Mmesoma hii barua ya CHADEMA kuomba msaada kutoka kwenye Bunge La Marekani kuhusu kesi ya Lissu? Wananchi mko wapi?

Mmesoma hii barua ya CHADEMA kuomba msaada kutoka kwenye Bunge La Marekani kuhusu kesi ya Lissu? Wananchi mko wapi?

Mahakama Kuu ya Tanzania imeagiza Mashahidi wa Kesi ya Uongo ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu Wafichwe na ushahidi wao uwe kama Amri kuu za Mungu.

Kesi
hiyo inayovunja rekodi ya Dunia kwa kuwa Kesi ya kwanza ya Uhaini inayomhusisha mtu mmoja Pekee ilichelewa kupelekwa Mahakama Kuu kwa vile Mtukufu Masaju ambaye ndio Mtunzi na mwanzilishi wa vifungu hivyo Tanzania, alitaka vipelekwe kwanza Mahakama Kuu vikapigwe Mhuri ili vimshughulikie Tundu Lissu.

Masaju akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye aliyebuni vifungu hivyo na kuvileta bungeni ambapo sasa akiwa Jaji Mkuu amevibariki Rasmi na kuirejesha Tanzania miaka zaidi ya 400 nyuma ambako Vifungu hivyo vya kijinga vilitumika.

Taarifa ya Chadema iliyosambazwa Duniani kote hii hapa

View attachment 3432247View attachment 3432248
Mungu yupo! Apandacho mtu ndicho atakachovuna. Wao wanaangalia uchaguzi tu. Ni sawa waende kwenye uchaguzi na kushinda kwa kishindo lakini hivyo viti wanavyokimbilia kwa gharama za damu za watu vitawatapika na watajuta kufanya hayo wanayofanya sasa! Time will tell.
 
Mungu yupo! Apandacho mtu ndicho atakachovuna. Wao wanaangalia uchaguzi tu. Ni sawa waende kwenye uchaguzi na kushinda kwa kishindo lakini hivyo viti wanavyokimbilia kwa gharama za damu za watu vitawatapika na watajuta kufanya hayo wanayofanya sasa! Time will tell.
Ndugu sasa ni kuchukua hatua, maana Mungu tunamuomba kila leo. Metal mada kasema Watanzania tumekatiwa tamaa, kutegemea nguvu yetu ni kazi bure
 
Pia CHADEMA wapinge ili la kuwaficha watoto sura zao wakati wakitoa ushahidi. CHADEMA tukiingia madarakani hamna cha sheria wala nini ,tutafuata kauli na msimamo wa mwenyekiti basi.

..kwani wanaokwenda kutoa ushahidi dhidi ya Tundu Lissu ni watoto kiasi cha kulazimisha kuwaficha?
 
Wakuu

Nadhani kama wanachi tunatakiwa kujitafakari sana. Kwenye hii barua ni kama CHADEMA wamekata tamaa kwenye kuwategemea wananchi.

Mwishoni huku wamesema wanaomba Bunge la Marekani na Jumuiya za Kimataifa kuangalia kwa ukaribu what is going on kuhusu kesi ya Tundu Lissu.

Yaani ni kama wamegive-up kuhusu nguvu ya umma. The last hope they have ni international community.

Wananchi kuna haja ya kujitafakari.

===============================

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani uamuzi wa Mahakama Kuu kuruhusu mashahidi wa upande wa mashtaka dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Antiphas Lissu, kuficha utambulisho wao kwenye kesi ya uhaini.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, chama hicho kimesema hatua hiyo inakiuka haki za kikatiba za mshtakiwa kupata taarifa kamili za mashahidi na ushahidi dhidi yake pamoja na haki ya kuwahoji mashahidi hao.

CHADEMA imesema utaratibu wa ushahidi wa siri unaathiri uhuru wa mahakama na kugeuza mahakama kuwa chombo cha ukandamizaji badala ya ulinzi wa haki, na imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa ikiwemo Bunge la Mareakani pamoja na mashirika ya haki za binadamu kufuatilia mwenendo huo wa kisheria nchini Tanzania.

View attachment 3432234

View attachment 3432235
Kaa mbali na ya chadema mkuu, ni ushauri tu
 
Uzuri tunawajua mashahidi wanaolengwa kufichwa, ni Freeman Mbowe na genge la wafuasi wake aliowatanguliza Chaumma, kila ubaya utalipwa hapa hapa duniani.
Walete ushahidi uliojitosheleza ndiyo jambo la msingi
 
Chadema inajipa umuhimu kwa wananchi wasiotaka huo umuhimu wao.

Huwezi jifanya unapigania watu wasiotaka kupiganiwa.

Na pia ugomvi wa Lissu na chama tawala ni ugomvi wa wanasiasa wananchi sioni kama unawahusu acha wanasiasa wapigane vile wao wanavyoweza na wanavyoona wao.
Mwanasiasa ni yupi na mwananchi ni yupi?
 
Hapa siungi mkono.

Trump ni chizi sijui kama atawajibu
 
Maisha haya duh leo mtu anataka kupitisha mauongo yake ili aihukumu vibaya nafsi ya mtu ambae hana kosa zaidi ya mapenzi yake mema na hili taifa. Lakini mwisho wa yote sisi watanganyika ni kima wasio jitambua. Enough is enough sasa tokeni mtaan mkapiganie haki zenu chadema mpo wapu
Wewe sio Mtanganyika ?
 
Hakuna kesi hapo, nikupotezeana muda,uhaini upi?? Mtapata laana na Lissu atashinda.
 
Back
Top Bottom