Mmezipata habari za ChatGPT? Automation inatishia ajira za watu

Unawezaje ku detect kama content imekuwa generated na AI model kama ChatGPT?
OpenAI (walotengeneza chatGPT) walisema wako mbioni kutengeneza software itakayo detect maneno ya aina hio.

Kuna kizazi cha mambulula kinakuja kutokea hapa, sijui tu. Ila bora walio na real & deep knowledge wawe wachache coz kwa sasa duniani fujo sana kisa ujuzi mwingi
 
Kwa bahati mbaya hatuna wanafunzi ambao ni smart. Wengi wataishia ku_copy na ku_paste kila kitu.
Mambulula watajaa sana mitaani na duniani kwa ujumla, Innovation itafikia muda isimame, watabaki wachache sana wenye uelewa wa namna mambo yanavyofanya kazi. Kwa namna hii unategemea kweli mtu aje ajifunze coding wakati chatGPT anaandika hadi snippets? Inafikirisha sana
 
Nilichogundua humu watu wengi wapo against Technology Innovation. Roughly 80%wapo against chatgpt. Mfano nimeona mdau anasema kuwa programmers watakuwa lazy sababu chatgpt inakuandikia code zote.. mnachopaswa kuelewa ni kwamba AI imekuja kufanya maisha yetu yawe rahisi. Kama nilikuwa natumia wiki kufanya project ya kutengeneza system au mobile app then naweza kufanya kwa muda mfupi sana sasa sio jambo zuri kweli [emoji780]
 
Sio kweli kwa sababu mkiitumia wote kazi zenu zitafanana
 
Watu wengi wanasema watu watakuwa lazy kwani kuna tofauti gani na mtu kusoma kitabu? Mwingine anasoma anahifadhi kichwani mwingine anasoma anasahau...hivyo hivyo mwingine ataiuliza ChatGPT atahifadhi kichwani na kuelewa concepts na mwingine atasahau na ataingia tena siku nyingine kutafuta.

Hapa tatizo sio technilogy tatizo ni uwezo wa mtu na mtu kuhifadhi na kuelewa mambo.
 
IT wa kibongo wengi maneno meengi ila products zenu hatuzioni..siku zote mnaibuka kwenye kukosoa vya wenzenu. AI ndio future labda kama bado umekariri. Hata umeme ulipogunduliwa kulikuwa na maneno mengi sana against kutoka kwa walioshindwa kuona mbali.
 
Okay
 
Wapo kwenye mpango wa kuifanya kuwa ya kulipia
 
Huyo midjourney ni balaa jingine... Just imagine na yeye anakupa uhalisia wa ukifikiriacho
 
Inafanyaje kazi mkuu.
Thesis unawezaje kuandaliwa kirahisi hivyo!
... ha ha ha! Hope kila kitu inamaliza including kui-defend! Vilaza na sisi tuchangamkie phd za burebure sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…