Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

Walimu Hawana dili Wala marupurupu ya ziada Kama kada nyingine, hiki Ndo kinawafanya kua maskini Sana

1. Dreva wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu ila atapiga dili za vifusi,mchanga,kokoto n.k night za misafara n.k

2. Afisa biashara au ardhi wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu,
Ila atapiga rushwa za leseni za kufa mtu.

3. Afisa mifugo au kilimo atapiga elfu tano tano za sindano mifugo ya watu au atalima mashamba yake uko uchochoroni kwa kutumia dawa au pembejeo za ruzuku za serikali.

4. Mfamasia atakula laki tano tano kila mwezi for free za cheti chake tu kutumika kwny maduka ya dawa ya watu uko mitaani uku katulia tu..

5. Daktar au nesi wa halmashaur,
Hawa dili za semina,mafunzo n.k Ni nyingi mno(covid 19, chanjo, ukoma, malelia n.k). Hapo bado hawajaiba vifaa Tiba na kuviingiza mtaani kwenye hospital binafs.
[emoji117] Kuna na mabwana afya kaam matrafiki TU, wanatupiga Sana elfu hamsin hamsi Za faini uku mitaani

6. Wahasibu na maafisa manunuzi wa halmashaur wanapiga Sana dili za kimahesabu na 10% wakishirikiana na maboss wao (wakurugenz) ili Kupiga Cha juu kwenye tenda na matumiz mbalimbali ya fedha kwny halmashaur.

7. Maengineer wa halmashaur Ndo kabsaa wezi wakubwa, wao kila mradi wa serikali wakipewa kusimamia Lazima umalizike na yeye tayar ana kijumba keshakijenga kwa material zile zile za mradi.

8. Maafisa masjala wao Ni Kama matrafiki au madalali wa viunga vya halmashaur, una faili lako pale kwa mkurugenz au mkuu wa wilaya,ili likimbie chap chap Lazima utamwachia elfu 2 au elfu 5 ya maji.

9. Afisa maliasili wa halmashaur Hawa Ni wazee wa madili na rushwa za misitu,mikaa,mbao na magendo mbalimbali ya serikali.

10. Afisa utumiishi Hawa ndio wazee wa madili ya watumishi hewa.
[emoji117]Mtu anafariki, ripoti haiendi hazina kusitisha mshahara. Inatolewa ripoti ya mwajiriwa kubadili account yake, mshahara wa marahemu wanaula hata miaka 10 mfulurizo bila yeyote kujua.
[emoji117]mtu anamakosa ya kinidhamu,kasimamishiwa mshahara. Ripoti haiendi hazina, inabadilishwa tu account. Wanaupiga kimya kimya. Ukisamehewa ukarudishiwa mshahara, ule wa nyuma hata uulizii.
[emoji117]mtu anaripoti Ila haendi kituo Cha KAZI, au anaacha kazi anaenda zake private kwa muda.
wanakula dili na afisa utumishi, wanaugawana nusu nusu huku yeye Yuko zake private sector anapiga Ela nyingine.

Kama Kuna mtumish mwngne wa halmashaur nmemsahau nikumbushe.

Ila kiuhaisia mwalimu nje ya mshahara sijui atapiga dili gani atoboe,

ukiachilia mbali suala la twisheni ambalo bado kipato chenyewe Ni kidg mno na jasho linalomtoka Ni jingi mno

Sijui atapiga dili gan jingine maana vitabu vyote vya serikali vimeandikwa "HAKIUZWI", boksi lenyewe la chaki Mtaani halizidi hata elfu 2.
Kama ni kweli haya uliyosema, basi ni rahisi kwa ngamia kupenya tundu la sindano kuliko mtu kuingia ufalme wa mbiniguni!
 
sijaona hapa sababu ya yeye(mwalimu) asipiganie fursa ya kumuongezea kipato kisa Ana mshahara mzuri na Hali ya kuwa hakuna wafanyaji wa hyo kazi..Tajiri haidharau shilingi hamsini!!
 
Mwalimu mwenye degree Basic yake ni 771,000/=..? Kwan Askar Jesh au Polisi mwenye degree nae analipwa sh ngap nliwahi sikia wao wana mishahara miwili na katikat ya mwez wanalipwa
Hahaaa akili za wabongo eti wana mishahara miwili, wale wana allowance laki 3
 
Huu upuuzi sijui tutauacha lini? Kama mtumishi wa umma unayefahamu mfumo wetu wa ajira za serikali utagundua kuwa Mwalimu anatofautiana kidogo sana na watumishi wa kada zingine .

