Mmezipata habari za ChatGPT? Automation inatishia ajira za watu

Mmezipata habari za ChatGPT? Automation inatishia ajira za watu

Unawezaje ku detect kama content imekuwa generated na AI model kama ChatGPT?
OpenAI (walotengeneza chatGPT) walisema wako mbioni kutengeneza software itakayo detect maneno ya aina hio.

Kuna kizazi cha mambulula kinakuja kutokea hapa, sijui tu. Ila bora walio na real & deep knowledge wawe wachache coz kwa sasa duniani fujo sana kisa ujuzi mwingi
 
Kwa bahati mbaya hatuna wanafunzi ambao ni smart. Wengi wataishia ku_copy na ku_paste kila kitu.
Mambulula watajaa sana mitaani na duniani kwa ujumla, Innovation itafikia muda isimame, watabaki wachache sana wenye uelewa wa namna mambo yanavyofanya kazi. Kwa namna hii unategemea kweli mtu aje ajifunze coding wakati chatGPT anaandika hadi snippets? Inafikirisha sana
 
Nilichogundua humu watu wengi wapo against Technology Innovation. Roughly 80%wapo against chatgpt. Mfano nimeona mdau anasema kuwa programmers watakuwa lazy sababu chatgpt inakuandikia code zote.. mnachopaswa kuelewa ni kwamba AI imekuja kufanya maisha yetu yawe rahisi. Kama nilikuwa natumia wiki kufanya project ya kutengeneza system au mobile app then naweza kufanya kwa muda mfupi sana sasa sio jambo zuri kweli [emoji780]
 
Nimejaribu hii kitu na kiukweli kwa mara ya kwanza tekinolojia imenifanya nitafakari sana. Maana inaenda kubadilisha vitu vingi. kwa mfano.

1. Itafanya wanadamu tuwe lazy...hii ngoma inafanya kila kitu mtu anachoweza kuandika na kwa ufasaha. Kwa mgano juzi nilikuwa nataka kuandika cover letter...ambayo kiuhalishia ingenichukua kama 1 hr kupangia lugha na content...lakini ngoma hii iliniandika kwa dk 1. Niliedit tu mstari mmoja..ili kila kitu fresh.

2. Itapunguza ajira. Hizi kazi za consultancy na nyingine kama hizo nyingi zitapungua. Maana hii ngoma ni consultant anaye jua kila kitu.

3. Mashuleni na vyuo inabidi wabadilishe mfumo wa ku asses wanafunzi. Kwa mfano hizi homework/group work zitakuwa hazina maana tena. May be sasa inabidi ziwe complex localized scenario ambayo chatgpt haiwezi kuwa na majibu yote..lakini bado inaweza kusaidia kukupa idea za ujumla.

Hizi research za masters na PhD inabidi kutafuta mfumo mwingine. Otherwise ngoma itaandika thesis na mwanafunzi ku submit. Na cha ajabu haifanyi plagarise.
Sio kweli kwa sababu mkiitumia wote kazi zenu zitafanana
 
Hii kitu ni nzuri, lakini ina hatari ya kufanya watu kuwa wajinga zaidi, sababu people will no longer store information in their heads; they will always rely on asking AI what to do. So, tutakuwa na wasomi wengi ambao vichwa ni vyeupe sababu wanajua watapata majibu kutoka kwa AI, hivyo watu watakosa kujiongeza kutafuta maarifa na taarifa kutoka vyanzo mbalimbali.

Japokuwa, uzuri wa hii kitu inasaidia sana kwenye automation ya task, mfano nimeitumia kufanya debug ya code na imenionyesha bugs ziko wapi ndani ya sekunde chache na nikaiambia iandike upya hizo code ikafanya hivyo tofauti na ambavyo ningechukua muda kuanza to go through codes kupata solution.

Kwangu mimi tunapaswa kufungua macho zaidi kuiona hii kama opportunity ya kutuwezesha kutengeneza products bora ambazo zitaunganishwa na AI ili kuweza kuchakata taarifa na kutoa suluhisho kwa changamoto za jamii yetu. Tusiitazame AI kama threat ila oppotunity.

Mfano 1: Nilijaribu kutumia AI kutuma picha ya jani la mimea ambao una magonjwa kati ya mimea 10 kwa magonjwa tofauti iliweza kunipa majibu sahihi kwa magojwa 7.

2. Nikajaribu kuweka picha ambayo iko na idadi tofauti tofauti ya watu na kuuliza kuna watu wangapi kwenye hizo picha ikanipa majibu sahihi kwa picha 5 kati ya 10.

3. Nikaweka picha nyingine ya watu wakiwa wanafanya action tofauti tofauti na ikanipa majibu sahihi kwa picha 4 kati ya 10

4. Nikaweka picha 10 za wanyama tofauti na kuiuliza ni mnyama gani ilinipa majibu sahihi kwa picha 6

Sasa kutokana na mifano hiyo niliweza kujifunza kuwa as much as ambavyo wanaendelea kuifundisha AI itakuwa bora zaidi na tutafika wakati ambapo tutaweza kutengeneza solution ambazo zita_automate task kwenye kila sekta.

Ukifikiri nje ya box kama wewe ni mfuatiliaji wa technology au uko na interest kwenye development ya products mbalimbali kuhusu technology utakuwa umepata idea nyingi sana za namna gani ya kuunganisha AI kwenye product zako.

