Mkuu wa wilaya Kigamboni asema wanajeshi wanapiga na kuua wananchi

Mkuu wa wilaya Kigamboni asema wanajeshi wanapiga na kuua wananchi

Ameyasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa Mh Chalamila alipofanya ziara wilayani hapo. Mheshimiwa Chalamila ameahidi kukutana na Mkuu wa Majeshi.

Hii imekaaje wadau maana naona kiongozi wa Serikali anaituhumu Serikali yake mbele ya wananchi . Nadhani angefanya vile Mbunge au Diwani ndio ingekuwa sahii, lakini kwa mkuu wa wilaya asingetakiwa kusubiria ziara ya mkuu wa Mkoa .

Anyway huyo Mhe ni Mtoto wa Mzee Bulembo.

Tuhuma za kuua wananchi ni kubwa sana na ni vema kama ni kweli basi hatua zichukuliwe
Sasa mkuu wa wilaya kigamboni unamwambia nani? Kwani kabla ya ziara ya mkuu wa mkoa ulikuwa hulijui hilo? Sasa ulichukua hatua gani?

Raia wanalalamika, tena na wewe kiongozi badala ungechukua hatua kwa nafasi yako kutatua hiyo kero na wewe tena unavizia ziara ili ulalamike....

Duuh! Mbona maajabu!!!
 
By the way Halima ni mdogo sana kiumri ukilinganisha na madaraka yake ya u-DC.

Sidhan

Ameyasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa Mh Chalamila alipofanya ziara wilayani hapo. Mheshimiwa Chalamila ameahidi kukutana na Mkuu wa Majeshi.

Hii imekaaje wadau maana naona kiongozi wa Serikali anaituhumu Serikali yake mbele ya wananchi . Nadhani angefanya vile Mbunge au Diwani ndio ingekuwa sahii, lakini kwa mkuu wa wilaya asingetakiwa kusubiria ziara ya mkuu wa Mkoa .

Anyway huyo Mhe ni Mtoto wa Mzee Bulembo.

Tuhuma za kuua wananchi ni kubwa sana na ni vema kama ni kweli basi hatua zichukuliwe
La Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama?! Analalamika .! Hadharani! Mhhh Utumishinwa Umma uneingiliwa!
 
Mkuu wa Wilaya ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika eneo lake la Utawala,hivyo majeshi yote yaliyopo ndani ya mipaka yake ya Utawala yapo chini yake.Hakupaswa kulalamika mbele ya Rc bali alitakiwa kuwachukulia hatua kama ni kweli au angepeleka taarifa hizo kwa Rc ofisini na si public.
Exactly. Mkuu wa Wilaya kulalamika kwa mambo yanayotokea ktk eneo lake la ki-utawala, inamaanisha kazi alopewa na Mh. Rais ya kumwakilisha Wilayani hapo IMEMSHINDA. i.e. Ateuliwe mwingine kwani hivyo viatu hawezi kuvivaa.
 
Ameyasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa Mh Chalamila alipofanya ziara wilayani hapo. Mheshimiwa Chalamila ameahidi kukutana na Mkuu wa Majeshi.

Hii imekaaje wadau maana naona kiongozi wa Serikali anaituhumu Serikali yake mbele ya wananchi . Nadhani angefanya vile Mbunge au Diwani ndio ingekuwa sahii, lakini kwa mkuu wa wilaya asingetakiwa kusubiria ziara ya mkuu wa Mkoa .

Anyway huyo Mhe ni Mtoto wa Mzee Bulembo.

Tuhuma za kuua wananchi ni kubwa sana na ni vema kama ni kweli basi hatua zichukuliwe
Cha kushangaza huyo Mkuu naye kaagiza yeyote anayevunja nyumba kwa nia ya kuiba akikamatwa auawe. Kalitoa hilo mbele ya wananchi na kuita Afisa mmoja na kumpa amri hiyo. Sababu alizozitoa ni kuwa huyo afanyaye hivyo, anataka mambo matatu. Mosi kuiba, pili kuua mwenye nyumba na tatu kuuawa. Hivyo basi, pindi akikamatwa atimiziwe hilo la mwisho. Nimebaki kinywa wazi kwa mshangao!!!
 
Tatizo tuna Jeshi kubwa wakati hakuna hata dalili za vita.
Siiafiki kauli hii kwa sababu:-
1. Kuwa na jeshi kubwa halafu kukakosekana dalili za vita sio ndo kigezo cha kunahalalisha wanajeshi wapige na kuua watu - kama ni kweli lalamiko hilo.
2. Mbona Sheria zipo na wanaosimamia utekelezwaji wa sheria hizo wapo. Je wanajeshi wapo juu ya sheria?
3. Jeshi kubwa ni lile lenye wanajeshi (Wanaovaa combat i.e. Active) wangapi? Kumbuka Watanzania wengi sana wamepita JKT au wamepitia mafunzo ya mgambo - wote hao ni wanajeshi lakini sio active. Likitokea la kutokea (na hatuombei) Ndo utaona jeshi kubwa.
 
