Brake✔Kwa kweli baadhi ya wanajeshi wana ubabe wa kishamba sana. Juzi wametaka kutuua pale mbezi beach, tangi bovu.
Lori la jeshi lilikuwa likipita service road kwa spidi kubwa sambamba na daladala niliyopanda.
Lilipofika ukingoni mwa service road dereva wa jeshi aliingiza lori wangu-wangu main road, bila kujali hata usalama wa askari jeshi aliowapakia nyuma.
Ilibidi dreva wa daladala ashike break ya nguvu sana mpaka gari likazimika, abiria wameangukiana hovyo.
Jamaa wakatuangalia kwa jicho la "mngetugusa muone" na hawakusimama wala kuonesha kujali, bila kufikiri kwamba ajali ingetokea isingebagua.
Kila abiria aliyetaka kutukana akabaki anamung'unya maneno kooni baada ya kuona jamaa wa mabakabaka ndiyo waliotaka kutusabishia ajali. Nilisikitika sana.
Break❌