Mmezipata habari za ChatGPT? Automation inatishia ajira za watu

Mkuu..nitatakiwa kulipia?
Naona kuna malipo ya wiki na ya mwezi
 
Inafanyaje kazi mkuu.
Thesis unawezaje kuandaliwa kirahisi hivyo!
Google chatgpt then fanya simple registration, hii kitu ina human level conversation, cheza nayo utaielewa au ingia youtube utaelwa zaidi
 
Unawezaje ku detect kama content imekuwa generated na AI model kama ChatGPT?
 
Nimejaribu hii kitu na kiukweli kwa mara ya kwanza tekinolojia imenifanya nitafakari sana. Maana inaenda kubadilisha vitu vingi. kwa mfano.

1. Itafanya wanadamu tuwe lazy...hii ngoma inafanya kila kitu mtu anachoweza kuandika na kwa ufasaha. Kwa mgano juzi nilikuwa nataka kuandika cover letter...ambayo kiuhalishia ingenichukua kama 1 hr kupangia lugha na content...lakini ngoma hii iliniandika kwa dk 1. Niliedit tu mstari mmoja..ili kila kitu fresh.

2. Itapunguza ajira. Hizi kazi za consultancy na nyingine kama hizo nyingi zitapungua. Maana hii ngoma ni consultant anaye jua kila kitu.

3. Mashuleni na vyuo inabidi wabadilishe mfumo wa ku asses wanafunzi. Kwa mfano hizi homework/group work zitakuwa hazina maana tena. May be sasa inabidi ziwe complex localized scenario ambayo chatgpt haiwezi kuwa na majibu yote..lakini bado inaweza kusaidia kukupa idea za ujumla.

Hizi research za masters na PhD inabidi kutafuta mfumo mwingine. Otherwise ngoma itaandika thesis na mwanafunzi ku submit. Na cha ajabu haifanyi plagarise.
 
Kwa bahati mbaya hatuna wanafunzi ambao ni smart. Wengi wataishia ku_copy na ku_paste kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…