Mliokasirishwa kuhusu Rais Samia kutoa msaada Uturuki hii sio awamu ya Magufuli

Billion 2 si ni 0.001 ya makusanyo ya ndani hivi kweli inahitaji kukopwa hiyo?
Punguzeni chuki sukuma gang
Pesa za Umma ziheshimiwe. Kila siku mnatembeza bakuli, mkizipata mnaziiba na kuzitapanya kama karanga!!!!

Kuna Watu wanalala njaa, Leo wasikize Serikali inasaidia matajiri wataelewa nn!!!
 
Maafa kama haya yametokea katika Syria, Pakistan na Afghanistan Je tumewasaidia?
 
Malawi ni Nchi MASKINI, Turkey ni MATAJIRI, tumetoa mahindi Malawi, bt uturuki tumepeleka pesa.

Bunge lingeidhinisha msaada wa chakula kama Malawi tulivyofanya na kupeleka wanajeshi kusaidia kuliko pesa.

Uturukio imepata majanga lini na sisi tumetoa msaada lini ndo utajiua Si msaada ni SADAKA.
 
Ina maana siku hizi Chadema sio wamepumzika kupinga na kukosoa na kuwaachia sukuma gang? Maana kila anayekosoa ni sukuma gang tofauti na mwanzo ilikuwa chadema.
Tunakosoa sana tu unless hufuatilii thread zetu humu, tatizo ni Hawa sukuma gang wao wanapinga Kila kitu kisa tu aliyefanya sio JPM. Unadhani angetoa hizo pesa JPM asingesifiwa kuwa kavunja rekodi Tanzania kuwa donor country!?
 
Sasa wewe hiyo $1 millioni moja yako ina faida gani, bora ata wangeitoa kimya kuliko kututangazia maana ni kuchezea tu hela kwa nchi maskini
Hizo $1 million ndio zikikutana na za Nchi zingine zinapandisha total kuwa billions so every cent matters.

Kingine hakuna Hela imechezewa, msaada hutolewa sio kulingana na utajiri hii ni strategic pia. Kwani china wanavyotoa msaada kwetu huko kwao si ndio Moja ya nchi yenye payments ndogo zaidi kwa wafanyakazi!! Kwanini isi boost purchasing power ya raia wake ila isaidie Africa??

Jibu ni strategic reasons, unatoa msaada Ili uji position kama nchi inayoweza kuwa reliable kwenye crisis, nchi ambayo licha ya kwamba haina pesa ila ikiwezeshwa it can do more, inajenga picha ya kidiplomasia kwamba we care for our allies and so on. Sasa msaada wa aina hii hata siku tukipata shida watatusaidia mara 10 yake even if it means military support!!

Nakumbuka Turkey waliwahi tuma wanajeshi kupigana South Korea so hao Korea walipoona tetemeko walikua Moja ya nchi za kwanza kabisa kutuma askari wake kwenda kufanya rescue na ndege zilizosheheni misaada ya kibinadamu!!

Nashangaa mtu makini kama wewe huelewi basics za economic diplomacy!!
 
Pesa za Umma ziheshimiwe. Kila siku mnatembeza bakuli, mkizipata mnaziiba na kuzitapanya kama karanga!!!!

Kuna Watu wanalala njaa, Leo wasikize Serikali inasaidia matajiri wataelewa nn!!!
Wataelewa siku wakipata shida..... Mind you Nyerere aliwahi saidia nchi za Africa mpaka Biafra, Saharawi, sauzi, msumbiji, kwani tulikua matajiri??

Diplomasia ni akili kubwa sio utajiri.
 

Kwakifupi ni taila?
 
Kwanza hiyo pesa ya rambirambi katoa kwenye mfuko upi wa serikali bila idhini ya Bunge?


Katoa kwenye mfuko wa majanga uliopo chini ya ofisi ya waziri mkuu.
 
 
Tunakosoa sana tu unless hufuatilii thread zetu humu, tatizo ni Hawa sukuma gang wao wanapinga Kila kitu kisa tu aliyefanya sio JPM. Unadhani angetoa hizo pesa JPM asingesifiwa kuwa kavunja rekodi Tanzania kuwa donor country!?
Hilo la kupinga kila kitu tulizowea kusikia wakiambiwa chadema kuwa ndio wapingaji wa kila kitu tokea kipindi cha Kikwete huko ila sasa hivi Sukuma gang wanaonekana ni wapingaji wa kila kitu na sio chadema tena, yani kuna wakati hata wale chadema kabisa wanajikuta wanaitwa sukuma gang kwa sababu ya kukosoa baadhi ya mambo kama maridhiano.

Lakini pia hizo hela angetoa Magufuli nyie mngemkosoa kwa sababu hakuwa na jema kwenu.
 
Wanyamulenge mna roho mbaya sana

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Wakasirishwe Kwa Ajili ya Msaada ? Huo si utaahira Sasa.
 
Lakini pia hizo hela angetoa Magufuli nyie mngemkosoa kwa sababu hakuwa na jema kwenu.
Okay ila sukuma gang wangemsifia si ndio? Hapo hauoni unafiki wao??
Hilo la kupinga kila kitu tulizowea kusikia wakiambiwa chadema kuwa ndio wapingaji wa kila kitu tokea kipindi cha Kikwete
Waliokua wanasema Chadema wanapinga Kila kitu ni sukuma gang sio wananchi!! Maana upinzani obviously watapinga ujinga wa chama tawala it's not news.


yani kuna wakati hata wale chadema kabisa wanajikuta wanaitwa sukuma gang kwa sababu ya kukosoa baadhi ya mambo kama maridhiano.
Yes kama ambavyo hata sie Wana Chadema tukisifia tu zuri la Samia tunaambiwa tumelamba asali na kejeli kama hizo.

Nadhani hii perception ipo humu JF miaka yote.....ilikua ukimkosoa JPM unaitwa Chadema au Fisadi at the same time ukimsifia JPM utaitwa Sukuma gang!! It goes to show hatuna political tolerance ila Mama Samia anaturejesha kwenye mstari wa kukosoana hata kama upo chama kile kile (Refer Lema na Lissu kumpinga Mbowe) and kumsifia hata kama yupo chama kingine (Mbowe kumpongeza Samia).

Otherwise sukuma gang wanapinga sababu JPM sio RAIS
 
Kwani lilitokea Jana au juzi kwanza tulisha lisahau ndio nasikia msaada sikuzote zile mlikuwa wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…