Mliompiga risasi Lissu tambueni kuwa jinai haina mwisho. Kosa lenu lipo palepale

Mliompiga risasi Lissu tambueni kuwa jinai haina mwisho. Kosa lenu lipo palepale

Vilevile kwanini jeshi la POLISI halifanyi uchunguzi?

TL alipokuwa nchini alifika mpaka kwa RPC wa Dodoma kudai gari lake.

Kama victim yuko, na anazungumza, sielewi kwanini Polisi wameshindwa kumhoji.

Hakuna police force inayotumia gharama kubwa kuchunguza crime ambayo victim na eyewitnesses wake wako hai, lakini wamekimbia nchi. Kwa maneno mengine, ukitelekeza kesi yako yoyote (hata ya wizi) ndiyo basi tena!
 
Taratibu za kuhoji victim zinasemaje? Mpaka awepo nchini tu?
 
Mimi sina ujamaa na Lissu. Nasimamia misingi ya kisheria kuwa jinai haina mwisho. Ukifanya kosa leo utakamatwa hata baada ya miaka mia. Je waliompiga Lissu, jinai yao ina mwisho?

Jinai sio kumpiga mtu risasi kinyume cha sheria tu (hata wizi ni jinai)! Kama kumtangazia mwizi kuwa “jinai haina mwisho” kungekuwa na tija, wezi wangukuwa wameshaisha!
 
  • Thanks
Reactions: T11
Jinai sio kumpiga mtu risasi kinyume cha sheria tu (hata wizi ni jinai)! Kama kumtangazia mwizi kuwa “jinai haina mwisho” kungekuwa na tija, wezi wangukuwa wameshaisha!
Unanifundisha jinai ni kitu gani? Hapa tunatishia? Tunasema ukweli kuwa watu ambao walimpiga mtu risasi bila hatia kosa lao lipo palepale?
 
Taratibu za kuhoji victim zinasemaje? Mpaka awepo nchini tu?

Kuhoji victim aliyeko nje ya nchi kuna logistical issues. Kama victim ametelekeza case, obviously, investigators hawaingii gharama za ziada kuchunguza case yake. Hiyo ndiyo inaishia hapo. Hata kama ingekuwa imeshafika mahakamani, victim akiitelekeza itatupwa, kwa sababu victim (kama yuko hai) ni shahidi muhimu sana!
 
Kuhusu Lissu kutelekeza kesi nakukatalia. Yeye ni victim tu, Jamhuri ndio imefanyiwa kosa ilitakiwa ifanye juu chini waliohusika wakamatwe. Ila sababu jinai haina mwisho ipo siku watakamatwa.
 
Huu unyama bwana hauwezi ukawapa amani ya moyo wote waliopanga na kuutekeleza hata kama watafichwa.
 
Hivi ni visingizio tu.

Serikali ilimtengenezea passport mpya ili kumuwezesha Lissu kuondoka nchini.

Serikali inaweza kumtengenezea passport lakini haiwezi kumhoji kuhusu jaribio la kumuua?
 
Laana iwashukie wale wote waliohusika kwa namba moja au nyingine ili Lissu azurike au kufa kabisa.
Watanzania huwa hatuna tabia za kimyama kama hizi
 
Hakuna police force inayotumia gharama kubwa kuchunguza crime ambayo victim na eyewitnesses wake wako hai, lakini wamekimbia nchi. Kwa maneno mengine, ukitelekeza kesi yako yoyote (hata ya wizi) ndiyo basi tena!

Kumhoji Tundu Lissu na dereva wake kunahitaji gharama gani?

Hili suala Polisi wa Tz wanaweza hata kuomba msaada wa Interpol au Polisi wa Ubelgiji wawahoji victims.

Pia jaribio lile la mauaji sio " kesi " ya Tundu Lissu, ni " kesi " ya jamhuri.

Kwa kinachoendelea tunaweza kusema Jamhuri imetelekeza uchunguzi, na kesi.
 
