Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Nataman sana ila mambo yameumana balaa. Budget kikomo. Nishasqueez to the last point

Na siwezi fika mwezi Feb bila kuwa sijapaua aisee

Hapo ada ya dogo inadai na huku nategemea chalii tena
Usiwe na papara kwenye upauji. Endelea kudunduliza uweke kitu cha ALAF. Baadae Unaweza kujikuta unajuta na kujilaumu kwa papara uliyoifanya
 
TBS wanatoa uthibitisho kwa kutumia vipimo vya maabara. Huko duniani ndio kuna ukweli wa namna gani bati ita-perfom. Watu wanaogopa hizi kampuni ndogo ndogo kwa sababu hazina muda mrefu kwenye soko. Utajuaje performance yake kwa hiyo miaka 10? Kuna mdau hapa amesema ametumia miaka 3 na hajaona shida, hii ni feedback nzuri, ila kuamini tu TBS unaweza ukalia baada ya muda.

Kuna maeneo chumvi ni nyingi, mengine tofauti ya joto usiku na mchana ni kubwa, sehemu nyingine kuna mvua za mawe; hayo mambo yote ni ngumu TBS kufanya vipimo.
 
Utatambuaje bati original ya ALAF..?
 
Mkuu, ni rangi gani ambayo sio rahisi kupauka tofauti na hizo rangi ulizo zitaja?
 
Utatambuaje bati original ya ALAF..?
Mkuu Mimi nimekuwa sales officer wa dragon na Sasa niko na Kinglion,Si sales wa ALAF ila Kwa uzoefu wangu wa mabati naweza kutambua bati original ya ALAF kwa kuzingatia vitu viwili;
1. Muhuri wa moto ule wa vinundu(sijakua kama nitakuwa sahihi) ila ni ule muhuri unaobonyeza bati kabisa.
2. Kwenye migongo mipana katikati ya migongo huwa na vibaraza vya kumwagia maji,Sasa kwenye vile vibaraza utaona Kuna vimistari vitatu.
Naruhusu kurekebishwa pale nilipokosea.
 
Kiwanda kama alaf au sunshire kinakufaje kizembe mkuu?
Achana na huzo story.

Kaa na hela yako. Badae unaweza badili mawazo au unaweza pata shida kubwa ya kifamilia ukaitumia hiyo hela.
 
Hizi ni materials ambazo baadhi ya makampuni tunaita matte wengine wanaita royal ila Kwa kiswahili tunaita mchanga mchanga/chengachenga.
Ni matirio mazuri Sana na bati yake Ina Bei kubwa kulinganisha na Bei ya bati la rangi mterezo
zinapendezesha sana paa
 
Shida inawahi kupata ukungu kama vigae nyumba inaonekana chafu kama vigae vya nyumba za Mbezi beach.
Old fashion, kitu msauzi Alaf utojutia kampuni zingine jiandae na kopo la rangi juu baada ya miaka 2.
 
Kitu low price kitakuaje quality sasa, ukiezeka umeezeka
 
Shida inawahi kupata ukungu kama vigae nyumba inaonekana chafu kama vigae vya nyumba za Mbezi beach.
Old fashion, kitu msauzi Alaf utojutia kampuni zingine jiandae na kopo la rangi juu baada ya miaka 2.
[emoji23][emoji23][emoji23]shida mfuko ndugu. Alaf ni mkasi kweli kweli
 
Hizi ni materials ambazo baadhi ya makampuni tunaita matte wengine wanaita royal ila Kwa kiswahili tunaita mchanga mchanga/chengachenga.
Ni matirio mazuri Sana na bati yake Ina Bei kubwa kulinganisha na Bei ya bati la rangi mterezo
Kuna sister napiga nae nyumba yake alipiga hii chenachenga ya C.gray toka dragon. Nyumba inawaka balaa. Since 2020 bado kanadunda fresssh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…