Katiba inakataza watumishi wa umma kujihusisha na shughuli za vyama vya siasa, hasa majeshi kwa namna yoyote ile. Kuvaa sare ya chama cha siasa ni dhahiri kuwa una mahaba na chama husika.
Liko wazi kuwa katiba yetu ina mapungufu juu ya Urais mara bunge linapovunjwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu, kwani Rais anaendelea mpaka mwingine atakapoapishwa.
Kama kifungu ndio kinafuatwa, kwa nini hao walinzi wa Rais wavae ki-CCM wakati wana sare zao rasmi? Hivi na walinzi wa wagombea wengine nao wanavaa sare za vyama vile? Nimeuliza hivi kwani hawa wa Rais sura zao na maumbile yao ya muonekano wa mwili kwa nje yanafahamika.