Mkuu wa wilaya Kigamboni asema wanajeshi wanapiga na kuua wananchi

Mkuu wa wilaya Kigamboni asema wanajeshi wanapiga na kuua wananchi

Mkuu wa Wilaya anastahili pongezi kwa kufichua huo uovu wa Wanajeshi, wakamatwe waletwe Mahakamani na wakipatikana na hatia waning'inizwe.
Khe! Kwani ilikuwa ni siri?
Huyo Mkuu wa Wilaya anastahili awe ameshaondolewa(Kutumbuliwa) kwenye nafasi hiyo tena kwa haraka sana kwani ameiumbua Serikali iliyomweka hapo Ofisini ie. Mh. Rais amemteua kilaza fulani kushika nafasi kubwa na nyeti kama hiyo. Kwa kifupi ni kama Baba wa nyumbani analalamika eti watoto wake mwenyewe 7-9 yrs old ameshindwa kuwadhibiti.
 
Ameyasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa Mh Chalamila alipofanya ziara wilayani hapo. Mheshimiwa Chalamila ameahidi kukutana na Mkuu wa Majeshi.

Hii imekaaje wadau maana naona kiongozi wa Serikali anaituhumu Serikali yake mbele ya wananchi . Nadhani angefanya vile Mbunge au Diwani ndio ingekuwa sahii, lakini kwa mkuu wa wilaya asingetakiwa kusubiria ziara ya mkuu wa Mkoa .

Anyway huyo Mhe ni Mtoto wa Mzee Bulembo.

Tuhuma za kuua wananchi ni kubwa sana na ni vema kama ni kweli basi hatua zichukul
 
Wavuliwe Magwanda kibarua kioteshwe majani wasifikiri kuwa wao ni Miungu watu.
Mkuu; Hawavuliwi magwanda kihovyo-hovyo au kirahisi-rahisi kama unavyodhani. Tena kibarua kuotesha majani kibarua chao napo ni kazi pia.
 
Mkuu wa Wilaya ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika eneo lake la Utawala,hivyo majeshi yote yaliyopo ndani ya mipaka yake ya Utawala yapo chini yake.Hakupaswa kulalamika mbele ya Rc bali alitakiwa kuwachukulia hatua kama ni kweli au angepeleka taarifa hizo kwa Rc ofisini na si public.
Achukue hatua kama zipi?
 
Mkuu; Hawavuliwi magwanda kihovyo-hovyo au kirahisi-rahisi kama unavyodhani. Tena kibarua kuotesha majani kibarua chao napo ni kazi pia.
Kwa umri wangu huu nimeona wengi wakitimuliwa na kufukuzwa kazi kwa makosa mbali mbali yakiwemo ya utovu wa nidhamu.
 
Kwa umri wangu huu nimeona wengi wakitimuliwa na kufukuzwa kazi kwa makosa mbali mbali yakiwemo ya utovu wa nidhamu.
Mkuu; Ukisikia "Utovu wa nidhamu" Jeshini unaficha mengi sana. Usidhani ni neno jepesi kivile kauli hiyo. Unaweza kukumbuka ni wanajeshi wangapi wamelambana shaba na ni kwa nini? Unajua ni kwa nini mwanajeshi anatambulika kwa namba na sio jina tu?
 
Jeshi la tanzania ndo jeshi linaloongoza kwa ushamba kuliko majeshi yote duniani.
Wewe raia unapata wapi jeuri ya kutuita sisi makamanda ni washamba?Nchi tumeiepusha kwenye kuvamiwa na maadui wewe unatuita washamba?hebu fafanua maana ya ushamba
 
Mkuu kama n kweli hizi tuhuma zifanyiwe kazi ....m niliwahi toka beach na familia yangu sikumoja narudi hme sijui walikuwa wanamtafuta mtu kilagari ikawa inasimamishwa pemben kuna madogo wanapigishwa kichura chura hatare...ajabu kufungua mlango wakasalimia akaniuliza mbona ujafjbga mkanda pony yangu nilianza na sorry wakuu...wakaona vile vitioto vinaangalia zile adhaabu za wengine wakaniruhusu aisee sijawahi kanyaga tena yaan Beach sijui kuogele an kunduchi
Watoto wenye baba dizaini yako, hao watoto ni yatima
 
Wewe raia unapata wapi jeuri ya kutuita sisi makamanda ni washamba?Nchi tumeiepusha kwenye kuvamiwa na maadui wewe unatuita washamba?hebu fafanua maana ya ushamba
Hapo sasa !! 😳🙏
 
Mkuu wa Wilaya ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika eneo lake la Utawala,hivyo majeshi yote yaliyopo ndani ya mipaka yake ya Utawala yapo chini yake.Hakupaswa kulalamika mbele ya Rc bali alitakiwa kuwachukulia hatua kama ni kweli au angepeleka taarifa hizo kwa Rc ofisini na si public.
Jibu sahihi...
 
Kwa kweli baadhi ya wanajeshi wana ubabe wa kishamba sana. Juzi wametaka kutuua pale mbezi beach, tangi bovu.
Lori la jeshi lilikuwa likipita service road kwa spidi kubwa sambamba na daladala niliyopanda.
Lilipofika ukingoni mwa service road dereva wa jeshi aliingiza lori wangu-wangu main road, bila kujali hata usalama wa askari jeshi aliowapakia nyuma.
Ilibidi dreva wa daladala ashike break ya nguvu sana mpaka gari likazimika, abiria wameangukiana hovyo.
Jamaa wakatuangalia kwa jicho la "mngetugusa muone" na hawakusimama wala kuonesha kujali, bila kufikiri kwamba ajali ingetokea isingebagua.
Kila abiria aliyetaka kutukana akabaki anamung'unya maneno kooni baada ya kuona jamaa wa mabakabaka ndiyo waliotaka kutusabishia ajali. Nilisikitika sana.
Jamaa baadhi hawana akili na hawajitambui kabisa, hawana upendo kwa watu wengine
 
Ameyasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa Mh Chalamila alipofanya ziara wilayani hapo. Mheshimiwa Chalamila ameahidi kukutana na Mkuu wa Majeshi.

Hii imekaaje wadau maana naona kiongozi wa Serikali anaituhumu Serikali yake mbele ya wananchi . Nadhani angefanya vile Mbunge au Diwani ndio ingekuwa sahii, lakini kwa mkuu wa wilaya asingetakiwa kusubiria ziara ya mkuu wa Mkoa .

Anyway huyo Mhe ni Mtoto wa Mzee Bulembo.

Tuhuma za kuua wananchi ni kubwa sana na ni vema kama ni kweli basi hatua zichukuliwe
Labda wanamdharau pia inawezekana kashindwa kutimiza jukumu lake km mwenyeki wa ulinzi wa wilayaya husika
 
Back
Top Bottom