Mkuu wa Wilaya ya Ubungo adhamiria kutokomeza biashara ya ukahaba

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo adhamiria kutokomeza biashara ya ukahaba

Hongera sana Mkuu wa wilaya ya Ubungo kwa kudhamiria kutokomeza biashara haramu ya kuuza mili.
Leo hii tarehe 6/06/2024 Mkuu wa wilaya amekamata jumla ya madada poa 20 wakiwemo wateja wa biashara hiyo.

Tunaomba moto huu usipoe, bado maeneo ni mengi sana, sisi wananchi tutafichua vichaka vyote.

Chanzo ni chanel ten habari sa 1 usiku leo hii tarehe 06/06/2024

Ukiangalia wasichana na wamama walio kamatwa utabaki kinywa wazi.

Pamoja na kuwakamata, dawa pia ni kuvunja madanguro yote lakini pia kuwapiga picha makahaba wote na picha sura zao kisha zionyeshwe kwenye tv na mitandao ya kijamii.
Hawa wana siasa ndivyowanavyowadanganya wakati wao ndiyo wateja wakubwa wa makahaba? Au kwa kuwa wanatembea na makahaba wanaouza bei ghali na kutaka kuhongwa magari ndiyo mnadhani siyo makahaba? Hawa ma-slayqueen wooote unaowaona kwenye mitandao wanaojiita ni wasanii wengi wao ni makahaba wa wanasiasa. Kamuulize mbunge wa Ulanga.
 
Aende pia Riverside kuna baa inatazama kituo cha daladala zielekeazo Buguruni. Kuna siku nilienda saa nane usiku kama abiria wa bus la Tilisho, sikuamini kilochopo
Nani aende? Mnapigwa changa la jicho na wanasiasa? Wanasiasa wengi wanaume mbona wana makahaba wasanii?
 
Nani aende? Mnapigwa changa la jicho na wanasiasa? Wanasiasa wengi wanaume mbona wana makahaba wasanii?
Tusidharau kila kitu. Kama kuna hatua zinafanyika au hazifanyiki, zitaonekana tu. Jambo la msingi ni kuwa kila mtu afanye lililo ndani ya uwezo wake, mfano, kama unaweza kutoa taarifa, just toa tu utakuwa umetimiza wajibu wako. Usiache kufanya eti kwa kuhofia wengine hawatatimiza wajibu wao
 
Pamoja na kua wengi wao ni wasambaza ngoma kwa makusudi hasa usipokua makini ila huyo mkuu wa wilaya aache kuchota akili za vilaza na kuwatumia kisiasa.
 
Biashara hiyo ndio biashara kongwe Kati ya biashara zote Duniani. Labda atafanikiwa, ngoja tuone!
Hiyo biashara ni rahisi sana kuifuta, waboreshe maisha ya watu kwa kushusha bidhaa km umeme, maji na pia watoe ajira za kutosha
 
Wataalamu Ndiyo wanatengeneza sera bunge huzijadili na kuzipitisha, labda wataalamu wamesahu kukutengezea sera za kukupa furaha, swali fikirishi je wewe furaha yak ni kuchimba migodi hadharani, yaani watu wakifanya umalaya mtaani kwako, hili swala siyo la mkuu wa wilaya peke yake

Wafanye kuwepo mitaa maalum kwa huduma hiyo iliyojaa madanguro yatakayokaguliwa usafi wa mazingira, mwili na afya za watumiaji pia watoa huduma.

Machine za TRA kulipia kodi, pia kodi za kuzoa taka, usafi wa mitaa hiyo maalum kama Uturuki vile:

Ukahaba nchini Uturuki ni halali na kuratibiwa kupitia mamlaka za taasisi za kiserikali. Sera za kisekula za jamii ya Kituruki zilianza kuliruhusu ukahaba wakufikia hadhi ya kisheria mwanzoni mwa karne ya 20.

Inajulikana kama "nyumba za jumla" ( genelevler ) nchini, madanguro lazima kupokea vibali kutoka kwa serikali kufanya kazi.

Kwa upande mwingine, mashirika ya udhibiti hutoa kadi za utambulisho kwa wafanyabiashara ya ngono ambazo zinawapa haki ya kupata huduma za matibabu bila malipo na huduma zingine za kijamii . [1]

Hata hivyo, serikali nyingi za mitaa sasa zina sera ya kutotoa usajili mpya, na katika baadhi ya miji, kama vile Ankara na Bursa , madanguro yamebomolewa kwa amri ya mahakama . [ nukuu inahitajika ]

Kufikia mapema miaka ya 1900, idadi inayokadiriwa ya makahaba waliosajiliwa huko Istanbul ilikuwa 2,000. [2] Ndani ya idadi hii ya watu, utafiti uliofanywa mwaka 1919-1920 ulihitimisha kwamba asilimia sitini ya wanawake hawa hawakuwa Waislamu na asilimia arobaini walikuwa Waislamu; hata hivyo, idadi hii haikuwahusu makahaba waliokuwa wakifanya kazi kinyume cha sheria. [2]

Uchunguzi ulionyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wa Kiislamu walikuwa wakijihusisha na ukahaba kinyume cha sheria au kwa siri, ikilinganishwa na wenzao wasio Waislamu. [2]

