Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Kama ww n mwanaume n kukaza roho mkuu ...huwez badili kitu..mm nmefiwa na mama angu mwezi wa 6 mwaka huu nilipata taarifa asubuh nikiwa tayari naenda kazin tena n mbali na hakuna dereva n ww mwenyew ...IMAGINE NLIPGA KAZ HADI JION NKARUD ZEN NIKAWAAMBIWA WAFANYAKAZI WENZANGU kwamba maza gone!!! Ukizaliwa mwanaume tambua hutakiwi kutia huruma n kukubaliana na tukio lolote. .na katika maisha jiandae kuskia habar yoyote mbaya au zur...OVER
Braza uliweza vip kufanya kaz huku umepewa taarifa kuwa mam ako kafariii duh uliwezaje mkuu hpn mkuu ukipazwa pale pale ujeuze uende kujiandaa na safari tayar kurud nyumbn ukaomboleze

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana. Mungu akupe faraja kuu. Mimi nina experience kufiwa na baba nilikuwa na miaka 7 niliumia sana sana...lakini nilichojifunza ni kwamba haya maisha tuishi kwa kujua kabisa kwamba tunaowapenda ipo siku tutatenganishwa na kifo. Na pia tujua hata sisi tutakwenda na tutawaacha wake zetu, watoto, waume, wazaz na marafiki. Inauma ila tujue tu hiyo ndio nature ya hapa duniani. Raha ya milele uwape ee bwana na Mwanga wa milele uwaangazie, marehemu wote wapumzike kwa amani. Amina.
 
Baada ya kusoma huu uzi imebidi nimpigie simu Mama alisafiri akiwa anaumwa naomba Mungu amponye huko alipo baba yangu alikufa nikiwa mdogo Sana sikumbuki hata sura yake zaidi ya kuona picha, Mama ametulea tukasoma hadi Sasa na sisi Ni wazazi ila kuna muda nawaza hivi siku Mama akitutoka itakuaje nashindwa kuvumilia hilo wazo nalipotezea kabisa, poleni ndugu zangu mlioondokewa na wazazi.
 
Tutafute hela tule bata, huu uzi unaonesha jinsi gani watanzania tunaishi maisha mafupi mno, yani hapo naona hao wazazi 90% hawakufika miaka 50, noma sana
 
Kama ww n mwanaume n kukaza roho mkuu ...huwez badili kitu..mm nmefiwa na mama angu mwezi wa 6 mwaka huu nilipata taarifa asubuh nikiwa tayari naenda kazin tena n mbali na hakuna dereva n ww mwenyew ...IMAGINE NLIPGA KAZ HADI JION NKARUD ZEN NIKAWAAMBIWA WAFANYAKAZI WENZANGU kwamba maza gone!!! Ukizaliwa mwanaume tambua hutakiwi kutia huruma n kukubaliana na tukio lolote. .na katika maisha jiandae kuskia habar yoyote mbaya au zur...OVER
Mkuu mbona unaongea kigangster sana kufiwa na mama kusikie kwa wenzio haijalishi wewe ji mwanaume wau mwanamke utalia tu hata uwe kauzu kiasi gani hakuna namna
 
siku mdogo wangu alivyofariki ilinitia huzuni na simanzi sana[emoji24][emoji24].....maadui zangu walitaka kuutumia huo msiba kunimaliza kabisa....kwa sababu kama nisingekaza ningeathirika kisaikorojia ila hilo nililitambua mapemaaa....nilisimama imara kama nilivyosimama imara kipindi cha mwendazake...mwendazake alikuwa amepania kutupoteza kabisa kwenye ramani sisi wasomi watoto wa wakulima tusiokuwa na connection....alitaka wengi wetu tuishie kufanya kazi za hovyoo....alitaka nyuso zetu zipoteze nuru kwa sababu ya kukosa matumaini ya maisha yetu ya baadae.......lakini mungu aliamua kusimama nasisi[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22] .....wasomi wote tusiokuwa na connection tupo imara mpaka leo mikono juuuuuuuuuuuuuuuuuu.......mwamba wa miamba wote mikono juuuuu....[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Heeeee[emoji134][emoji849][emoji849][emoji849]

Mwendazake vs mdogo wako[emoji848][emoji848]
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Ni jambo zito sana!
Ila kwa mtu wa chini ya miaka kumi na nane ni balaa zito
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Ukijizuia kulia hutapona!!lia utoe uchungu ndugu!
Pole Sana kwa msiba huo mzito!

