Mmezipata habari za ChatGPT? Automation inatishia ajira za watu

Mmezipata habari za ChatGPT? Automation inatishia ajira za watu

Nimeona hizo screenshot, mbona naona ni kama dictionary tu
 
Hii kitu nimekuwa nikicheza nayo kama week sasa, kwa kweli hii kitu iko vizuri sana na nimeipenda sana, nimeijaribu vitu vingi, niliiambia iandikie love letter to my x girlfriend, nikaiuliza iniambie kuhusu Julius Nyerere na inionyeshe speech yake ambayo ni muhimu sana , nikaiambie inifundishe calculus, nikaiambia iniandikie thank you note to my co worker, nikaiuliza kama inajua kiswahili, nikaimbia iandike short essay kumaliza umaskini Tanzania etc kwa kweli i was impressed na majibu yake na kila kitu chake, ni kama unaongea na binadamu mwenzako ambaye ni genius na ana majibu yote, ijaribuni then muweke matokeo hapa
Ila hana taarifa za 2022 kuendelea.
Taarifa zake ni mwisho 2021

Sent from my 2201117TG using JamiiForums mobile app
 
Midjourney vs Dall - E unaichagua ipi? Maana Dall - E ni project ya OpenAI pia.
Ofcourse Dall-E inatengeza more realistic images kuliko Midjourney na Stable diffusion, generally. Dall-E inakimbiza.
 
ChatGPT ni nzuri lkn ndio mwanzo na step nzr ya tech colonialism.

Wanaenda ku-cap knowledge ya watu. Duniani tutajazwa garbage na itafikia hatua kutakua na wataalam wachache saaana na hao watamilikiwa na mamlaka zilizolenga kufaidika na huu ukoloni, kwangu chatGPT ni kama game tu au assistant, naipaga movies nnazopenda then inanipa suggestions kutokana na taste zangu, na pia kwa sababu napenda Ancient chinese poetry huwa naiambia initungie poems kwa style za kina Zhuge Liang, Cao Cao etc..... Ila hata siku moja siwezi fanya kitu serious na chatGPT.

In simple terms hii AI model imetrainiwa kutokana na data watu walizoandika mitandaoni toka enzi zile. Sasa kwa speed hii nmeona blog posts nying zimeanza kutumia hii AI generated content. Kwa maana hio in 2 to 5 years ChatGPT itakua inalearn kutumia 'its own output' coz ndo zitakazokua zimejaa online kpnd hiko and trust me kama ushafanya AI development na ukajaribu kutrain model yako kwa output yake basi unafaham kiakachokukuta. Ni kama vile binadam uwe unakula nnya yako. Facebook na twitter wanajua vzr madhara ya hio kitu coz iliwatokea kwenye algos zao za newsfeed suggestion kpnd fln miaka ya nyuma.

Mitandao inayoendeshwa na akili kubwa kama StackOverflow wameshazuia hizo content kutoka ChatGPT
Is it actually intelligent?Is it learning? Can it b creative? Au ni linakopi tu majibu ya data zilizokuwa fed kwake mtandaoni na kuzitapika kwa user?
 
Uzuri kama kitu hakajui au hakawezi kujibu kanakwambia! 🤣 🤣 🤣 Kako humble, and I like that!

Screenshot 2023-01-15 145228.png
 
Open AI ilianzishwa na watu wanne; Sam Altman, Ilya Sutskever, Wojciech Zaremba na Elon Musk. Japo alijiuzulu kutoka kwenye bodi mwaka 2018 kuondoa mgongano wa maslahi. Lakini generally bado yupo karibu na team ya Open AI.
Hivi tunaposema elon Musk ameanzisha kitu fulani, huwa tunamaanisha aliingia na spana na Nyundo akakaa na PC kwenye garage yake kucode, ...au anakuta watu wameshaanza ila hawana hela, anaiskiliza pitch ya biashara anamwaga mpunga kama early investor au??
 
Well, vyovyote iwavyo; Co-Founders wana majukumu tofauti. Startup inapoanza sio wote watakuwa washika nyundo au PC. Na sio wote huwa wanaweka mtaji. Kwahiyo Co-Founder ni Co-Founder kwasababu alishiriki katika shughuli za mwanzoni kabisa za kampuni.

Huwezi kusikia Elon Musk anaitwa Founder au Co-Founder wa Tesla kwasababu hakushiriki mwanzo wakati Tesla inaanza, ila yeye ni Angel investor wa Tesla.

Kwahiyo mimi nadhani tunaposema mtu fulani ni mwanzilishi au mwanzilishi mwenza wa kitu fulani ni kwasababu alishiriki wakati kitu hicho kinaanzishwa, iwe ni kwa hali au ni kwa mali. Naomba kusahihishwa kama nimechochora.
 
AAAgh mbona Elon mwenyewe anapendaga kujiita Tesla Co- founder
Anasemaga aliikuta Tesla with nothing but drawings on a paper
 
AAAgh mbona Elon mwenyewe anapenaga kujiita Tesla Co- founder
Anasemaga aliikuta Tesla with nothing but drawings on a paper
Well, wenyewe wanaita "Bragging rights"... hata Palamagamba Kabudi aliwahi kusema aliokotwa majajalani... haimaanishi kweli alikuwa jalalani akateuliwa kuwa Waziri la hasha, bali anajaribu kuelezea hali ilivyokuwa kabla hajawa hapo alipo.

Kujiita yeye ni Co-Founder kwasababu alikuta hawajapiga hatua yoyote ina-make sense; hiyo ni bragging right yake - kwasababu kama ni Angel investors wako wengi lakini Angel investors walioweza kuzitoa kampuni zao majalalani na kuzifikisha kwenye kilele cha mafanikio wanahesabika. Acha wajigambe, wanastahili!
 
CHATGP inamuelekeo mzuri na itateka na kuangusha baadhi ya mifumo ya utafutaji content kwenye mtandao japo kwa sasa bado siwezi kusema sana ila bado kufika huko.....
Inakupa kila kitu kwa jinsi unavyo hitaji katika mpangilio unao hitaji na kwa % kubwa, hata ukitaka ikuandikie simple program ,Thesis, blog content etc inakufanyia.
Ukitaka kujua bado ina mapungufu copy content ya kingereza iambia itransilate kwenda kwenye kiswahili utaona makosa mengi.
CHATGP yasasa as on Jan 2023 ina info kuanzia Dec 2021 kurudi nyuma na info zote Jan 2022 todate hazipo.Bado kwenye majaribio na wana mpango wa kuweka mpya ambayo iko improved zaidi soon.
Nafurahi kuwa kati ya watu wa kwanza TZ kuitumia Last year 2022 todate[emoji4]
Mbona kwenye app store haipo..?? Inapatikana wap ??
 
ChatGPT iko vizuri sana, nina wazo kama kuna mtanzania ana pesa basi awekeze katika kutengeneza AI ya ya kibongo means mtu akitaka kupata usaidizi wa jambo lolote anaingia anachat na robot
 
Back
Top Bottom