Aisee,pole sana mkuu,nimesoma nimesikitika sana,kwanza nikupongeze kwa uvumilivu na uaminifu ulionao kwa mkeo,ni wachache sana wanaoweza kushinda hili karibu.
Kama ilivyozoeleka ni kwamba ndoa ni watoto,lakini wakati mwingine huja tofauti na matarajio yetu,hapo ndipo wakati wengi hukata tamaa.Nawashangaa sana baadhi ya wanaume wanaokataa watoto,au mimba au kuwadhihaki waliowabebea mimba na kuwazalia watoto,na kufanya waitwe baba. Mungu akusaidie mkuu,upate hitaji la moyo wako,usikate tamaa siku yako ya furaha inakuja.
Endelea kupiga goti wewe pamoja na mkeo,salini kwa pamoja Wala usifikirie kumuacha mkeo kwa sababu hiyo,wakati wa Mungu ndio wakati sahihi.