Mlikutana wapi wewe na mke/mume au mpenzi wako?

Mkuu story tamu fanya kuimalizia
 
Wewe na mpenzi wako katika kuanzisha mahusiano yenu ya kimapenzi.

Je, at the first day mlimeet mahala gani?
sie tumekulia mtaa mmoja so tumecheza kombolela pa1, tumepka ugali mchangan pamoja, michezo ya baba na mama shule ya primary na secondary i-iv pamoja

ni miaka 10 sasa hakka sijawah kuijutia ndoa yetu
 
umemsifia xn aisee,

ntumie no ake nmpe hongera ake
 
Nilienda kwao kupeleka mzigo flani ile nagonga yeye ndo akaja kufungua tuliooangaliana wote tukawa kama tumepigwa ganzi Mimi mdomo ukawa mzito nikaishia kuuliza mama yupo? Nikaungia ndani kukabidhi ule mzigo nilipokua natoka tukaaonana tena akanipa bonge la smile kilichofuata hapo ni historia
 
Nikikutana nae ntakuja kuleta story hapa...
 
Tulikutana kwenye ndege tulikua tunaenda kwa malkia, mimi ndio ilikua mara yangu ya kwanza kupanda ndege na kusafiri nje ya nchi.. so ule ushamba na hofu ya ndege + vishuzi vya kimya kimya alinigundua maana tulikaa siti moja, basi akaanza kunisemesha kunitoa hofu na akanipa ushirikiano mkubwa sana ili nipoteze mawazo na hofu kufikiria mambo ya kipuuzi ndani ya ndege. basi tulikutana hapo tukapeana namba tukaanza kuwasiliana baada ya muda mimi niliwahi kurudi bongo, then nae akarudi bila kupoteza muda tukaanzisha mahusiano.
 
Noma sana, tulikutana viwanja vya Soweto A city mtoto wa mashavuni naona alielewa slang za mselaa wa kidevuni. Nikapiga masauti mtoto akajaa mwaka wa 4 huu tupo kwa fasi ni toto kali laana
 
Mpenzi wangu tulikutana 1931 nijijini wakati naenda kupeleka ngombe malisho ndiyo ikawa first time, amekuwa mchumba tumeenda hadi leo n mke wangu, ambae leo n bibi yenu
 
Nilipewa namba na dogo baada ya kumuoa dem ni makali na akili ipo. Then nikampigia tukaonana na mahusiano yetu yalianzia hapo mpaka leo ndo wife.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…