Kwa miaka mingi, idadi inayoongezeka ya wanawake walianza kukimbilia ukahaba kama njia ya mapato ya kifedha. Wanawake wengi walioingia kwenye ukahaba walifanya hivyo kutokana na kuwa mama wasio na waume single mothers, ukosefu wa makazi, umaskini, na kumudu huduma za malezi ya watoto. [2]

Ingawa ni wanawake waliosajiliwa na ambao hawajaolewa pekee walio na umri wa zaidi ya miaka kumi na minane wanaweza kufanya kazi katika madanguro yaliyodhibitiwa na serikali, wale ambao hawajasajiliwa wanalazimika kufanya kazi nje ya mfumo. [3]

Kwa hivyo, wanawake ambao hawakujiandikisha walilazimika kufanya kazi katika madanguro haramu, kama wapita njia, na kuuza huduma za ngono kutoka kwa nyumba zao.
 
MASHARTI VIGEZO NA KANUNI ZINAZOTUMIKA KURATIBU MADANGURO NA BIASHARA HUSIKA

Mbali ya kipato,tozo,kodi pia sheria hii nchini Uturuki imeweka kipaumbele kuhusu afya za watoa huduma na walaji.

Hali ya kisheria​

Ukahaba nchini Uturuki unadhibitiwa chini ya kifungu cha 227 cha Kanuni ya Adhabu ya Uturuki (Sheria Na. 5237). [4] Kutangaza matangazo ya ukahaba hairuhusiwi pia adhabu ya kifungo cha miezi miwili hadi miaka minne. Sheria ya pasipoti [5] inakataza kuingia Uturuki kwa madhumuni ya ukahaba.

Madanguro ( Genelev ) ni halali na yana leseni chini ya sheria za afya zinazohusika na magonjwa ya zinaa . [6] Wanawake wanahitaji kusajiliwa na kupata kitambulisho kinachoeleza tarehe za uchunguzi wa afya zao. Ni lazima kwa makahaba waliosajiliwa kufanyiwa uchunguzi wa afya mara kwa mara wa magonjwa ya zinaa, na matumizi ya kondomu ni ya lazima. [7] Polisi wanaruhusiwa kukagua uhalisi wa makahaba waliosajiliwa ili kubaini kama wamechunguzwa ipasavyo na kuhakikisha wanaona mamlaka ya afya ikiwa hawafanyi hivyo.

Wanaume hawawezi kujiandikisha chini ya kanuni hii. Makahaba wengi, hata hivyo, hawajasajiliwa, kwani serikali za mitaa zimeweka sera ya kutotoa usajili mpya. [8] [9]

Kanuni nyingine zinazoathiri makahaba nchini Uturuki ni pamoja na Sheria ya Misdemeanor , Kifungu cha 32. [10] Hata hivyo, matumizi ya sheria hii yamekuwa na utata. [11] Katika baadhi ya miji, kama vile Ankara na Bursa , madanguro yamebomolewa kwa amri ya mahakama. [12] [13]

Ingawa sheria zilitungwa kudhibiti ukahaba na kuenea kwa magonjwa ya zinaa, sheria hizi huwawajibisha wafanyabiashara ya ngono zaidi ya kuwanufaisha.

Wafanyabiashara ya ngono lazima wapimwe magonjwa ya zinaa mara mbili kwa wiki katika hospitali zilizotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara ya ngono waliosajiliwa. [14] Ingawa hakuna sheria inayowatia hatiani wafanyabiashara ya ngono haramu, bado wanaweza kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu ikiwa watakamatwa na utekelezaji wa sheria. [14]

Ingawa sheria na sera kuhusu ukahaba nchini Uturuki zinalenga kufaidi afya ya umma, hazizingatii haki za wafanyabiashara ya ngono. Licha ya kanuni kali za ukaguzi wa afya, wanaume wanaolipia ngono hawafanyiwi uchunguzi wowote wa kimatibabu kwa magonjwa ya zinaa. [14]

Huenda hii ni kutokana na juhudi za serikali kuweka madanguro wazi kwa ajili ya “mahitaji ya ngono ya wanaume.” [14] Uvumilivu wa jinsia ya kiume na ukosefu wa uchunguzi wa kimatibabu, adhabu, au adhabu yoyote kwa wateja wanaonunua ngono huchochea ukuaji wa biashara ya ngono nchini Uturuki. [14]
 
Hapa kuna biashara ya kuuza mwili na mm ni mteja wao... Changamoto ni kwamba usipokuwa na pesa hupati huduma...
 
Tusidharau kila kitu. Kama kuna hatua zinafanyika au hazifanyiki, zitaonekana tu. Jambo la msingi ni kuwa kila mtu afanye lililo ndani ya uwezo wake, mfano, kama unaweza kutoa taarifa, just toa tu utakuwa umetimiza wajibu wako. Usiache kufanya eti kwa kuhofia wengine hawatatimiza wajibu wao
Una umri gani wewe? Ni mara ya kwanza usanii kama huu kufanyika? Unadhani ku deal na dalili kunaondoa ugonjwa? Tafuta kwanza sababu zinazofanya ukahaba uwepo kwa wingi ushughulike nazo.
 
Back
Top Bottom