Cha kushangaza huyo Mkuu naye kaagiza yeyote anayevunja nyumba kwa nia ya kuiba akikamatwa auawe. Kalitoa hilo mbele ya wananchi na kuita Afisa mmoja na kumpa amri hiyo. Sababu alizozitoa ni kuwa huyo afanyaye hivyo, anataka mambo matatu. Mosi kuiba, pili kuua mwenye nyumba na tatu kuuawa. Hivyo basi pindi akikamatwa basi atimiziwe hilo la mwisho. Nimebaki kinywa wazi kwa mshangao!!!
Dah! Ama kweli walisema kua uyaone. Hata mm nimeshangazwa mno na kauli hii kutoka kinywani mwa Aliyekabidhiwa Dhamana ya Ulinzi na Usalama katika eneo lake. Hii inji bhana .... :KEKBye:
 
Mkuu wa Wilaya ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika eneo lake la Utawala,hivyo majeshi yote yaliyopo ndani ya mipaka yake ya Utawala yapo chini yake.Hakupaswa kulalamika mbele ya Rc bali alitakiwa kuwachukulia hatua kama ni kweli au angepeleka taarifa hizo kwa Rc ofisini na si public.
Awachukulie hatua kina nani ??!
Unawajua ??!
 
Mkuu wa Wilaya ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika eneo lake la Utawala,hivyo majeshi yote yaliyopo ndani ya mipaka yake ya Utawala yapo chini yake.Hakupaswa kulalamika mbele ya Rc bali alitakiwa kuwachukulia hatua kama ni kweli au angepeleka taarifa hizo kwa Rc ofisini na si public.
DC anaweza kumchukulia hatua gani mwanjeshi? hebu tupe elimu kidogo mkuu huenda namm siku moja naikawa dc
 
Mkuu wa wilaya yupo sahihi,kama amejiridhisha kwa hizo tuhuma kwanini asiseme! Juzijuzi kule Vunjo kuna raia aliuawa na askari wa Tanapa na maiti yake kukutwa huko msituni lakini kuna kiongozi mmoja alitoa taarifa kwamba marehemu alijinyonga lakini uchunguzi wa daktari ulibaini mwili ulikuwa na majeraha ya risasi.
Je mlitaka huyo DC wa Kigamboni naye aseme wananchi wamejipiga na kujiua wenyewe?
Nanukuu:
"Mkuu wa wilaya yupo sahihi,kama amejiridhisha kwa hizo tuhuma kwa nini asiseme!"
Kwa kauli hiyo 👆 👆 👆 , ni wazi kabisa bila hata ya kupepesa macho au kumung'unya maneno; Mkuu huyo wa Wilaya ni completely Inefficient katika nafasi hiyo.
Kama ameweza kufuatilia na kujiridhisha kabisa pasi na shaka , imemshinda nini kuchukua Hatua stahiki? Yan ameona na kuridhika kabisa kwamba yy hawezi, lakini kwa kukosa hekima na busara akaona aseme kwa kulalamika kama mtoto mdogo tena hadharani?
**Zamani Wateule wa Rais walikuwa wanapelekwa Semina e.g. Ngurdoto walau kwa siku chache kabla hawajaanza rasmi kutekeleza majumu yao.
 
Sasa mkuu wa wilaya kigamboni unamwambia nani? Kwani kabla ya ziara ya mkuu wa mkoa ulikuwa hulijui hilo? Sasa ulichukua hatua gani?

Raia wanalalamika, tena na wewe kiongozi badala ungechukua hatua kwa nafasi yako kutatua hiyo kero na wewe tena unavizia ziara ili ulalamike....

Duuh! Mbona maajabu!!!
Hakuna maajabu ila iko vile !
Nadhani ameamua au kwa kushauriwa aliweke jambo hilo wazi ili liwe na nguvu na kulifanya lishughulikiwe na wanaohusika ,
 
Mkuu wa Wilaya anastahili pongezi kwa kufichua huo uovu wa Wanajeshi, wakamatwe waletwe Mahakamani na wakipatikana na hatia waning'inizwe.
Wana mahakama zao makambini kwao !
Hawawezi kuwapeleka mahakama za kiraia mpaka awe ameacha kazi. !
 
Back
Top Bottom