Mkuu wa wilaya Kigamboni asema wanajeshi wanapiga na kuua wananchi

Brake✔
Break❌
 
Wanajeshi wanatakiwa wajue kuwa kazi tuliyowatuma ni kutulinda dhidi ya Maadui wa kutoka nje sio kutugeukia sisi wenyewe ambao ndio walipaji mishahara yao.
 
Tatizo tuna Jeshi kubwa wakati hakuna hata dalili za vita.
You're completely Wrong in this idea.

Tatizo lipo ktk Jeshi lenyewe, hususani kwenye suala la Mitaala yao ya Mafunzo, Nidhamu, na mifumo yao yote ya Utawala sambamba na ubovu wa Sheria za nchi zilizopo ukianzia na Katiba ya nchi hii.
 
Tatizo tuna Jeshi kubwa wakati hakuna hata dalili za vita.
Hivi huwa hawawapeleki kwenye mission? Ujue wasoja wa Bongo wapo wapo tu yaani, wengine wanauza na kupangisha fremu na maduka
 
Mkuu utumishi wa umma si unataka miaka 18 ukitoa hizo qualifications zingine?

Nimezungumzia madaraka na siyo utumishi.

Cheo chake ni kikubwa sana ukilinganisha na umri
 
Ndio shida ya, hv vyeo vya kuteuliwa, MTU hana elimu hata ya kuwa mama, ntilie, kisa, baba ni kada wa CCM, anateuliwa kuwa DC!
Na, yeye analalamika! Mwenyekiti wa, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya! Ambayo Ina officer wa, jeshi kama liaison officer na jeshi!
Hili swala angeweza kulitatua, vzr tu kwa kufata taratibu ndogo,
M jeshi kapiga raia,mtafute raia andikisha maelezo polisi, mfate huyo mjeda,atiwe mitama kidogo baaasi!
 
Ki Katiba na Utendaji Jeshi letu liko karibu sana na WANANCHI ndio maana likaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania

Watuhumiwa wasakwe wavuliwe Magwanda tukutane MAHAKAMANI!!!!
 
Wanajeshi kuua Wananchi siyo jukumu lao wao waende wakatulindie mipaka huko.
 
Huyu ni DC kwa sababu ni mtoto wa mzee Bulembo na ni muumini mwenzetu!! Nje ya vigezo hivyo huyo binti na mama yake mdogo ambaye ni DC wa Bagamoyo hawakustahili hata Utendaji wa Kata
 
You're completely Wrong in this idea.

Tatizo lipo ktk Jeshi lenyewe, hususani kwenye suala la Mitaala yao ya Mafunzo, Nidhamu, na mifumo yao yote ya Utawala sambamba na ubovu wa Sheria za nchi zilizopo ukianzia na Katiba ya nchi hii.
Mie naona KATIBA NDIO INAMAPUNGUFU MENGI SANA
 
Tatizo tuna Jeshi kubwa wakati hakuna hata dalili za vita.
Hili tatizo ni la siku zote. Halijaanza leo. Na serikali haitaki kulimaliza kwani wanataka wananchi waogope wanajeshi ili hata wakiibiwa kura waogope kupigania haki yao. BTW mna uhakika huyo mkuu wa wilaya hanyemelei hilo jimbo kiubunge? Unachaguzi unapokaribia kila mwanasiasa anajifanya yuko upande wa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…