Mlioko Dar naombeni muongozo. Maisha yakoje huko?

Utakachofaidi Ni starehe K kama zote niwewe tu na Mitungi.
Kama huwezi Biashara ni bora ubaki hukohuko usije kuteseka bure.
 
umeandika ukweli mtupu mkuu.
 
Af mkuu me form 4 nimemaliza kitamb
 
Mabibo nadhani saa hz ndo umeamka na jua hafifu hafifu ukishangaa kina mama koridoni wengine wapo karibu na mlango wa choo,

Huku choo kikiwa mlango ni wa bati au shuka na kina ngazi kama kizingiti Cha nyumba

Ooh huku milio ya bodaboda nayo siyo haba

Ghafla unakaa umeme umekata ni zamu ya zuuuh na alitoka toka alfajiri tutakaa mpk usiku arudi jipange

Hujakaa sawa kina mama wachoma mihogo sambusa na kachori wengi wao maeneo hayo usoni wametumika na vikarolaiti vya hapa na pale akikukazia jicho,,

Haya na ugeni wako chooni hujaenda na maji unavamiwa na dada mpangaji wa hapo

Huku mtoto ama watoto wa hapo wakikuita anko na wewe ni chalamila

Nakuja mabibo hapo natokea karume jiandae
 
Raha ya Dar ni Black colored job.
Ukijipendekeza kwenye white colored job umekwisha.

Ni mji mzuri. Unafursa nyingi.
Hauhitaji uwe na aibu hii itakufanya usikushinde.
Hauhitaji uwe na tamaa. Ili usigeuzwe.

Maisha ni rahisi kama utakuwa na sehemu ya kukaa.
Tena kama unaishi Mabibo. Basi utaenjoy.

Changamoto za Dsm hasa huko uswahilini ni Uchafu na kunuka, joto kali ingawaje umekuja msimu wa baridi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…