Mlinzi wa Rais kuvaa sare za chama ni sahihi?

Safari hii mishale itakuwa ya kutosha, mpaka kila kitu kwenu kinakuwa uvunjifu wa katiba.
 
Atajiondoa kwa hoja zake tu Dr Alexander
 
Hata wewe ni usalama wa taifa..... Muhimu ni uzalendo mavazi kitu gani bwashee!
 
Unachokiona wewe ni tofauti na yeye anachokikusudia
Yeye anakusudia nini?!

Hapo itakuwa sawa endapo tu hao jamaa sio TISS bali ni walinzi wa kawaida walio kwenye payroll ya CCM!

Lakini kwavile JPM bado ni rais, hata anapofanya shughuli za chama bado urais wake upo pale pale na kwahiyo bado Walinzi wa Rais ambao ni mali ya serikali wataendelea kutekeleza wajibu wao.

Hata hivyo, hawatakuwa wanatekeleza wajibu wako kwa Mwenyekiti wa chama bali kwa rais, na wao watakuwa hapo kwa niaba ya serikali na sio kwa niaba ya chama hadi wafikie kuvaa sare za chama!!
 
Kama kifungu ndio kinafuatwa, kwa nini hao walinzi wa Rais wavae ki-CCM wakati wana sare zao rasmi?
Kabla sijakujibu kwa nini wanavaa hivyo hebu nijibu maswali haya
  1. Sare rasmi ya usalama wa taifa (TISS) ni ipi?
  2. Nani kakuambia kuwa kila mlinzi wa rais ni usalama wa taifa (TISS)
  3. Ni sheria ipi inayowazuia usalama wa taifa (TISS) kuvaa nguo za vyama?
 
Katiba na Sheria za Tanzania hairuhusu Mtumishi wa umma kuwa mwanachama wa chama cha siasa
Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama ndio hawaruhusiwi.Watumishi wengine wanaruhusiwa isipokuwa hawatakiwi kufanya siasa katika maeneo ya kazi.
 
Wenzako wako ki professional, wewe unatema pumba. Hivi Rais angekuwa wa Chadema, na hao walinzi wakavaa jezi ya Chadema ungelalamika?
Zama za chama kushika hatamu zimepita., mlinzi wake ni mtumishi wa umma just keep it on your mind
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…