Hizi ni tofauti chache sana.

1. Posho. Mwalimu hana posho ila kada zingine wanazo

2.Mianya ya rushwa. Hakika mashuleni rushwa ni ngumu sana kupatikana labda kwa mkuu wa shule.

Hizi tofauti mbili ndizo zinazomfanya Mwalimu aonekane ana njaa sana hasa tarehe za katikati.

OMBI KWA WALIMU

Wawekeze zaidi katika professionalism na hii sababu ndiyo inayowaumiza sana. Walimu wengi ni Incompentent , unskilled not well developed. Hawawezi hata kujibu hoja tu za kiutumishi . Mfano ukiomba barua zilizoandikwa na walimu kwa mikono yao[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Aisee utacheka . Kujielezea ni sifurii.
Swala la kujieleza halina uhusiano na ualimu ni suala la mtu binafsi, kuna mainjinia madokta, nesi, afsa ugani wana tatizo hilo
 
Walimu wengi ni masikini tena wanadharaulika kwasababu ni wachafu hawajipendi, hawavai nguo Safi kila siku nguo hiyo hiyo kauka nikuvae, wake zao ni Walevi wa pombe za kienyeji... Ndio maana wanawake wengi hukataa kuolewa na mwalimu. Mtu akishajua wewe ni mwalimu basi anakushusha heshima na unadharaulika mpaka na watoto wadogo maana wanajua wewe ni fukara tu Wali maharage.
Hivi wauza karanga,wauza maji, madobi, wafagia barabara, mafundi nguo, mafundi baiskeli, machinga wanamaisha mazuri kuliko walimu
 
Mambo ya mishahara hayana uhusiano na kudharaulika kwa kazi ya ualimu. Dunia nzima kazi ya ualimu inadharaulika licha ya kwamba ni miongoni mwa proffesional nne kongwe zaidi duniani ambazo ni Elimu, Tiba, Sheria na uhandisi. Kuna tafiti zimefanyika juu ya hili na haya ndio yalikuwa ndio baadhi sababu ya kudharaulika kwa hii kada.

1. Idadi

Kada ya elimu ndio kada yenye watumishi wengi kuliko kada zote duniani. Hii ni kawaida kitu kikiwa na watu wengi kinaonekana cha kawaida hakina upekee.

2. Aina ya client inayodeal nao

Kada ya ualimu kwa kiasi kikubwa inadeal na watoto na vijana wadogo ambao hawajapevuka kiakili. Hii mambo imepelekea jamii kuona kama ni kazi ya kitoto-toto. Haigusi moja kwa moja shida na maslahi ya watu wazima ukilinganisha na kada zingine.

3. Mazingira ya kufanyia kazi

Kazi ya ualimu ina mazingira magumu ya kufanyia kazi ukilinganisha na kada zingine dunia nzima. Kada zingine mtu anaweza kulipwa mshahara mdogo lakini yuko kwenye ofisi nzuri na usafiri wa heshima kutoka ofisi husika. Hii inapandisha hadhi ya mtu automatically.

Lakini yote kwa yote hii ni kada mama Kati ya nada zote. Ni ngumu kada hii kupata heshima lakini mchango wake ni mkubwa pengine kuliko kada zote.
Hahaaaa uko kijiji gani eti dunia nzima kada ya ualimu inadharaulika, nchi nyingi zilizoendelea ualimu ni miongoni mwa kada zinazolipa zaidi
 
Ndomana nilishauligi kuwa walimu waanze kupigwa oral na written interview, shida tunawadekeza sana hawa inabidi tukutane nao ajira portal waone hiyo compitition ilivyo. Unakuta mwalimu yupo yupo tu kama waokota makopo. Nikiendaga shuleni kumsalimia dogo wangu unakuta naongea na mwalimu hajiamini anatetemeka tu nguo hawapigi pasi wala hawapo smart kama majaa yaliyopo TRA, TCRA, TPDC, BANK au NSSF
Weye unayelala sebuleni kwa dada yako,unathubutu kumkandia Mwalimu aliyekufundisha kuandika na kuhesabu!
 
