Mmeona sasa utofauti kati ya Uwajibikaji wa Wazungu na Waafrika? Kwetu Rais mpaka afie madarani vinginevyo hatoki!

Wazungu nchi zao zinaendelea kwasababu wanajielewa.linapokuja swala la uongozi na uwajibikaji wanafanya kwa maslahi ya nchi tofauti na afrika tunakofanya kwa maslahi ya matumbo yetu na yawajukuu zetu.
 
Umeanza vizurii mwishoni umeharisha Haya ya mwisho
 
Bado kuna tofauti kubwa kati ya waafrika na wazungu.mifano iko mingi duniani.ata huyo biden bado alikua na uamuzi wakwenda hadi kwenye sanduku la kura uchaguzi ukaamue.Kwa mwafrika hadi kifo kimuondoe au jeshi liingilie kati kama ilivyotokea kwa baadhi ya nchi za afrika magharibi.
 
Mtu mwenye miaka 76 hakutakiwa kuwa rais,ni kuyumba kwa dish la Biden kwenye mdahalo ndiyo kumemtoa,mnakuaje na rais hawezi nyoosha sentensi kisa dishi haliko sawa!!?
 
Kwahio Trump mpaka watu kuvamia Congress na mpaka leo kusema aliibiwa alibadilika kuwa Muafrika ?, Na mtu kama Nixon baada ya kufanya ndivyo sivyo na shinikizo kubwa ndio akajifanya kutoka. In short ni kwamba Biden Sponsors walianza kusema hawatatoa pesa kwahio there was no way out na Marekani Bila Pesa huchukui nchi (Wanaochagua ni Donors, Delegates ) sio kapuku anayeletewa choice ya kuchagua, Wanasiasa wote ni walewale
 
Huyo mzee anaetembea kama Robot
Halafu kakaa mda gani Uraisi?
Mzee anasahau na ana Covid pia
Mwacheni akaangaliwe hawezi kuendelea kuwa Rais
Labda useme wengine ila sio Biden
 
Mtu mwenye miaka 76 hakutakiwa kuwa rais,ni kuyumba kwa dish la Biden kwenye mdahalo ndiyo kumemtoa,mnakuaje na rais hawezi nyoosha sentensi kisa dishi haliko sawa!!?
Biden anamkaribisha Zelensky alafu anamuita Jina Putin na Nchi anampa Ukraine, Biden ni Yuniki Fulawa wa Marekani dish limeyumba
 
putin vipi ni mwafrika?
queen yule wa uingereza si kafia madarakani
yupo rais wa china nadhani naye wamemptisha afie madarakani
mzee wa kibwenzi
 
Kwani hujui maana ya Neno Uzungu, yani usmart, utulivu, unyoofu na sifa zingine ka hizo hata wewe ukipata pisi wife material unasema demu ni Mzungu yule.
 
Tofauti ninayoiona mimi ni unfair election.

Lakini kwenye chaguzi za haki hakuna nchi itaenda na raisi kama Biden, maana atawapotezea kura na wabunge kibao katika safari yake. Kama kuna uwezekano wa kumtoa watafanya hivyo.

Hao wanaofia madarakani Africa ni internal power struggle, mfano Mugabe ukiongea na wazimbabwe wanaofuatilia siasa zao. Watakwambia Mugabe alikuwa hoi muda mrefu yuko tayari kuachia nafasi, isipokuwa wale waliokuwa wanafaidika na uwepo wake ndio walikuwa wanambakiza madarakani.
 
Hata nape nauye na January makamba wamejiuzulu wadhifa wao wa waziri. πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…