Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

Walimu wengi ni masikini tena wanadharaulika kwasababu ni wachafu hawajipendi, hawavai nguo Safi kila siku nguo hiyo hiyo kauka nikuvae, wake zao ni Walevi wa pombe za kienyeji... Ndio maana wanawake wengi hukataa kuolewa na mwalimu. Mtu akishajua wewe ni mwalimu basi anakushusha heshima na unadharaulika mpaka na watoto wadogo maana wanajua wewe ni fukara tu Wali maharage.
 
Ndomana nilishauligi kuwa walimu waanze kupigwa oral na written interview, shida tunawadekeza sana hawa inabidi tukutane nao ajira portal waone hiyo compitition ilivyo. Unakuta mwalimu yupo yupo tu kama waokota makopo. Nikiendaga shuleni kumsalimia dogo wangu unakuta naongea na mwalimu hajiamini anatetemeka tu nguo hawapigi pasi wala hawapo smart kama majaa yaliyopo TRA, TCRA, TPDC, BANK au NSSF
 
Kwanza mwaka juzi Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Wizarani alisema Waalimu ni miongoni mwa kada ya watumishi wenye mishahara mikubwa serikalini..

Sijawahi watetea Waalimu Wala hawajawahi kuwa wanyonge.
 
Syo kweli! wewe ni mhanga wa taarifa potofu kuhusu walimu! Usichukue extreme case ya mwalimu mmoja ambaye hayuko vizuri halafu ukafanya ndivyo walimu wote walivyo. Mwalimu siyo fukara maana haidiwi mshahara na watumishi wengine walio wengi. Hata kada zingine walevi wapo tu. ulevi ni tabia ya mtu bila kujali taaluma au kada yake!! Soma post yangu #1.
Mimi binafsi sijawahi kutoka shule ya msingi hadi masters sijawahi kufundishwa na mwalimu mchafu na mlevi kama unaowasimulia wewe! Sisemi kama hawapo wa hivyo lakini hiyo haihusiani na ualimu wao, ni tabia yao tu hao uliowaona wewe. Hao unaowasema wewe hata kama wangekuwa na kazi zingine wangekuwa walevi tu kwa tabia yao.
 

Trafiki?
 
🤣🤣🤣🤣
 
Kada ya afya sijaiweka kwenye mlinganisho! UJue wanapiga kitabu miaka 4 hao wauguzi kwa diploma na wanaitwa STAFF NURSE. Hata hivyo hiyo data yako sijui kama ndiyo mshahara wa kuanzia!!
ni miaka mitatu tena alietokea kidato cha nne mwenye D nne masomo ya sayansi
 
Kwa maelezo haya ni wazi mkuu una kitengo nyeti kwenye nchi hii nimekutumia CV zangu DM unipe japo kaconnection na Mimi.
 
Dah umetisha,,,nilizoea kukuona kuleeee mkiparurana na mk254 na Annunaki[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mambo ya mishahara hayana uhusiano na kudharaulika kwa kazi ya ualimu. Dunia nzima kazi ya ualimu inadharaulika licha ya kwamba ni miongoni mwa proffesional nne kongwe zaidi duniani ambazo ni Elimu, Tiba, Sheria na uhandisi. Kuna tafiti zimefanyika juu ya hili na haya ndio yalikuwa ndio baadhi sababu ya kudharaulika kwa hii kada.

1. Idadi

Kada ya elimu ndio kada yenye watumishi wengi kuliko kada zote duniani. Hii ni kawaida kitu kikiwa na watu wengi kinaonekana cha kawaida hakina upekee.

2. Aina ya client inayodeal nao

Kada ya ualimu kwa kiasi kikubwa inadeal na watoto na vijana wadogo ambao hawajapevuka kiakili. Hii mambo imepelekea jamii kuona kama ni kazi ya kitoto-toto. Haigusi moja kwa moja shida na maslahi ya watu wazima ukilinganisha na kada zingine.

3. Mazingira ya kufanyia kazi

Kazi ya ualimu ina mazingira magumu ya kufanyia kazi ukilinganisha na kada zingine dunia nzima. Kada zingine mtu anaweza kulipwa mshahara mdogo lakini yuko kwenye ofisi nzuri na usafiri wa heshima kutoka ofisi husika. Hii inapandisha hadhi ya mtu automatically.

Lakini yote kwa yote hii ni kada mama Kati ya nada zote. Ni ngumu kada hii kupata heshima lakini mchango wake ni mkubwa pengine kuliko kada zote.
 
Mkuu research unayo lakini ? Sinjui Kama unachosema hapa kina uhalisia even 16% ? Hizo posho na overtime za 900000 kwa mwezi Sijui ni kwa fani ngapi. Amini wengi wanaolalama huku sio walimu tu zipo na fani nyingine nyingi zinazolalama hasa wale wasio ngazi za halmashari Kama vile katani, na vijijini, Sema tu kwenye utumishi wa serikali mwalimu ndio rahisi kumwongelea zaidi.

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
 
kingine wanagombania kazi za sensa na wanafunzi wao
 
Uko sahihi kabisa
 

Huu ndo ukweli bila haya makandokando ni ngumu sana mtumishi wa umma kutoboa.! Na serikali isopo boresha masilahi ya watumishi kamwe rushwa haiwezi kuisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…