Kwa mwanajeshi sina uhakika, lakini kwa polisi wanapigwa gepu na walimu!! Halafu kupanda cheo kwenye upolisi ni ngumu sana!!Kwa zamani ukijiunga polisi na digrii autoimatically unakuwa afisa muda mfupi, lakini siyo leo!! Unabaki private na digrii yako hadi miaka ya kueleweka!! Hizo ndizo kazi zinazotegemea kipato ambacho si rahisi kukielezea kimaadili! rushwa, uonevu nk!1
Hamna gepu lolote unalipwa kwa cheo kama ni koplo au constable hana elimu yeyote hapo sawa umemzidi kwanzia tu ukiwa sajenti hata hauna nyota bado mshara ni mzuri unakula kilo saba bado posho zao zile lakitatu na ukiwa na elimu unalipwa ujuzi wako

Unataka useme mwalimu analingana na sp au ssp utachekwa[emoji3]

Wanachozingua hawa watu ni wanawake na pombe tu ndio maana wanakuwa hawana hela
 
Waliokuwa na akili kama zako saa hii wanasota!! Mfano wa karibu ni Sabaya!
Hili na Sabaya nalo ni mada nyingine mkuu.

Ninamsifu kuwa ana uwezo mkubwa sana wa kuhimili vishindo, ingawa kakonda kaisha.

Kila nimuonapo akishushwa kwenye karandinga bado ana ari na nguvu ya kuweza kuwapungia mikono ya heri hadhira pamoja na wapenzi wake.

Kwa mwimgine hapo, angelikuwa keshapoteza uelekeo tayari.
 
Walimu wakitaka wathaminiwe na selikari ijali maslahi yao,
just simple, walimu wote wasiombe kazi za muda uchaguzi mkuu 2025.

Selikari haiwezi kuwabana majobless eti waibe kura fisiemu iibuke kidedea.

Walimu wote kuacha kuomba kazi za muda uchaguzi mkuu 2025 Hilo haliwezekani kila mtu anajua.
Hiyo ndiyo sababu ya sekta yao kukosa posho kama sekta nyingine?
 
Jamii ya watanzania wanavyoelewa ni kwamba kazi ya ualimu ndiyo yenye mshahara mdogo kuliko kazi zingine zote. Hivyo hii imepelekea hadhi ya mwalimu kwenye jamii kushuka sana na mwalimu kuhesabika kuwa ni duni katika jamii. Lakini hii si kweli hata kidogo. Msichana akitaka kuchumbiwa na mwalimu anajisikia mnyonge, na mara nyingi hukataa labda akihisi kuwa umri unamtupa mkono au akiona hajapata chaguo la moyo wake.

Ukweli ni kwamba watumishi wote wa serikali (walimu na kada zingine) mishahara yao iko chini sana! Lakini ukiilinganisha hiyo mishahara yao midogo, mshahara wa mwalimu unakuwa juu kidogo kuliko kada zingine isipokuwa kwa kada ambazo wanasoma miaka mingi zaidi kama madaktari, wafamasia na wahandisi.

Ngoja niwaanikie hapa:

Mishahara ya walimu wanaoanza wenye digrii ya kwanza:
Hadi Juni 2022 walikuwa kwenye TGTS D1 = 716,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGTS D1 = 771,000/=

Mishahara ya kada zingine wasio walimu wenye digrii ya kwanza:
Hadi June 2022 walikuwa kwenye TGS D1 = 710,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGS D1 = 765,000/=

Kwa hiyo hadi Juni 2022 mshahara wa mwalimu ulikuwa unazidi mshahara wa kada nyingine kwa sh 6,000/=.
Kuanzia Julai 2022 mshahara waq mwalimu unazidi mshahara wa kada zingine kwa sh 6,000/= pia.

Kwa wastani mishahara ni midogo kwa wote japo jamii inaamini kuwa mwalimu ndiye mwenye mshahara mdogo wakati siyo kweli. Wahanga wa uongo huu wamekuwa ni wasichana kukataa kuolewa na walimu na kushobokea kada zingine kwa kigezo cha mshahara.

Mtumishi wa serikali akilalamika kuwa mshahara ni mdogo watu wanakimbilia kusema kuwa huyo lazima atakuwa ni mwalimu.

Nashauri tuwaheshimu sana walimu wetu, tusiwabeze bali tuwatie moyo maana kazi yao ni ngumu na ni muhimu sana. Kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni kukejeli walimu eti ndio wanaolalamikia nyongeza kiduchu ya mshahara mwaka huu kinyume na matarajio yao.
Hela ndogo sana hyo.bado makato ya Kodi na nssf.
 
