Mkuu,
Mimi ni mdau wa Kisarawe. Pugu, Kazimzumbwi, Kinyanyiko, Minaki, Chanzige, Maneromango, Samvulachole, Masaki (original), kote kwetu huko. Sasa niko New York City.
Nafurahi kumuona DC wa Kisarawe akifanya kazi kupitia mitandao, napata habari za kazi zake mara moja. Anafanya kazi kwa "ushirikishwaji wa umma", si kwa kujifungia.
Wewe hujalazimishwa kufuatilia habari za Kisarawe wala kuchangia. Kama unaona hazikuhusu, zipotezee tu.
Kwani kuna mtu kakulazimisha kufuatilia na kuchangia habari hizi?
Kikubwa zaidi, DC namjua naweza kumtafuta mara moja nikamuambia hapo kuna mtu gani atakusaidia vipi, mtu gani muepuke, fulani mwizi, sokoni kuna mpango gani wa kuuangalia. Hospitali pale kuna upigaji gani.Nawajua watu wa pale kwa namna ambayo yeye itakuwa vigumu kuwajua mara moja.
Sasa hapo napo utalaumu DC kufanya kazi kwa uwazi mitandaoni ili hata watu wa Kisarawe tulio New York City na sisi tujue maendeleo ya kwetu na kusaidia?