Mliofanikiwa kutoa Zaka asilimia 10% ya vipato vyenu mmewezaje? Binafsi naishia kusaidia 2% hadi 4%

Ni utayari tu na kuamini kuwa ukitoa utapokea vingi.

Tena unatakiwa kutoa kwa moyo wa ukarimu [emoji4]

Hapo utaona mambo yako mengi yakifunguka na kuwa wazi.

Tena toa kwa Siri ujitangazie kwa mtu awaye yote.

Utakuja ushuhudie ukuu wa Mungu kwenye maisha yako.
 
Mkuu

Uko sahihi,coz hiyo ndio sheria pekee ninayohubiriwa katika ulimwengu wa agano jipya tulilonalo!

Yaani watumishi wameacha SHERIA zote za israel na kukomalia hilo Moja wakiisapoti na Malaki 3;3!

Wakati kuna sheria NYINGI tu ambazo wameziacha wakisema hayupo chini ya SHERIA!

Yesu

Alileta mbadala wa kila sheria

-Amri kumi za Mungu zilinebwa na upendo!yaani mpendane kama Amri mpya!

-Matoleo yalibebwa na kutoa KWA kadiri ulivobarikiwa bila kiwango chochote kama kristo alijitoa mwili wake wote iweje wewe ujitoe KWA asilimia!!?

Ndio maana mtu akiguswa na Roho hawezi toa KWA asilimia kama zakayo alivotoa!!

Pia asili na chimbuko la zaka HALIKUWA AGIZO LA MUNGU KWA WATU WAKE BALI ILIKUWA AHADI ;-

KWANZA KWA IBRAHIMU ALIYETOA NYARA KWA MELKIZEDEK KUHANI MKUU

BAADAE

YAKOBO WAKATI AKIENDA KWA LABAN ALIAHIDI KUTOA SEHEMU YA KUMI YA MALI ZAKE NA IKAFANYIKA SHERIA ILIYOWAKIZA WATOTO WAKE NDIO MANA MUNGU ANAIDAI AHADI ILE KATIKA MALAKI 3;3!

HAYA SHALOM WAKRISTO
 
Mkuu safi sana kwa maelezo mazuri.
Najaribu kutafakari kwanini kwenye agano jipya hakuna mistari inayoeleza suala la zaka? Kama ipo naomba kueleweshwa.
 
Kila nikifikiria kiasi nachotenga kwenye starehe na matanuzi mengine najikuta tu nshachkua bahasha kuweka zaka asee..

Yani matanuzi unaweza kutoa yanazidi hata hiyo 10% ya kipato chako ila unaskia Uzito kutoa kwa Mungu...
Shetani yupo kazini siku zote
 
Zaka inatolewa hekaluni tu na hekalu la mungu lilikuwa moja tu kabla ya kujengwa na baada ya kujengwa hekalu...kasome vizuri zaka ya fungu la 10 ilianzaje na ilitolewa wapi.
 
Usisahau pia kuisha maisha ya utakatifu kwamaana haitasaidia kitu kutoa zaka then hutendi yaliyo mema
Anapotoa pia maombi huwa yanatolewa na mpokea zaka, hivyo lazima yatamkumbusha kuishi impavyo MUNGU wake.
 
Ntajitahidi japo dhambi ndo zimetamalaki
Nikujitahidi tu maana hakuna mkamilifu, ndiyo maana twaambia tukeshe tukiomba ni muda wowote MUNGU kwanza, bila shaka hawezi kukuacha upotee
 
Embu angalia watu wakistaafu wanavyobadilikaga akili pension yao, ukiwa unajitambua wengi humtolea MUNGU kisha wanakaa chini kufikiria atumie vipi! Mungu hawezi kukuacha uaibike kama upo naye karibu.
 
Malimbuko nayo ni amri kama zaka?
 
Hapana kwa kweli ata hiyo 2% tunajitahidi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…