Nimalizie kwa hili kwenye moja ya interview ambayo Elon Musk alikuwa na Jack Ma alisema watu wanafikiri kuwa nuclear ni hatari kwa ulimwengu, lakini AI ni hatari kubwa kuliko nuclear kwa kuwa siku za mbele zitatengenezwa silaha ambazo zinauwezo wa kujiamulia nini cha kufanya bia kupata instructions kutoka kwa mtu.
Watu wengi wanasema watu watakuwa lazy kwani kuna tofauti gani na mtu kusoma kitabu? Mwingine anasoma anahifadhi kichwani mwingine anasoma anasahau...hivyo hivyo mwingine ataiuliza ChatGPT atahifadhi kichwani na kuelewa concepts na mwingine atasahau na ataingia tena siku nyingine kutafuta.

Hapa tatizo sio technilogy tatizo ni uwezo wa mtu na mtu kuhifadhi na kuelewa mambo.
 
ChatGPT ni nzuri lkn ndio mwanzo na step nzr ya tech colonialism.

Wanaenda ku-cap knowledge ya watu. Duniani tutajazwa garbage na itafikia hatua kutakua na wataalam wachache saaana na hao watamilikiwa na mamlaka zilizolenga kufaidika na huu ukoloni, kwangu chatGPT ni kama game tu au assistant, naipaga movies nnazopenda then inanipa suggestions kutokana na taste zangu, na pia kwa sababu napenda Ancient chinese poetry huwa naiambia initungie poems kwa style za kina Zhuge Liang, Cao Cao etc..... Ila hata siku moja siwezi fanya kitu serious na chatGPT.

In simple terms hii AI model imetrainiwa kutokana na data watu walizoandika mitandaoni toka enzi zile. Sasa kwa speed hii nmeona blog posts nying zimeanza kutumia hii AI generated content. Kwa maana hio in 2 to 5 years ChatGPT itakua inalearn kutumia 'its own output' coz ndo zitakazokua zimejaa online kpnd hiko and trust me kama ushafanya AI development na ukajaribu kutrain model yako kwa output yake basi unafaham kiakachokukuta. Ni kama vile binadam uwe unakula nnya yako. Facebook na twitter wanajua vzr madhara ya hio kitu coz iliwatokea kwenye algos zao za newsfeed suggestion kpnd fln miaka ya nyuma.


Mitandao inayoendeshwa na akili kubwa kama StackOverflow wameshazuia hizo content kutoka ChatGPT
IT wa kibongo wengi maneno meengi ila products zenu hatuzioni..siku zote mnaibuka kwenye kukosoa vya wenzenu. AI ndio future labda kama bado umekariri. Hata umeme ulipogunduliwa kulikuwa na maneno mengi sana against kutoka kwa walioshindwa kuona mbali.
 
IT wa kibongo wengi maneno meengi ila products zenu hatuzioni..siku zote mnaibuka kwenye kukosoa vya wenzenu. AI ndio future labda kama bado umekariri. Hata umeme ulipogunduliwa kulikuwa na maneno mengi sana against kutoka kwa walioshindwa kuona mbali.
Okay
 
Nisaidieni jmn kwangu inakataa kufunguka
8663F63B-8109-4A44-8A6B-F7B01B77EFE5.png
 
Hii kitu nimekuwa nikicheza nayo kama week sasa, kwa kweli hii kitu iko vizuri sana na nimeipenda sana, nimeijaribu vitu vingi, niliiambia iandikie love letter to my x girlfriend, nikaiuliza iniambie kuhusu Julius Nyerere na inionyeshe speech yake ambayo ni muhimu sana , nikaiambie inifundishe calculus, nikaiambia iniandikie thank you note to my co worker, nikaiuliza kama inajua kiswahili, nikaimbia iandike short essay kumaliza umaskini Tanzania etc kwa kweli i was impressed na majibu yake na kila kitu chake, ni kama unaongea na binadamu mwenzako ambaye ni genius na ana majibu yote, ijaribuni then muweke matokeo hapa
Wapo kwenye mpango wa kuifanya kuwa ya kulipia
 
One thing that I know for sure, THEY WILL KEEP IMPROVING IT. Actually, wameiachia bure watu waitumie kwa sasa sio kwa lengo la kuwasaidia watu, au kuwafaidisha watu, bali wameiachia ili wajue mapungufu ya ChatGPT kabla hawajaiachia rasmi, pengine kwa mfumo wa App, au browser extension etc. Kwa lugha nyepesi, hivi sasa hii ChatGPT iko kwenye Beta version, bado wanaifanyia maboresho - na njia nzuri ya kujua mapungufu yake ni kuruhusu watu waitumie. Na kadiri watu wengi wanavoitumia ndivyo inavyozidi kuwa smart.

Binafsi naitumia kuandika baadhi ya code, then kazi yangu inabaki ku-edit baadhi ya vitu; and I am loving it!🥳 Wakati huo kule Discord kuna binamu anaitwa Midjourney - tunamtumia kutengeneza images - and it is jaw dropping epic!
Huyo midjourney ni balaa jingine... Just imagine na yeye anakupa uhalisia wa ukifikiriacho
 
Back
Top Bottom