Mmezipata habari za ChatGPT? Automation inatishia ajira za watu

Nimeona hizo screenshot, mbona naona ni kama dictionary tu
 
Ila hana taarifa za 2022 kuendelea.
Taarifa zake ni mwisho 2021

Sent from my 2201117TG using JamiiForums mobile app
 
Midjourney vs Dall - E unaichagua ipi? Maana Dall - E ni project ya OpenAI pia.
Ofcourse Dall-E inatengeza more realistic images kuliko Midjourney na Stable diffusion, generally. Dall-E inakimbiza.
 
Is it actually intelligent?Is it learning? Can it b creative? Au ni linakopi tu majibu ya data zilizokuwa fed kwake mtandaoni na kuzitapika kwa user?
 
Open AI ilianzishwa na watu wanne; Sam Altman, Ilya Sutskever, Wojciech Zaremba na Elon Musk. Japo alijiuzulu kutoka kwenye bodi mwaka 2018 kuondoa mgongano wa maslahi. Lakini generally bado yupo karibu na team ya Open AI.
Hivi tunaposema elon Musk ameanzisha kitu fulani, huwa tunamaanisha aliingia na spana na Nyundo akakaa na PC kwenye garage yake kucode, ...au anakuta watu wameshaanza ila hawana hela, anaiskiliza pitch ya biashara anamwaga mpunga kama early investor au??
 
Well, vyovyote iwavyo; Co-Founders wana majukumu tofauti. Startup inapoanza sio wote watakuwa washika nyundo au PC. Na sio wote huwa wanaweka mtaji. Kwahiyo Co-Founder ni Co-Founder kwasababu alishiriki katika shughuli za mwanzoni kabisa za kampuni.

Huwezi kusikia Elon Musk anaitwa Founder au Co-Founder wa Tesla kwasababu hakushiriki mwanzo wakati Tesla inaanza, ila yeye ni Angel investor wa Tesla.

Kwahiyo mimi nadhani tunaposema mtu fulani ni mwanzilishi au mwanzilishi mwenza wa kitu fulani ni kwasababu alishiriki wakati kitu hicho kinaanzishwa, iwe ni kwa hali au ni kwa mali. Naomba kusahihishwa kama nimechochora.
 
AAAgh mbona Elon mwenyewe anapendaga kujiita Tesla Co- founder
Anasemaga aliikuta Tesla with nothing but drawings on a paper
 
AAAgh mbona Elon mwenyewe anapenaga kujiita Tesla Co- founder
Anasemaga aliikuta Tesla with nothing but drawings on a paper
Well, wenyewe wanaita "Bragging rights"... hata Palamagamba Kabudi aliwahi kusema aliokotwa majajalani... haimaanishi kweli alikuwa jalalani akateuliwa kuwa Waziri la hasha, bali anajaribu kuelezea hali ilivyokuwa kabla hajawa hapo alipo.

Kujiita yeye ni Co-Founder kwasababu alikuta hawajapiga hatua yoyote ina-make sense; hiyo ni bragging right yake - kwasababu kama ni Angel investors wako wengi lakini Angel investors walioweza kuzitoa kampuni zao majalalani na kuzifikisha kwenye kilele cha mafanikio wanahesabika. Acha wajigambe, wanastahili!
 
Mbona kwenye app store haipo..?? Inapatikana wap ??
 
ChatGPT iko vizuri sana, nina wazo kama kuna mtanzania ana pesa basi awekeze katika kutengeneza AI ya ya kibongo means mtu akitaka kupata usaidizi wa jambo lolote anaingia anachat na robot
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…