Mliowahi kudate na wazungu, nipeni muongozo

Mliowahi kudate na wazungu, nipeni muongozo

Kwani wazungu wote wako sawa?

Unanikumbusha siku moja nilikwenda ofisini kwa mshua nimempitia turudi home.

Nimefika pale nimekuta watu kibao wanasubiri kuonana naye.

Basi anakuja chumba cha kungojea, anawasalimia, anakutana nao ofisini kwake. Kwa hiyo anakuwa kashajua kuna nani na nani anasubiri kumuona.

Basi mara akaja mzungu mmoja. Sekretari akamfanya yule mzungu aliyekuja mwisho, awe ndiye mtu wa kwanza kuonana na mshua. Kwa sababu kamuona huyu mzungu.

Basi, mshua akaongea naye muda si mrefu, akamtoa.

Sasa mwisho kabisa, watu wameisha, mshua akawa anampa somo yule sekretari. Akamwambia, yule mzungu uliyemuwahisha kabla ya watu wote ni tapeli tu, hana deal lolote, hao watu weusi uliowaruka wengine wana ma deal makubwa sana. Usione mtu mzungu tu ukafikiri ni mfanyabiashara mkubwa kwa sababu ni mzungu tu.

Sasa naona hata mtoa mada anafikra zile zile za "wazungu wote wako sawa".

Wakati kuna wazungu wa aina tofauti tofauti sana.
Haya mataifa ya ulaya kidogo wamestaarabika, ukikutana na Warusi ni sawa na waswahili wa mbagala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ya wabongo wengi ubongo upande mmoja umejaa maji.

Kila mtu anawaza kukazana (Ng'ono),
umepata zari kama hili tumia hii nafasi kupata VISA na hata ikiwezekana hati ya ukazi ya nchi huyo dada anatokea

Kama anatoka umoja wa ulaya au USA anza kumchomekea na wewe uzame majuu. Connection za misafara serikali huna sasa unaenda nje lini??

Jitahidi upate VISA kipitia mgongo wa yuyo dada usepe zako majuu, huko ukiwa hata dereva wewe ni mtu mweingine

CCM hapa tanzania haina mpango wa kuachia madaraka
 
jaman T, kweli huu ni ushauri wako uliouona?
NIMEIFUTA ILE COMMENT YANGU.SIJUI NILIIANDIKA LINI NA NIKIWA NA HALI GANI?
YULE SIO MIMI TIMAMU KABISA.

DUNIA YA JF NAOMBA MNISAMEHE KWA UANDISHI ULE.
 
Haha!
Ila humu ndani ndio maana haitakiwi mfahamiane.
Nimewaza hii comment angeandika mtu nayemjua.. ningemvutia picha na kubaki kucheka sanaaa
NIMEIFUTA ILE COMMENT YANGU.SIJUI NILIIANDIKA LINI NA NIKIWA NA HALI GANI?
YULE SIO MIMI TIMAMU KABISA.

DUNIA YA JF NAOMBA MNISAMEHE KWA UANDISHI ULE.
 
Back
Top Bottom