Umenikumbusha mama yangu alifariki nikiwa chuo mwaka wa tatu tukiwa kwenye mitihani ya semester ya mwisho,nilijikaza sikulia,kilichofuatia wiki moja mbele nilianza kulia,pona yangu ilikuwa ni kuhama nyumbani,lakini mpaka leo nikifika nyumbani lazima machozi yananilengalenga.
Lazima utalia tu sababu mtu unayetegemea kwenda kumuona hayupo basi unajikuta mnyonge tu.
Vipi mzee bado yupo?
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Pole dogo
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Dah sasa ambao mama zetu walitangulia tukiwa na 3yrs tukoment wapi jmni

ukiona lako zito ujue kwa jirani ni zito zaidi
Kitu nilichogundua maumivu ya kutiwa ukiwa mtoto mdogo ni tofauti na ukiwa mtu mzima. Ingawa yote ni maumivu.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Pole Sana Tena saana maana najua machungu unaenda nyumban hayupo unazunguka nyumba haumuon Ni kipindi kigum Sana na kunahitaj uvumiluvu was Hari ya juu Sana ,
Mimi baba mpendwa kafariki 2006 ,Mama mpendwa 2019 ndapambana hivyo hivyo changamoto kibao mpka muda mwingine nasema wazaz wangekuwepo wangenisaidia lakin wapi!!
Nakimbia naenda home likizo daaa kukimyaaa naona makaburi Yao migombani .
Vumilia na mm nishavumilia lakin picha hainitok I'la God is good.
 
Ni kipindi kigumu kwakweli, asikwambie mtu ambaye bado hajafikwa na hili. Nilifiwa na mama mzazi 2018 , alikuwa na 50+ years, roho iliniuma mno natamani angekuwepo aone juhudi za mwanaye ninavyopigana kimaisha, lakini basi . Allah amrehemu kwenye maisha ya kaburi . Kijiji kilitikisika kwa msiba huu mzito, mana mama angu alikuwa ni mtu wa watu.
 
I don't like hizi mada kabisaaaaaaaaaaa
Nimejaribu kupotezea Ila wapi.
Any way mama alivyofariki walidhani sitoweza kuhimili hiyo hali au hiyo taarifa. Walidhani ningeweza kujidhuru mwili au roho yangu.

Ndugu hawakutaka nitoke au niwe mbali na macho yao. I destroyed relationships, friendship, nimegombana na ndugu na jamaa. Kuna ndugu wengine hatujakaa sawa kwa maneno tuliyosemeshana. Si kosa lao wao hawajui how the funeral took me.

What helped me ilikuwa kwenda mbali na home. It took me almost 8 months to come to normal l. I acted very normal outside ila ndani maumivu si ya kitoto.

Nakumbuka niliwai kulia mara moja msibani. Ila ktk msiba wa mama nimelia mara elfu.

Ndoto, mawazo, ukirudia au kukumbuka vitu mlivyoongea au kufanya pamoja, mipango, mada kama hizi na kadharika.

Hakuna experience mbaya kama kufariki kwa mpendwa wako ambaye yupo peke yake ktk hiyo nafasi.
 
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Ukikua utamove on. Subiri.
 
Lazima utalia tu sababu mtu unayetegemea kwenda kumuona hayupo basi unajikuta mnyonge tu.
Vipi mzee bado yupo?
Mzee yupo mkuu,he is approaching to 70yrs,lakini kawa mtu wa pombe Sana,ameoa MWANAMKE waliyekutana naye kwenye vinywaji,alikuwa mjane wa watoto watatu!

Mi namlea mzee but naye anailea hiyo family aliyoikuta na maisha yanasonga,najitahidi kuilinda furaha yake,nahofia nisije nkampoteza naye mapema,
Life is a circle.
 
Safi mzee, endelea kumtunza dingi
 
Back
Top Bottom