Watumishi wengine wanalipwa overtime kwa siku 15 kwa mwezi ambazo hazikatwi kodi , kwa rate ya sasa 60,000 × 15 = 900,000
Analipwa posho ys vikao na kazi, kupitia madokezo,
Mealimu ukitoa mshahara hana chochote kingine anachotegemea,akiukopea mshahara ndo kabisaaaaa utamuonea huruma!

Watu wasichotaka kukubali ni kwamba nje ya salary mwalimu hana issue.
Kada zingine kuna madokezo, overtime, vikao, semina n.k

Mwalimu hana yote hayo hata akipata safari ya nje ya wilaya wanamuonea sana anaweza kulipwa 30K wakati rate ya DSA yake inaweza kuwa 100K.

Kuna mambo ya hovyo sana walimu wanaonewa na maskini ya Mungu walimu wamekuwa ni kundi linaloonewa sana na Serikali, kukiwa na mwenge lazima wachange lazima waende kukesha pia
 
Walimu Hawana dili Wala marupurupu ya ziada Kama kada nyingine, hiki Ndo kinawafanya kua maskini Sana

1. Dreva wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu ila atapiga dili za vifusi,mchanga,kokoto n.k night za misafara n.k

2. Afisa biashara au ardhi wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu,
Ila atapiga rushwa za leseni za kufa mtu.

3. Afisa mifugo au kilimo atapiga elfu tano tano za sindano mifugo ya watu au atalima mashamba yake uko uchochoroni kwa kutumia dawa au pembejeo za ruzuku za serikali.

4. Mfamasia atakula laki tano tano kila mwezi for free za cheti chake tu kutumika kwny maduka ya dawa ya watu uko mitaani uku katulia tu..

5. Daktar au nesi wa halmashaur,
Hawa dili za semina,mafunzo n.k Ni nyingi mno(covid 19, chanjo, ukoma, malelia n.k). Hapo bado hawajaiba vifaa Tiba na kuviingiza mtaani kwenye hospital binafs.
[emoji117] Kuna na mabwana afya kaam matrafiki TU, wanatupiga Sana elfu hamsin hamsi Za faini uku mitaani

6. Wahasibu na maafisa manunuzi wa halmashaur wanapiga Sana dili za kimahesabu na 10% wakishirikiana na maboss wao (wakurugenz) ili Kupiga Cha juu kwenye tenda na matumiz mbalimbali ya fedha kwny halmashaur.

7. Maengineer wa halmashaur Ndo kabsaa wezi wakubwa, wao kila mradi wa serikali wakipewa kusimamia Lazima umalizike na yeye tayar ana kijumba keshakijenga kwa material zile zile za mradi.

8. Maafisa masjala wao Ni Kama matrafiki au madalali wa viunga vya halmashaur, una faili lako pale kwa mkurugenz au mkuu wa wilaya,ili likimbie chap chap Lazima utamwachia elfu 2 au elfu 5 ya maji.

9. Afisa maliasili wa halmashaur Hawa Ni wazee wa madili na rushwa za misitu,mikaa,mbao na magendo mbalimbali ya serikali.

10. Afisa utumiishi Hawa ndio wazee wa madili ya watumishi hewa.
[emoji117]Mtu anafariki, ripoti haiendi hazina kusitisha mshahara. Inatolewa ripoti ya mwajiriwa kubadili account yake, mshahara wa marahemu wanaula hata miaka 10 mfulurizo bila yeyote kujua.
[emoji117]mtu anamakosa ya kinidhamu,kasimamishiwa mshahara. Ripoti haiendi hazina, inabadilishwa tu account. Wanaupiga kimya kimya. Ukisamehewa ukarudishiwa mshahara, ule wa nyuma hata uulizii.
[emoji117]mtu anaripoti Ila haendi kituo Cha KAZI, au anaacha kazi anaenda zake private kwa muda.
wanakula dili na afisa utumishi, wanaugawana nusu nusu huku yeye Yuko zake private sector anapiga Ela nyingine.

Kama Kuna mtumish mwngne wa halmashaur nmemsahau nikumbushe.

Ila kiuhaisia mwalimu nje ya mshahara sijui atapiga dili gani atoboe,

ukiachilia mbali suala la twisheni ambalo bado kipato chenyewe Ni kidg mno na jasho linalomtoka Ni jingi mno

Sijui atapiga dili gan jingine maana vitabu vyote vya serikali vimeandikwa "HAKIUZWI", boksi lenyewe la chaki Mtaani halizidi hata elfu 2.
Umeuwa, harudi tena huyo mwalimu
 
Jamii ya watanzania wanavyoelewa ni kwamba kazi ya ualimu ndiyo yenye mshahara mdogo kuliko kazi zingine zote. Hivyo hii imepelekea hadhi ya mwalimu kwenye jamii kushuka sana na mwalimu kuhesabika kuwa ni duni katika jamii. Lakini hii si kweli hata kidogo. Msichana akitaka kuchumbiwa na mwalimu anajisikia mnyonge, na mara nyingi hukataa labda akihisi kuwa umri unamtupa mkono au akiona hajapata chaguo la moyo wake.