Kuhusu Lissu kutelekeza kesi nakukatalia . Yeye ni victim tu, Jamhuri ndio imefanyiwa kosa ilitakiwa ifanye juu chini waliohusika wakamatwe. Ila sababu jinai haina mwisho ipo siku watakamatwa.

Huelewi unachoandika. Lissu na driver wake (ambao wote wako hai, lakini wamekimbia nchi) ndiyo spinal cord ya hiyo case. Wewe siku ukivamiwa (au ukiibiwa) peleka case yako police kisha uitelekeze uone itaishia wapi. Jamhuri haifanyi biashara ya kuendeleza cases ambazo victims wake wako hai lakini wamechagua kuzitelekeza. Victim angekuwa amekufa, hilo lingekuwa jambo jingine; investigation ingefanyika at any cost!
 
Ishu sio walio mpga shaba Lissu tu, hadi alie orcherstrate mpango mzima na alie to amri pia nadhani hadi waziri na wakuuu kwenye idara husika wanatakiwa kuwajibika hadi mkuu wa mkoa husika maana lile halikuwa jambo dogo lilishtusha taifa zaidi ya corona, ila pia hadi huku mitaani madiwani na wenyekiti waaeneo husika wana paswa kuwajibika pale matukio ya unyanyasaji yanapotokea na Waka yafumbia macho
Mimi sina ujamaa na Lissu. Nasimamia misingi ya kisheria kuwa jinai haina mwisho. Ukifanya kosa leo utakamatwa hata baada ya miaka mia. Je waliompiga Lissu, jinai yao ina mwisho?
 
Acha kutanga tanga kama mtoto. Umeanza kusema wametelekeza,sasa hivi hana ushiriano. Ushirikano upi ambao victim atautoa bila polisi kuanza wao kufanya uchunguzi? Aaanze kuwalazimisha kufanya uchunguzi?
 
Investigation haifanyiki kwenye vacuum. Kutokutoa ushirikiano wakati wa investigation ndiyo kutekeleza kwenyewe. Afadhali case ya wizi kwa sababu victim naye siyo eyewitness. Kwa case ya kushambuliwa, victim ni eyewitness. Kama yuko hai lakini ameshindwa kutoa ushirikiano unaohitajika, hiyo case lazima ifie kituo cha police.

Kwa hizi hoja zako unazozitoa, sidhani kama unaelewa uzito wa ushahidi wa victim kwenye case ya jinai! A victim makes or breaks the case! Actually, kwenye baadhi ya nchi, involvement ya victim kwenye criminal justice ni muhimu kiasi kwamba hata msamaha wa Rais hupewi kama victim hajaridhia!
 
Jikite kwenye mada, waliompiga Lissu risasi kosa lao lipo palepale. Maana unajaza pumba tu.

Kama ulifikiria mpaka ukafikia ukomo wako, kabla ya kuweka hili tangazo lako kwenye social media, basi ulikuwa unahitaji msaada wa kifikra, kwa sababu halina tija yoyote!
 
Siyo kweli. Wakati mwingine victims wanakuwa wamekufa lakini wachunguzi wanaendelea kutimiza wajibu wao.
 
Siyo kweli. Wakati mwingine victims wanakuwa wamekufa lakini wachunguzi wanaendelea kutimiza wajibu wao.

Approach ya kuchunguza case ya shambulio ambalo limemuacha victim akiwa hai haifanani na ile ya shambulio ambalo victim wake amekufa.

Kama victim yuko hai, hakuna investigation itakayofanyika bila input ya victim. Kama victim anataka case ifie kituo cha police aache kutoa ushirikiano unaohitajika.

Kama victim amekufa, hilo ni swala jingine; wapelelezi watajaribu kujenga na kutathimini theories mbalimbali kutoka vyanzo vyovyote (na wakati mwingine kwa gharama kubwa) ili kusolve hiyo crime.
 
..Polisi wa Tz hawataki kuchunguza jaribio la mauaji dhidi ya Tundu Lissu.

..Ukweli huo umejidhihirisha baada ya Lissu kuja nchini, na kufika ofisini kwa RPC Dodoma, lakini hakuhojiwa.
 
Back
Top Bottom