ni mbunge. KILA Rc, DC Ras na Def yeye hua lazma awakatae. Majungu anavyofanywa saizi ni sababu huyo DC anapita hiki KWENYE kata kutatua kero za wananchi. Sasa Gambo yeye hataki, anataka yeye ndo aonekane KILA kitu anafanya.Mkuu umekata mzizi wa fitina kabisa hiyo mikoa miwili kila siku ma DC na RC wanaoneka wabaya tu gambo wakati wake alikuwa strong sana na alifanya kazi nzuri sana,hao wafanya biashara na wanasiasa hasa hao wawili ni shida sana wanataka waangaliwe tu kwa chochote wanachotaka hata kama si halali kwa manufaa yao binafsi, suala la Sabaya kuna uwezekano mkubwa kuna watu nyuma yake wameunda hayo mambo busara na umakini unahitajika sana maana kila kukicha watu wanaibuka tu sijui kabla walikuwa wapi.
Duuu mwogope Mungu. Wananchi yupo na tunaona. Halafu mama hafanyi KAZI kupitia mitandao ama kwa kuskiza cheap gossips. Uraisi ni TAASIS, taarifa za jinsi huyo DC anafanyaje majukumu yake zipo kwa usahihiChondechonde Mhe Rais
Huyu kijana mwenzetu hastahili kabisa kuwepo kwenye mkeka wako wowote ule.
Hivi kweli kabisa kijana mdogo kama huyu kuwachapa watu wazima viboko hadharani ni utawala bora kweli.
Hata huko magereza waliohukumiwa viboko wanachapwa faragha.
Mhe. Rais huyu kijana hana sifa za uongozi kabisa.
Kwanza anamajivuno
Pili anapenda kujichukulia sheria mikononi.
Tatu anadharau kwa viongozi hata watendaji wa chini
Anaonyesha uwezo wake wa kufikiri ni Mdogo Sana ukifuatilia mambo anayofanya.
Wale ni wafanyabiashara ama waizi?? YANI unatuma watoto waibe dawati kwa shilingi 500???Angekutandika viboko kama wale wafanyabiashara usingesifia ujinga wake.
Sabaya alipokuwa anakuja kufanya fujo hapo yeye alikuwa wapi?Mwezi uliopita kama kumbukumbu zangu zipo sana alizindua mradi mdogo {mradi uchwara} wa kufyatua matofali wa halmashauri ya Jiji la Arusha.Huo msafari ungefikiri anakwenda kuzindia kinu cha Nyuklia gari zilikuwa zinakimbizwa,ving'ora na taa za magari yote zikiwashwa full light.Tutakae tukubali Vijana wakipewa madaraka kidogo wanaharibu sana,wanaumiza wananchi sana,wanatumia madaraka vibaya sana bahati mbaya Mkuu wa Wilaya ya Arusha yumo katika kundi hilo.
Nimetazama hii video kidogo tu nikashindwa kuendelea...jamani tuelezane ukweli, hii tabia ya kishenzi ya kuwadhalilisha wananchi imetoka wapi?Tatizo sio Ma DC vijana kiongozi,, tatizo ni Ma DC wanaotokea UVCCM.