Ukweli ni kwamba watumishi wote wa serikali (walimu na kada zingine) mishahara yao iko chini sana! Lakini ukiilinganisha hiyo mishahara yao midogo, mshahara wa mwalimu unakuwa juu kidogo kuliko kada zingine isipokuwa kwa kada ambazo wanasoma miaka mingi zaidi kama madaktari, wafamasia na wahandisi.

Ngoja niwaanikie hapa:

Mishahara ya walimu wanaoanza wenye digrii ya kwanza:
Hadi Juni 2022 walikuwa kwenye TGTS D1 = 716,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGTS D1 = 771,000/=

Mishahara ya kada zingine wasio walimu wenye digrii ya kwanza:
Hadi June 2022 walikuwa kwenye TGS D1 = 710,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGS D1 = 765,000/=

Kwa hiyo hadi Juni 2022 mshahara wa mwalimu ulikuwa unazidi mshahara wa kada nyingine kwa sh 6,000/=.
Kuanzia Julai 2022 mshahara waq mwalimu unazidi mshahara wa kada zingine kwa sh 6,000/= pia.

Kwa wastani mishahara ni midogo kwa wote japo jamii inaamini kuwa mwalimu ndiye mwenye mshahara mdogo wakati siyo kweli. Wahanga wa uongo huu wamekuwa ni wasichana kukataa kuolewa na walimu na kushobokea kada zingine kwa kigezo cha mshahara.

Mtumishi wa serikali akilalamika kuwa mshahara ni mdogo watu wanakimbilia kusema kuwa huyo lazima atakuwa ni mwalimu.

Nashauri tuwaheshimu sana walimu wetu, tusiwabeze bali tuwatie moyo maana kazi yao ni ngumu na ni muhimu sana. Kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni kukejeli walimu eti ndio wanaolalamikia nyongeza kiduchu ya mshahara mwaka huu kinyume na matarajio yao.
Ualimu sio kazi ngumu ya kumlipa hela nyingi, wanakula bata sana hawa...
Diploma kwetu wanalipa 1,000,000 dgree 1,355,000 hiyo ni basics...
Sasa degree ya mwl.ni 710,000/= take home bei gani kama hiyo ni basics..
Hawana kazi ngumu, kufundisha tu watoto na hawana side effects za kazi afu unataka hela nyingi
 
Hamna gepu lolote unalipwa kwa cheo kama ni koplo au constable hana elimu yeyote hapo sawa umemzidi kwanzia tu ukiwa sajenti hata hauna nyota bado mshara ni mzuri unakula kilo saba bado posho zao zile lakitatu na ukiwa na elimu unalipwa ujuzi wako

Unataka useme mwalimu analingana na sp au ssp utachekwa[emoji3]

Wanachozingua hawa watu ni wanawake na pombe tu ndio maana wanakuwa hawana hela
kwa hiyo huyo SP ndio umeona ana salary kubwa? hivi unajua Fresh CPA anayeanza kazi eGA anaweza kuwalipa hao SP hata mara 3 au nne,
-vitengo vyenye salary kubwa ni eGA,TCRA,TANAPA,LATRA,ⓣⓡⓐ
 
Hapa tunazungumzia walimu mbona unajichanganya unaenda o.p soma juu huyo niliye mquote reply yake utaelewa jibu langu
 
Ualimu sio kazi ngumu ya kumlipa hela nyingi, wanakula bata sana hawa...
Diploma kwetu wanalipa 1,000,000 dgree 1,355,000 hiyo ni basics...
Sasa degree ya mwl.ni 710,000/= take home bei gani kama hiyo ni basics..
Hawana kazi ngumu, kufundisha tu watoto na hawana side effects za kazi afu unataka hela nyingi
Hapa umenena.Lakini kimbuka wao hawana side effect(s) ila ikitokea ktk utendaji wao wa kazi wakafanya chini ya kiwango basi madhala yake ni makubwa.Kwa maoni yangu hizi posho zitolewe bila ubaguzi kwa kada zote!
 
Back
Top Bottom